Tulonge

MJADALA WA VAZI LA TIFA LA TANZANIA UNA TIJA YEYOTE KWA WATANZANIA?

Ndugu zangu wanatulonge, Wakati taifa la Tanzania likikabiliwa na changa moto nyingi ambazo hazijapatiwa uvumbuzi, kama vile mchakato wa kuunda katiba  mpya, ukosefu wa maabara katika shule mbalimbali za sekondari hapa nchini, tatizo la maji safi vijijini na upungufu wa madarasa kwa shule mbali mbali hapa nchini ambapo wanafunzi wengine hulazimika kusomea chini ya miti, Wizara ya habari, utamaduni, vijana na michezo imeibuka tena na mjadala wa kufanya mchakato wa kutafuta vazi la Taifa. je mjadala huu unatija yeyote kwa watanzania?

Views: 565

Reply to This

Replies to This Discussion

Nitarudi badae .....

najua hilo vazi litabagua tu mwenye kipato na asie na kipato, mkibisha mtanikumbuka kwa hili ninalosema,

Ni upuuzi tu! Watu wanaacha kujadili mambo ya msingi, badala yake wanaanza kujadili vazi la taifa. Inachekesha sana! Maoni yangu, huo mchakato ukome mara moja kwa maana kuna mambo mengi, matatizo mengi yanatukumba, hivyo basi ni lazima tuyashughulikie hayo kwanza kisha yafuate mengine. Kwanza hakuna anayetembea uchi. Kungekuwa na anayetembea uchi ingekuwa sawa kujadili.

Mkuu CHA, nakuunga mkono asilimia 1500 kabisa. Ni upuuzi usio na maana kabisa....watu wangapi wanahangaika na maisha magumu, hata chakula ni shida. Sasa watu wanatumia fedha nyingi kwa upuuzi kama huu, hivi tutakuja kuelimika lini? Kwakweli elimu bado hatuna kabisa.

hembu tuambieni nyie mnaokaa huko ughaibuni kuna sare za nchi huko jmn? au tz mafisadi wanatafuta kila namna ya kula pesa za Watanzania. inashangaza na kusikitisha, nchi inaacha kujadili mambo yenye manufaa kwa nchi wanajadili vazi, haya wakishapata tunashonewa wananchi wote au inakuwaje sasa?

@ Olivia......Hakuna upuuzi kama huo, mimi nikianza kufikiria wakati mwingine nashindwa hata kupata hamu ya kurudi nyumbani Tz, maana kumejaa upuuzi mwingi kweli. Nenda Vijijini ukaone hali ilivyongumu, watu wanaongelea vazi la Taifa, linawanufaisha nini Wananchi? Na sisi Wananchi tunakubali tu, upuuzi kama huu?

sioni kama tukichagua hilo vazi maisha yetu yatabadilika ni upotevu wa mda tu.

OLIVIA.... huku ughaibuni unavaa sare pale tu kazi yako inapokuhitaji uvaae sare (e.g. nurses, police, etc.). Unapokuwa mtu wa kawaida unavaa unavyojisikia weye iwe umevaa suruali ina matobo kwenye makalio yako nje hakuna anayefatilia. Uingereza ni nchi huru unavaa unavyopenda wewe. Kuna watu wamebahatika kualikwa kwenye nyadhifa maalum na head of state (Queen Elizabeth II) na watu hao wamekuwa wakiingia kwenye jumba la kifalme (ambako kuna ofisi za Queen Elizabeth II) huku wamevalia mavazi ya makabila yao ya kizulu, kimasai, kitswana, etc. na wanakaribishwa na mavazi yao kuheshimiwa.

Wanashindwa kujadili kuhusu huduma ya afya ilivyoshuka miaka hii 20 iliyopita kuwafanya wao wenyewe (wabunge na viongozi) kukimbilia INDIA kila wanapoumwa kwani imefikia hali mbaya hadi wanapokishikwa malaria wanakimbilia INDIA. Dawa feki (ambazo ni sumu) zinaingizwa Tanzania na kuua watu kila kukicha, hawaoni kuwa tatizo bali wanaongelea kuhusu vazi la taifa. 

Yaelekea huko bungeni kutwa wanaongea utumbo tuuuu.... Sasa hao wamasai, wamang'ati, etc. nao ambao wanavaa kufatana na jadi yao nao watawaambia wavae hilo vazi la taifa?

@ mama Malaika tz sijui imekuwaje, mimi ambaye ni mlala hoi nashindwa kuelewe hilo vazi wanatafuta la nini haswa? tz kuna mambo mengi ya msingi ambayo ya kijadiliwa na hiyo wizara ya habari, vjana, utatamaduni  na michezo vinaweza vikaleta tija, mf; suala la ukosefu wa ajira kwa vijana, ongezeko la vijana wavuta unga na bange. wanajadili vazi vazi kweli? au watz tumekuwa watu wakuchezewa akili zetu kila wakubwa wanavyojisikia,. Mi kwa kutokutoka kwangu nje ya Tz nilidhani labda huko ughaibuni ukifika na kitambulisho chako unatakiwa pia uwe umevaa vazi linalo wakilisha nchi yako, lakini kila mmoja ambaye amebahatika kutoka nje ya TZ ukimuuliza  anasema huko hamna jambo kama hilo, sasa tunapelekwa wapi jmn? vazi la kanga lipo huko uzunguni? rubega la kimasai nalo vp?
 
Mama Malaika said:

Wanashindwa kujadili kuhusu huduma ya afya ilivyoshuka miaka hii 20 iliyopita kuwafanya wao wenyewe (wabunge na viongozi) kukimbilia INDIA kila wanapoumwa kwani imefikia hali mbaya hadi wanapokishikwa malaria wanakimbilia INDIA. Dawa feki (ambazo ni sumu) zinaingizwa Tanzania na kuua watu kila kukicha, hawaoni kuwa tatizo bali wanaongelea kuhusu vazi la taifa. 

Yaelekea huko bungeni kutwa wanaongea utumbo tuuuu.... Sasa hao wamasai, wamang'ati, etc. nao ambao wanavaa kufatana na jadi yao nao watawaambia wavae hilo vazi la taifa?

Mavazi ya kanga tunavaa sie ambao tunabeba khanga kutoka Tanzania. Na mavazi ya kimasai hivyo hivyo tunakuja nayo toka Tanzania

Reply to Discussion

RSS

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*