Tulonge

Michango ya harusi INANIKERA kweliiiiiiii.

Michango ya harusi ni moja kati ya vitu VINAVYONICHEFUA katika maisha yangu kwa sasa. Imekuwa ni kitu cha kawaida kwa watu kuchangisha wenzao pindi wanapotaka kuoa.Kwa nini usumbue wenzako kwa kutoa hela ambayo hawajapangia kwa starehe yako binafsi? Kwani ni lazima kafanya sherehe kubwa,unatakiwa ufanye sherehe unayoweza kuigharamikia mwenyewe bila kisumbua mtu then alika watu wachache tu.

Hapo hapo ukiwaambia watu wamchangie mgonjwa aliye mahututi hospitali watakuona waajabu sana. Mimi naona huwa tunatoa hela za harusi kinafiki (tunaogopa lawama) lkn si kutoka moyoni. Hata kama ni kutoka moyoni mimi sioni haja ya kuchangiana kwenye harusi pamoja na sherehe nyingine zisizo na lazima. Mtu asije akaniambia nimchangie harusi,nitamshushua hadi akome.

Wewe unaonaje?

Views: 920

Reply to This

Replies to This Discussion

Kumbe wengi mnaichukia,nilidhani nipo mwenyewe hahahahahaa.Milikua mnaogopa kulianzisha?

Lahasha ...Belita hapa sikubaliani nawe, si kwamba tunaogopa, ni kwamba halijatupitia kichwani kulianzisha hapa! Kama mtu angeogopa asingetoa wala maoni kwa kuogopa  kulaumiwa. Najua kuna wengi kati yetu hawakubaliani nawe na wana haki zote za kutoa maoni yao.

 

 

Hahahahahaa mkuu Eddie umenifurahisha sana,kidume hakiogopi kulianzisha au c o?

eddie said:

Lahasha ...Belita hapa sikubaliani nawe, si kwamba tunaogopa, ni kwamba halijatupitia kichwani kulianzisha hapa! Kama mtu angeogopa asingetoa wala maoni kwa kuogopa  kulaumiwa. Najua kuna wengi kati yetu hawakubaliani nawe na wana haki zote za kutoa maoni yao.

 

 

kwa kweli hauko peke yako hata mie inaniboa sana tu

Huenda wakristo tunaiga kanisani mambo ya sadaka! Toa ndugu ulochonacho....lakini hii ya kukupangia mtu utoe kiasi gani ...

noma!

Severin said:

Huu upuuzi huwa siupendi kwelii. Huwa naona noma kusema pindi ninapopewa kadi. Ila inarudisha nyuma maendeleo ya watu na inasababisha kuonana wabaya pindi unaposhindwa kutoa mchango. Mimi mtu aandae sherehe kwa gharama zake halafu awaalike rafiki/ndugu zake awatakao. Kama hawezi asifanye sherehe kabisa,atoke kanisani/msikitini arudi nyumbani kulala na mkewe wale tunda kihalali kwa raha zao.

 

Tena wenye tabia ya kupenda kuachangisha michango ya harusi zaidi ni WAKRISTO, wenzetu waislamu siyo sana kivile. Hawamaindi harusi kubwa kwa sana.

Ujue hata mie sipendelei mambo ya kuchangishana harusi wakati wagonjwa au ada za watoto hatuchangishani vitu ambavyo ni muhimu sana sana katika jamii yetu. Watu wanapenda sifa na miharusi mikubwa huku hata nyumba wakati mwingine hawajajenga. Ni sawa na mtu anayemfanyia birthday party kubwa mtoto wake wakati mtoto huyo huyo hata shamba au kijibanda hana kusema wazazi leo wakifariki mtoto ana sehemu ya kuanzia. Mie nilishawaambia ndugu na jamaa zangu nitachangia kwenye shida (misiba na ada za watoto wa shule), mambo ya harusi, ubatizo, birthday party au kitechen party wahangaike wenyewe, uzuri kwetu nina madada wawili hivyo hakuna vidume vya kusema tunaoa. LOL.....

Mie na mume wangu tulifanya harusi yetu simple na tuliamua kwenda bongo kufunga ndoa huku familia zetu na ndugu wa karibu tu ndio waliokaribishwa. Mume wangu hakutaka purukushani za kiswahili na pia tulikuwa na siku 7 tu za kutua bongo, kufunga harusi na kurudi ughaibuni. Siku chache baada ya harusi tulirudi ughaibuni basi huko nyuma ndugu wa mbali, jamaa na marafiki walitulaani hao. Tatizo la wabongo kunapokuja michango ya harusi mtu anatoa 20,000 ya peke yake, siku ya harusi utashangaa anakuja na nyumba yake yote matokeo yake hata vinywaji na msosi vinapelea. Ukitaka kuwakomesha wabongo fanya harusi yako wewe na ndugu wa karibu tu. Kwani harusi ni maharusi, mashahidi na familia zenu (wazazi, kaka na madada) basi.

Hata huku nje wazungu hawafanyi kama wabongo wanavyofanya vitu kwa kupenda sifa. Mtu wa kawaida wa kizungu anafanya mambo yake kawaida na sio kwa sifa kama wabongo. Na hawa watu wanajua kweli kubana pesa yao tofauti na sie.

Mie nafikiri weusi duniani karibu kote tuna tabia/hulka moja inafanana ya kupenda misifa. Mtu hana pesa lakini bado ana show off.  

 

Kisusi Mohammed said:

Wanadamu tumekuwa WATU wa ajabu sana! Tunaongozwa na hisia zetu kama wanyama, tumeondokana na uhalisia wetu sasa tunaendeshwa na mazingira na vishawishi vya nje! Kila mmoja anajaribu kuwa bora zaidi ya mwingine kwa kufanya jambo zaidi ya alilofanya mwenzake! Michango ya harusi, kipaimara, ubatizo, ubarikio, birthday, kitchen party, unyago, sendoff na sherehe zote za mtazamo wa aina hy ni kupoteza dira kwa cc wanadamu na kuckiliza hisia zetu kuliko kutazama UHALISIA. Mfano, juzi nimesikia harusi ya bwana mm
Dah! natamani sana kuchangia juu ya hii ishu ila moya unasita. Ngoja nitakuja baadae kidogo...
ha ha haaa.. kuwa mkweli tu.. unaogopa kusema cos bado hujaoa nini .??? hahahaaaa Nasubiri comment yako kwa hamu kubwa sana. PamoJah!!

Tulonge said:
Dah! natamani sana kuchangia juu ya hii ishu ila moya unasita. Ngoja nitakuja baadae kidogo...

Wala usihofu, siku ya harusi yako nakuletea 20 bags of cements ndio mchango wangu mkubwa mimi na baba yako, biashara ya bia na pilau tutaweka kando. LOL.....


Tulonge said:

Dah! natamani sana kuchangia juu ya hii ishu ila moya unasita. Ngoja nitakuja baadae kidogo...
Jana nimefahamiana na mtu kwa mara ya kwanza,eti leo ananieleza mambo ya kumchangia harusi hahahahhaaaaaaa. Inakera sana.

Kuolewa au kuoa ni jambo la kawaida ktk maisha ya sasa,lkn unapooa au kuolewa si lazima kufanyike sherehe au m2 kuchangisha michango ya harusi yake.kuoa ni kumpa bint muolewaji mahari yake,na pia lazima mtoa idhini awepo yaani baba au kaka.sasa hapa m2 utakuta anakodisha disco,matarumbeta nawengine hupeleka sherehe ukumbini.Hapa ndipo kwenye matatizo wewehuna hata kazi wala biashara ya maana unachangisha wa2.

Kwanini usiombe wakupe pesa hizo ili zikunyanyue kiuchumi na huweze kusaidia familia yako,hapohapo wa2 watakutukana kwamba aaah sherehe yenyewe ilikuwa ovyo tu bia hamna,mc hajui,bwana harusi mfupi na n;k.Wazazi nawaombeni kama mnahela sana za kufanya sherehe basi watazameni watoto wenu walioko shule,wasaidieni mayatmana wagonjwa,kuliko mambo haya ya harusi tunapoteza pesa bure,baada ya muda tu utasikia maharusi wameachana tena kupigana.Tubadilike jamani

Reply to Discussion

RSS

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*