Tulonge

Leo bahati imemuangukia Mama Malaika.Cha kupendeza zaidi kesho anasheherekea siku yake ya kuzaliwa. Kama kawaida yetu unaruhusiwa kumuuliza swali,kumpa ushauri,kumpa sifa,kutoa lalamiko kwako n.k. Uwanja ni wako mdau

Views: 826

Replies are closed for this discussion.

Replies to This Discussion

Kazi unayo mama,lazima nirudi hapa kukukandamiza maswali
Hahahaaa.. Wahenga walisema "usitukane mamba kabla hujavuka mto" lol.. kumbe ulikuwa kimya kwasababu ulikuwa njiani eee? Karibu ulingoni Mama...
Hongera mama malaika kupata nafasi hii tunataraji kujifunza mengi kutoka kwako na pia nawe utajifunza mengi kutoka kwa wadau wa safu hii ya mdau wa wiki.Tunakutakia kila la kheri katika siku yako ya kuzaliwa hapo kesho mungu akuafikishe kuifikia ili tusherehekee sote.Hivi unafikisha miaka mingaapi vile? Na una familia au huna na kama unayo inawatoto wangapi?Na mtoto wa kwanza ana umri gani.Ni hayo tu kwa kukukaribisha, mengi yatafuata hapo baadae, Mama malaika umekuwa Malaika wetu wiki hii congratulation again and again.
Ngoja nirudi safari Jumatatu...mswali yako mama yapo yamejaa debe na usichomoe jibu hata moja!!  hongera!!

Asante sana Riziki. Ni kweli usemayo wote kila mmoja wetu anajifunza toka kwa mwezie (each one teach one). Na asante sana kwa pongezi za kuzaliwa. Namshukuru Mungu kaweza kunifikisha hadi siku ya leo, na kesho Jumamosi nitatimiza miaka 41. 

Kuhusu swali lako la familia, nimeolewa na nina watoto wawili. Mtoto wangu wa kwanza ni binti wa miaka 7 aitwa Malaika

riziki matitu said:

Doh! hongera sana mama kwa kuwa mdau wa week ngoja nikayachakachuwe kwa nia nzuri maswali yangu kisha nitarudi ila nawaasa wanakijiji tupunguze ukali wa maneno kutokana m2 tunaemuuliza maswali ni MAMA hivyo tuwe na maswali yenye busara na hekima tutajifunza mengi toka kwake kwani natumae mpaka kufikia umli huo kaona mengi sana, KARIBU MAMA utujuze.

Ha ha aaahaaaa..... Dixon shauri yako, mama atakunyima bigijiii akija.

Asante sana Dixon kunikaribisha

Dixon Kaishozi said:

Hahahaaa.. Wahenga walisema "usitukane mamba kabla hujavuka mto" lol.. kumbe ulikuwa kimya kwasababu ulikuwa njiani eee? Karibu ulingoni Mama...

Haya nakusubiri ila usinishindilie maswali mengi. LOL.....

Severin said:

Kazi unayo mama,lazima nirudi hapa kukukandamiza maswali
Haya weye... mama anakusubiri kwa hamu

Gratious Kimberly said:
Ngoja nirudi safari Jumatatu...mswali yako mama yapo yamejaa debe na usichomoe jibu hata moja!!  hongera!!
mama kwanza shikamoo, natumaini baba na wadogo zangu hawajambo. mama mimi swali langu nataka tu kujua maoni yako kuhusu tiba ya babu wa loliondo vipi unaichukuliaje ingawa uko mbali na  je huyu babu angeibukia birmingham city vipi angelipata wateja?
AH mama malaika kweli kazi unaiweza naona umeanza kwa kasi ya umeme lkn sio ule wa dowans na TANESCO.Nashukuru kwa majibu yako mazuri na hongera kwa kuwa na familia yenye upendo.Mungu akubaliki sana na tutaendelea kukuhoji maswali kadri siku zinavyokwenda

Mama Malaika said:

Asante sana Riziki. Ni kweli usemayo wote kila mmoja wetu anajifunza toka kwa mwezie (each one teach one). Na asante sana kwa pongezi za kuzaliwa. Namshukuru Mungu kaweza kunifikisha hadi siku ya leo, na kesho Jumamosi nitatimiza miaka 41. 

Kuhusu swali lako la familia, nimeolewa na nina watoto wawili. Mtoto wangu wa kwanza ni binti wa miaka 7 aitwa Malaika

riziki matitu said:

Hongera mama malaika kupata nafasi hii tunataraji kujifunza mengi kutoka kwako na pia nawe utajifunza mengi kutoka kwa wadau wa safu hii ya mdau wa wiki.Tunakutakia kila la kheri katika siku yako ya kuzaliwa hapo kesho mungu akuafikishe kuifikia ili tusherehekee sote.Hivi unafikisha miaka mingaapi vile? Na una familia au huna na kama unayo inawatoto wangapi?Na mtoto wa kwanza ana umri gani.Ni hayo tu kwa kukukaribisha, mengi yatafuata hapo baadae, Mama malaika umekuwa Malaika wetu wiki hii congratulation again and again.

Marahaba Chaoga. Baba na wadogo zako wote wazima.

Kuhusu swali lako la Loliondo, nimesikia na ninasubiria miezi 12+ ipite kuona athari/faida zake maana babu wa Loliondo sio wa kwanza kwani kumeshatokea hadi watoto wadogo miaka ya zamani huko Mwanza, Shinyanga, etc. na baadae wakatoweka. Tanzania iko sub Sahara Africa ambako ndiko kumeathirika sana na HIV/AIDS, serikali inapasa kushirikiana moja kwa moja na babu wa Loliondo ili kuhakikisha wagonjwa wa HIV/AIDS wanaendelea kunywa dose zao wanazopewa toka clinics za kuongeza nguvu.

Chaoga kusema ukweli huyo Babu wa Loliondo angeibukia Birmingham City siajabu angeishia Mahabusu/Jela na tungemsahau sababu nchi hii wanajali sana mambo ya health and safety. Na sio kwenye dawa peke yake bali kila kitu. Britain huruhusiwi kutoa dawa bila ya kibali cha serikali, kila dawa inayotolewa kwa binadamu au wanyama lazima ifanyiwe utafiti wa kisayansi wa muda mrefu ili kujua kama ina madhara. Na dawa zote zinatolewa kwa wagonjwa lazima cheti (prescription) kitoke kwa Doctor. Waenda kwa Doctor wako (Family Doctor) au yeye anakuja nyumbani kwako kukuona/kukupima na kukuandikia cheti cha dawa kutokana na ugonjwa ulionao, baada ya hapo ndio waenda Pharmacy na hicho cheti kununua/kupewa dawa iliypandikwa kwenye cheti na sio zaidi ya hapo.

chaoga said:

mama kwanza shikamoo, natumaini baba na wadogo zangu hawajambo. mama mimi swali langu nataka tu kujua maoni yako kuhusu tiba ya babu wa loliondo vipi unaichukuliaje ingawa uko mbali na  je huyu babu angeibukia birmingham city vipi angelipata wateja?

RSS

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*