Tulonge

Nilipofikia kuhusu kumuunganisha mdau wa Tulonge 'Grace Kamonga' na Mwananchi Communication Ltd ili aweze kutoa msaada wa kumtunza na kumsomesha mtoto wa binti mlemavu

Asha Musa (katikati) akiwa na bibiu yake na mtoto wake. (Picha na Shakira Nyerere,mwananchi)

Siku ya tarehe 20 Jan 2013 tovuti ya www.mwananchi.co.tz ilitoa habari ya msichana mwenye ulemavu wa viongo vya mwili karibu vyote ambaye alibakwa. Binti huyo analelewa na bibi yake na ana mtoto mmoja wa kiume(6) ambaye pia alimpata baada ya kubakwa siku za nyuma.Bofya hapa kusoma zaidi.

 

Habari hiyo nilii-share hapa tulonge, ndipo Grace Kamonga ambaye ni mdau wa tulonge.com alipoguswa na habari hiyo na kuamua kujitolea kumtunza na kumsomesha mtoto wa binti huyo. Licha ya Grace kuthibitisha hilo kupitia comment yake hapa tulonge, pia niliwasiliana na nae kwa njia ya simu na akathibitisha hilo.

 

Jitihada za kuwasiliana Mwananchi Comm Ltd nilizianza hivi:-

1. Jana niliwaandikia barua pepe kuwaeleza hili lkn kwa bahati mbaya iligoma kufika, sikujua kama kulikua na tatizo upande wao au vipi. Niliituma kwa webmaster@mwananchi.co.tz ambayo ndiyo email address iliyopo kwenye tovuti yao.

 

2. Leo baada ya kugundua email niliyo watumia haikufika, niliamua kuwapigia simu kwa namba +255 713471195 ambazo ipo kwenye tovuti yao lkn haikupokelewa.

 

Baada ya simu kutopokelewa nilipokea ujumbe toka kwao 'Mwananchi', na majibizano yalikua hivi:-

 

Mwananchi: Andika sms plz

 

Tulonge: Mimi ni administrator wa www.tulonge.com, kuna member wangu ameamua kutoa msaada wa kumtunza na kumsomesha mtoto wa dada mlemave wa Kondoa. Habari yake mliitoa tar 20 Jan yenye kichwa "Mlemavu anayeteseka baada ya kubakwa". Kinachotakiwa ni kumuunganisha na familia hiyo.Sheria zote zifuatwe ktk kufanikisha hili. Waweza nipigia kwa maelezo zaidi.

 

Mwananchi: Asante tutasaidiana kufanikisha hili.

 

Tulonge: Sawa, namba ya anayetaka kutoa msaada ni +255767882525 anaitwa Grace Kamonga wa Wizara ya Elimu, Kongwa,Dodoma.

 

Mwananchi: Asante, nimewapa wahariri wanashughulikia

 

Tulonge: Sawa Mkuu.

 

Tuliishia hapo, ujumbe wa mwisho niliutuma saa 6:12 mchana wa leo.Nitaendelea kufuatilia

 

Saa 6:27 mchana wa leo(January 23, 2013):

Nimepokea simu kutoka kwa Bw. Daniel Mwaijega ambaye ni Editorial Manager wa Mwananchi Comm Ltd. Ameushukuru Uongozi wa Tulonge na wadau wote wa tulonge kwa jitihada za kutaka mtoto huyu asaidiwe. Pia wamesema watawasiliana na Grace Kamongo ili kufanikisha suala hili.

 

Saa 7:24 mchana wa leo(January 23, 2013)

Mdau 'Grace Kamonga' amenipa taarifa kuwa amepigiwa simu na Mwananchi Comm Ltd ili kufuata taratibu za kisheria za kukabidhiana mtoto huyo.

Saa 9:30 mchana wa leo(Feb 05, 2013)

Nimewasiliana na Grace ili kujua kama Mwananchi wanaendelea na mchakato. Ameniambia mchakato bado unaendelea, mhariri (Daniel) alienda Manyoni ambapo huyo mtoto anaishi ili kuzungumzia suala hilo. Baada ya hapo mhariri huyo atarudisha ripoti Ofisi za Mwananchi ili wajue kinachofuata.

Saa 5:28 usiku wa leo(Feb 06, 2013)

Nimepokea sms toka kwa Grace, ikisema kuwa wana familia ya mtoto ambaye anataka kumsaidia IMERIDHIA kumtoa mtoto wao ili akatunzwe na Grace. Kesho Grace ataongea na Mwananchi kwa njia ya simu ili kujua nini kitafuata.

Saa 3:54 usiku wa leo (Feb 12, 2013)

Nimeongea na Grace kwa njia ya simu akanieleza kwa sasa anasubiriwa arudi nyumbani kwake Kongwa,Dodoma ili aweze kukabidhiwa mtoto huyo. Grace yupo masomoni Iringa, anategemea kumaliza masomo yake mwezi wa 7/ 2013.Ila kuna uwezekano wa kukabidhiwa mtoto huyo hata kabla ya mwezi wa 7.

Email toka kwa Grace baada ya kumuuliza walipofikia

Saa 5:17 usiku wa leo (Sept 30, 2013)

Najua wengi mtakua mnajiuliza mbona kuna ukimya juu ya tukio hili. Nilichat na Grace na akanieleza kuwa bado yupo Chuoni, kuna mambo anayakamilisha ndomaana hajakabidhiwa mtoto hadi sasa. Lakini kasema itabidi akabidhiwe mtoto ndani ya mwaka huu (2013) ili mwakani aweze anza shule. Ifuatayo ni Chat yetu.

Nitaendelea kuwajuza nini kinaendelea

Views: 2434

Reply to This

Replies to This Discussion

hongera sana kaka Mungu akupe afya katika kufanikisha mtoto anapata msaada

Pa1 sana mkuu Mathias

mathias mwita said:

hongera sana kaka Mungu akupe afya katika kufanikisha mtoto anapata msaada

Great!!!!!!!!!!

Kila kinachoendelea nitakua nakiongezea hapo juu.Kwahiyo mtakua mnaangalia hapo juu,sitaweka kama comment.

Safi sana mkuu kwa jitihada zako..Pamojah

Pa1 sana wakuu, kuna update hapo juu kutoka kwa Editorial Manager wa Mwananchi.Unaweza itupia jicho kujua nn kinaendelea

Asante Dismas nwamenipata na wanawasiliana na mimi ili kufuata taratibu za kisheria katika ngazi mbalimbali za uongozi ili niruhusiwe kumtunza.  Kazi nzuri kaka. Ni mimi  Grace

tupo pa1 Grace, utaendelea kutujuza nini kinaendelea

John Genda said:

Asante Dismas nwamenipata na wanawasiliana na mimi ili kufuata taratibu za kisheria katika ngazi mbalimbali za uongozi ili niruhusiwe kumtunza.  Kazi nzuri kaka. Ni mimi  Grace

Mungu ambariki sana huyu Dada Grace Kamonga kwani wapo matajiri wengi sana fadhila zao zinapelekwa kwenye mpira na kwingineko lakini si kwa wahitaji kama mtoto huyu. Huyu Dada Grace wala si tajiri lakini amejaa utu, wema na ukarimu. Ubarikiwe sana. "Heri Masikini wa Roho kwa maana watamuona Mungu"

Good News!!

Mtandao unafanya kazi ya jamii na hayo ni matunda mazuri...................siyo kutumia kwa maswala yanayo ipelekea jamii kupata majeraha. Hongera TULONGE..................kufanikisha msaada kwa ndugu huyo.

Asante Jeath, pa1 sana

Jeath Justin Prosper said:

Mtandao unafanya kazi ya jamii na hayo ni matunda mazuri...................siyo kutumia kwa maswala yanayo ipelekea jamii kupata majeraha. Hongera TULONGE..................kufanikisha msaada kwa ndugu huyo.

Reply to Discussion

RSS

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*