Tulonge

Leo bahati imemuangukia Mama Malaika.Cha kupendeza zaidi kesho anasheherekea siku yake ya kuzaliwa. Kama kawaida yetu unaruhusiwa kumuuliza swali,kumpa ushauri,kumpa sifa,kutoa lalamiko kwako n.k. Uwanja ni wako mdau

Views: 822

Replies are closed for this discussion.

Replies to This Discussion

Ha haaa ahaaa... we mwana ntamwambia baba yako akunyime pocket money.

riziki matitu said:
AH mama malaika kweli kazi unaiweza naona umeanza kwa kasi ya umeme lkn sio ule wa dowans na TANESCO.Nashukuru kwa majibu yako mazuri na hongera kwa kuwa na familia yenye upendo.Mungu akubaliki sana na tutaendelea kukuhoji maswali kadri siku zinavyokwenda

Mama Malaika said:

Asante sana Riziki. Ni kweli usemayo wote kila mmoja wetu anajifunza toka kwa mwezie (each one teach one). Na asante sana kwa pongezi za kuzaliwa. Namshukuru Mungu kaweza kunifikisha hadi siku ya leo, na kesho Jumamosi nitatimiza miaka 41. 

 

Kuhusu swali lako la familia, nimeolewa na nina watoto wawili. Mtoto wangu wa kwanza ni binti wa miaka 7 aitwa Malaika

 

riziki matitu said:

Hongera mama malaika kupata nafasi hii tunataraji kujifunza mengi kutoka kwako na pia nawe utajifunza mengi kutoka kwa wadau wa safu hii ya mdau wa wiki.Tunakutakia kila la kheri katika siku yako ya kuzaliwa hapo kesho mungu akuafikishe kuifikia ili tusherehekee sote.Hivi unafikisha miaka mingaapi vile? Na una familia au huna na kama unayo inawatoto wangapi?Na mtoto wa kwanza ana umri gani.Ni hayo tu kwa kukukaribisha, mengi yatafuata hapo baadae, Mama malaika umekuwa Malaika wetu wiki hii congratulation again and again.
Haya Omary nakusubiri.. ukirudi utakuta na ice cream nshakuandalia. Ha aha ahaaaaa

Omary said:
Doh! hongera sana mama kwa kuwa mdau wa week ngoja nikayachakachuwe kwa nia nzuri maswali yangu kisha nitarudi ila nawaasa wanakijiji tupunguze ukali wa maneno kutokana m2 tunaemuuliza maswali ni MAMA hivyo tuwe na maswali yenye busara na hekima tutajifunza mengi toka kwake kwani natumae mpaka kufikia umli huo kaona mengi sana, KARIBU MAMA utujuze.

yehoo! haya mama nimesharudi ice cream yangu pls mama lol

1 nimefurahi umeshanijibia wasali langu la kwanza umli

2 hebu tuambie myaka ileee uliokulia ww na hii yetu cc unaonaje?

3 unatushauli nini? vijana i mean umekutana na Omary,Dis,Chaoga unataka umuas ungemwambia afanye nn?

ili awe mtt mwema na mwenye mafanikio?

4 unafikiri kiongezwe nn? ili tulonge ipige hatuwa?

5 ww tungekupa nafasi ya JK wa sasa ungefanya nn? kinachokukera?

6 tz kunavijana wengi hawana ajira wanakaa mitaani wanavuta bangi na kunywa pombe za gongo,mnazi nk wakikuona ukipita wanaomba 500, 200 hayo ndio maisha yao wamekata kabisa tamaa je wa2 hawa ukikaa nao chini utawaambiaje? japo swali hili linashabiana na la namba 3

7 sehem kubwa ya TZ imezunguukwa na mapori na hatuna faida nayo au niseme tunavyanzo vingi sana je ungekuwa muheshimiwa ungetafuta wawekezaji wawekeze kwenye nn? 

8 TZ inawatoto yatima wengi sana wanalelewa katika vituo na mitaani watt hawasomi wanaishi kwa kuomba omba

je unafikiri wakiwa wakubwa watafanya kazi gani? unaishauli nn? selikari ya tz? kuhusu watt hawa?

mwisho naomba umshauri Dismas aowe umli unaenda anazeeka sasa ila me simo mwambie mwenyewe usinitaje pls lol. nikikumbuka swali usinichoke nitarudi.

 

Shkamoo mama. Nakupongeza sana kwa kupata nafasi hii adimu na adhimu ya kuwa mdau wa wiki. Pili, nakutakia siku njema ya kuzaliwa kwako, na maisha marefu zaidi yaliyojaa furaha, amani na mafanikio. Na tatu, kwa kuwa wewe ni mama mkwe wangu naomba nioneshe heshima kwa kutokuuliza maswali.

  Happy birthday Dada! Hongera  dada kwa kuchaguliwa kuwa mdau wa week!

Maswali yangu ni kama yafuatavyo;

1. Hobbie zako?

2. Top ten ya vyakula uvipendavyo. Vinywaji pia, matunda?

3. Nchi/Mji unayoipenda/unaoupenda bila kutaja nchi yako.

4. Mcheza filamu maharufu unaempenda (actor and actress)

5. Filamu (Movie) gani ambayo unaipenda na unaweza kuangalia tena na tena bila kukuchosha!

6. Tabia uliyoizoea ambayo huwaudhi ndugu na marafiki.

7. Ndoto yako na mategemeo yako hivi karibuni?

8. Jambo ambalo umejifunza nje ya nchi ambalo ungefurahi kuwafundisha wananchi wenzako.

9. Jambo ambalo linakuudhi na halikupi amani yako ughaibuni.

10. Una maoni gani kuhusu viongozi wa sasa nchini Tanzania?

  Hayo ni maswali yangu...naomba uwe na uhuru wa kujibu au kutojibu swali/maswali lolote/yoyote.

Nakutakia kila la heri katika maisha yako kwa ujumla. Be blessed ...hugs!!

Mama naomba majibu ya maswali haya:-

1. Nitajie mlikutana wapi na Baba Malaika kwa mara ya kwanza. Je alipoanza kukusumbua alituma mtu au alikuja mwenyewe?

2.Ndugu zako (hasa wazazi) walikuchukuliaje kuwa na mahusiano na mzungu? Walikubaliana moja kwa moja bila kikwazo?

3.Hakuna ubaguzi wowote huko UK hasa katika Mazingira ya kazi na mtaani? mfano ubaguzi wa rangi.

4.Unaizungumziaje tulonge,unamshauri nini admin wa Tulonge?

Hello Mama yetu mpendwa! Kwanza hongera kwa siku yako ya kuzaliwa.. Mungu akuzidishie maisha marefu na hekima wewe pamoja na familia yako.. Kwani Baba Malaika anamchango mkubwa kama baba wa familia kwa upendo wake kwako kuwafikisha hapo mlipo.

Pili kwa wenzangu walio ttangulia kuuliza maswali mazuri na washukuru pia kwani wamesaidia sis wengine kujua yale ambayo kwa njia moja au nyingine tusinge yafahamu.. Asante kwa majibu mazuri.

 

Mimi kwa upande wangu nina haya...

(1). Ulikutana vipi na Baba malaika ?

(2). Familia yako (wazazi na ndugu zako wengine ) walichukuliaje utambulisho wa baba malaika?

(3) Kwenu wewe ni mtoto wa ngapi na familia yenu kwa ujumla mpo wa ngapi ?

(4). Kuishi kwako NJE.. unatoa mchango gani kwa wale ulio waacha nchini kwako

(5). Tunatambua umuhimu wako ndani ya kijiji hiki kwa ushauri, ucheshi na mchango wako kwenye hii jumuia.. Unasemaje kwenye suala la katiba ya nchi yetu.. una maoni gani juu ya hii katiba ya sasa na katiba ijayo ?

yale utakayopenda kujibu nitashukuru.. mengine kama ni (personal) pia unaweza kupotezea.. lol

 

kwa sasa niachie hapa upate mda wa kutujibu wakati mengine yanakuja.. Nakutakia siku njema na hongera tena kuwa mdau wetu wa wiki. PamoJah

Mama hongera kwa kuwa mdau wa wiki. Haya nipe siri ya uzuri wa nywele zako.Huwa nazitamani sana

Mama Malaika kwanza shikamoo, pili hatumai wadogo zangu na baba wote hawajambo na ww pia........

nashukuru kukuta hujatolewa kwenye ukurasa wa mdau wa wiki coz i was out of my office attending others official duties.......

me sina maswali mengi coz kama mwanao sina sababu ya kuuliza sana naogopa fimbo zinaumaaa uwiii,

1.me nlitaka kujua huko uliko unafanya shughuli gani haswa?

2.je una mchango wowote wa mawazo,ushauri,nasaha nk kwa vijana wa kijiji cha tulonge kama kina chaoga,omar,alfan,dis,diana,jaq,hilda na wengineo,ukipewa nafasi ya kuwapa usia utawapa maneno gani?

3.una mpango gani na maisha ya wadogo zangu huko baadae?

4.ni kitu gani ktk dunia hii kinakufurahisha sana apart from ur family

5.nini mawazo juu ya kuinua tasnia ya michezo hapa tz? maana kila siku hatufanyi vzr ktk michezo ya kimataifa.

6.nini mchango juu ya HIV/AIDs in tanzania?

 

nikutakie siku njema wape hi wadongo zangu waambie kaka yao anawasalimu sana.

7.

Mimi nina swali,,,

Mchakato gani ulio wahi kupambana nao na uto usahau maishani mwako?

Ni hilo tuu dada ake

Kwa heshima na tahadima napenda kukupngeza kwa siku ya ko ya kuzaliwa

Kwnza hongera kwa siku ya kuzaliwa. Swali linakuja, jiandae kukusanya data.

PamoJah

Wadau msishangazwe na ukimya wa Mama Malaika,nadhani atakuwa ametingwa na majukumu ya kikazi. Aliniachia ujumbe ufuatao kwenye page yangu:-

"Yaani Dismas umenikomoa kweli kweli... mwenzio nimekuweko Namibia na Botswana kikazi wiki hii yote. Sasa niko Johannesburg (OR Tambo intern. airport) na dakika 30 zijazo naondoka na BA kurudi London. Hivyo maswali yote ya wadau watanisamehe hadi Jpili au Jtatu maana nawasili kesho asubuhi na nduguzo hawatoniachia hata kidogo hii weekend kwani niliwaacha na baba yao."

 

Ngoja tumvutie subira hadi kesho ili ajibu maswali aliyoulizwa.

RSS

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*