Tulonge

Ndugu wadau nikisema TULONGE.COM ya Dismas inatokana na FOTOBARAZA.COM ya Babukajda, nina hakika sintakuwa nimekosea. Hili hata Dismas mwenyewe analitambua--au niseme kuwa mimi kujuana na Dismas, Alfan, Angela, Chaoga, ALex Magere, Mama Malaika, Lucy wa Mama, na wengineo wengi ambao wanakaribia elfu moja ni kutokana na FOTOBARAZA ya BabuKadja. Na hata leo hii uwepo wa TULONGE unatokana na Fotobaraza ya Babukadja.

La kushitusha ni kwamba; leo yaani tarehe 4-3-2012 nilipojaribu kutembelea kijiji kile cha jirani (FOTOBARAZA) nilikutana na ujumbe unaoashiria kupotea kwa kijiji cha fotobaraza katika ulimwengu wa social network.

Ujumbe ulikuwa unasema "This Network is overdue in payment and at risk of being disabled".

Nilijaribu kumtafuta Babukadja ili nipate kujua zaidi juu ya hili, lakini all my efforts ended up in vain.

Wasiwasi wangu ni kuwa; marafiki ambao tulikuwa nao kule na hawajui ni wapi watatufuata wenzao tulipo, wanaweza kupotezana na sisi. Hivyo ombi langu ni kuwa tuwape taarifa ya kuwepo kwa kijiji hiki cha TULONGE.COM, hii itasaidia kuendeleza urafiki wetu uliodumu kwa takribani miaka mitano sasa. Mpe taarifa rafiki kwa njia yeyote ile, ilimradi tu atambue uwepo wa TULONGE.COM

MAONI YANGU

Maoni yangu kwa mkuu wa kijiji hiki na wadau wenye mapenzi mema na kijiji hiki ni kuwa, tufanye hima kwa maana ya kuitisha HARAMBEE kwa ajili ya kijiji ili tu tuweze kuepukana na kile ambacho naamini kinaweza kutokea kwa FOTOBARAZA siku chache zijazo.

Nina hakika kuwa; wapo wadau kwa kuwataja kwa uchache kama vile DIXON KAISHOZI, CHAOGGA, PASCAl aka MABAGALA, ANGELA, ALFANI, CRYSTER na wengine wengi ambao wapo teyari kuchangia chochote pale watakapoombwa kufanya hivyo. Haiitaji kuwa na pesa kama REGINALD MENGI ili kucangia. NI moyo tu. Binafsi nipo teyari kuchangia chochote kwa ajili ya kijiji, na mwisho nipendekeze kuwepo mradi utakaowezesha kijiji kujipatia pesa kwa ajili ya kujiendesha na si tu kutegemea pesa toka mfukoni mwa DISMAS. Si mbaya hata products za PamoJah zikitumika kutunisha mfuko kwa ajili ya pesa za kuendeshea kijiji. Maana yangu ni kuwa; pesa zitakazopatikana kutokana na mauzo ya products za PamoJah kwa maana ya STICKERS, T-SHIRTS, na products zingine asilimia fulani itatumika kutunisha mfuko maalum kwa ajili ya kuendeshea kijiji. Hii itawahusisha hata wadau waliopo nje ya nchi--Mama Malaika, Dunda, Magere, Chibiriti, Mary Wa Mkumbo na wengine wengi.

Nimalizie kwa kusema "PamoJah We Can" Keep on Moving.

Amani kwenu wote.

Views: 1142

Reply to This

Replies to This Discussion

Unajua ukimuombea mwenzio mabaya siku zote yanaweza yakakurudia wewe.Chunga sana!!

Baada ya Fotobaraza kuzimia kipindi cha nyuma, Dismas akaona tusipotezane akaanzisha kijiji hiki cha Tulonge ili kutuweka pamoja. Kwa bahati nzuri Fotobaraza ikamwagiwa maji ya barafu ikazinduka na kuwa hai tena na wadau tukafurahi maana tukawa tuna vijiji viwili vinavyoshirikiana. Kibaya kilichojitokeza ni kwamba wenzetu ambao hawakupenda tulonge iwepo wakawa wanapiga vijembe na kuponda kuanzishwa kwa kijiji cha tulonge kiasi kufikia kusema kuwa kitakufa muda si mrefu kwa sababu wadau wote ni waliokuwa fotobaraza. Lakini walishindwa kujua kuwa waliokuwa wanakiweka kijiji kile "alive" ni wadau hao hao waliounga mkono uwepo wa tulonge na waliogoma ni wadau ambao sio active sana matokeo yake kijiji kile kikakosa mvuto na nadhani ikapelekea na Mwenyekiti kukosa ari ya kukiendesha. Nina imani Tulonge kitazidi kudumu na kuimarika siku hadi siku ukitilia maanani kuwa wadau wake wengi ni wastaarabu na wanaopenda kushirikiana. Mungu Ibariki Tulonge daima..Pamojah We Can Change the World.

Kaka Alfan@,si utani kaka kwa maoni hayo umegonga mule mule.Foto baraza ilikuwa bomba sana lakini sasa kadiri siku zilivyokuwa zikiendelea kujongea mbele,ndivyo kulivyokuwa kukizidi ma-haaa-jabu kona zile.

Hayo madubwasha yaliyokuwa yakijiri mitaa ile ilisababisha wengi kunung'unika na hata wakawa spmetime wanakosa raha ya kutia maguu pale wakihofia kushuka heshima yao,ilitokea mtu mmoja akarusha mitaa ile picha ya uchi yaani full uchi biashara zote nje nje,nashukuru sana wadau walituma salamu za hasira dhidi ya kitendo hicho.

Lakini pamoja na hayo hiyo ilikuwa ni sababu ya kijiji kukosa mvuto,na kuna sababu zingine zingine huwenda wadau wakawa wanazimiliki zilizosababisha kijiji kile kukosa mvuto.

wakati mvuto wa kijiji ukiendelea kupotea huku kijiji cha Tulonge kinazidi kufunika ile mbovu,kutokana na kuwa cool zaidi,na ninaimani "Tulonge  itakuwa unbreakable zaidi".!

Hahahaahaaa Alfan naona na wewe umejitahidi kuandika ka-gazeti.Nways, ujumbe umeeleweka.

OMARY... nami nilikuwa na mawazo kama yako ukizingatia kijiji kimetuunganisha sana.

 

DISMAS nakuomba ndugu yangu iwapo unaona kuna tatizo la aina yeyote kuhusu kijiji chetu cha Tulonge basi utushirikishe. Na kushiriki kwetu sio kwamba tutakushuritisha ni jinsi gani uongoze kijiji bali tutachangia tu suluhisho na baada ya hapo tutakuachia uendelee na kuongoza Tulonge.

 

UMOJA NI NGUVU!!

 


Omary said:

Kiukweli news hii kwangu imekuwa ya kush2wa sana maana kiukweli kila aliopo hapa kama si wote ila asilimia kubwa tumetoka fotobaraza je tunaweza kumtafuta muasisi wetu na kujuwa kilichojili huenda tukipata kujuwa kinacho tunaweza kufanya jitihada za ziada za kuweza kukinusuru kijiji chetu pendwa. Babu popote ulipo jitokeze wajukuu zako tunahitaji kujuwa kitu toka kwako Tafadhali.

 

Mr Tulonge pls pls tafuta kamfuko katakakoweza kuendesha kijiji maana napata woga kupoteza ndugu zangu

Mama,Angela,Alfan,Chaoga,Dixon,Chalii,siwezi kuwamaliza wote jamani tupo wengi kama mjuwavyo umoja ni nguvu utengano ni Dhaifu hivyo kwenye umoja wetu naamini tunaweza chochote tutakachotaka kufanya kinawezekana ilimladi tuwe na lengo moja.  TULONGE me nitakuja mpaka geto kama utakuwa na nia ya kutusambaratisha sema tu kwa Babu sipajui ningefanya maandamano ya pekeangu mpaka kwa Babu nikamuuliza maswali 2 tu. 

Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha! Alfan na Chalii inaonesha mlikunywa soda zinazolewesha before kuchangia. NImecheka sana. Kwa hiyo Chalii unataka kuhamisha kila kilicho chako pale fotobaraza?

Anyway, wadau kikubwa ni kujadili namna gani tusaidiane kuendesha kijiji hiki cha TULONGE hasa ukizingatia kuwa raha tunazipata woote na si DISMAS peke yake kama walivyosema Alfan na Chalii. Na kama alivyosema Alfan na Dixon,kuwa Mkuu wa Tulonge asione soo kusema iwapo kuna tatizo la kiuendeshaji. Na sisi kuchangia pesa kwa ajili ya kijiji haina maana kuwa tunataka kuki-rule kijiji kwa sababu tu pesa yetu inafanya kijiji ki-run, la hasha....hitaji letu la kutaka kukichangia kijiji ni kujenga ushirikiano katika mambo mbalimbali, na kufanya tuwe pamoja zaidi. Na isifikie wakati tukashindwa kujuliana hali eti kwa sababu hakuna pesa za kuendeshea kijiji. Kwa kuzingatia michango ya Chalii, Dixon, na Alfani niseme tu kuwa tupange mikakati itakayofanya kijiji hiki kiendelee kupaa na kuwa unique. Ni hayo tu kwa sasa.

Asante Dixon

Tulonge said:

Teh teh teh hamna noma mzee Dixon, mimi yakinifika shingoni nitasema mapemaaa.Ila kwa sasa ngoja niendelee kukomaa peke yangu mdogo mdogo.

Lkn huwezi jua kama ni payment issues ndiyo zimefanya kijiji jirani kifikie hatua hii. Yawezekana ni sababu nyingine. Pia bado kuna muda wa kukifanya kikiji kiendelee kuwa hewani,siyo kwamba kimeshakufa kabisa.Dixon Kaishozi said:

Naungana na Cha kwa maoni yake.. Najua kuna gharama za kuendesha hiki kijiji ambazo inambidi Dismas aingie mfukoni kwake ambazo inabidi tusaidiane ili tuweze kufaidi yale mema tunayo yapata kwenye kijiji chetu. Kama hutajali bwana Dismas unaweza kuweka wazi gharama zilizopo ili tuchangiane yasije yakatukuta kama ya pale kijiji jirani.. naogopa na sipendi kabisa kupoteza NDUGU zangu nilionao hapa!!


Chalii sijawahi kukuona live. Natamani nikucheck live......tehe tehe tehe tehe teh!
Chalii_a.k.a_ILYA said:

Kaka Alfan@,si utani kaka kwa maoni hayo umegonga mule mule.Foto baraza ilikuwa bomba sana lakini sasa kadiri siku zilivyokuwa zikiendelea kujongea mbele,ndivyo kulivyokuwa kukizidi ma-haaa-jabu kona zile.

Hayo madubwasha yaliyokuwa yakijiri mitaa ile ilisababisha wengi kunung'unika na hata wakawa spmetime wanakosa raha ya kutia maguu pale wakihofia kushuka heshima yao,ilitokea mtu mmoja akarusha mitaa ile picha ya uchi yaani full uchi biashara zote nje nje,nashukuru sana wadau walituma salamu za hasira dhidi ya kitendo hicho.

Lakini pamoja na hayo hiyo ilikuwa ni sababu ya kijiji kukosa mvuto,na kuna sababu zingine zingine huwenda wadau wakawa wanazimiliki zilizosababisha kijiji kile kukosa mvuto.

wakati mvuto wa kijiji ukiendelea kupotea huku kijiji cha Tulonge kinazidi kufunika ile mbovu,kutokana na kuwa cool zaidi,na ninaimani "Tulonge  itakuwa unbreakable zaidi".!

Tehetehetehtehetehetehetehetehe..Yaani nilijiona kama nimeandika boonge la kitabu kumbe hata maneno 100 hayajafika...

Tulonge said:

Hahahaahaaa Alfan naona na wewe umejitahidi kuandika ka-gazeti.Nways, ujumbe umeeleweka.

Mama mep huwa najifunza mepngi sana hapa kijijini pia nikipitiaga hapa kijijini huwa nafurahi sana hatakama muda mwengine nina hasira zitokanazo na kazi, maudhi ya walimwingu c unajuwa jamii zeptu zinazotuzunguuka

sio wote watakaokufarahisha kuna wngin watakuudhi hivyo huingia kijijini na kujificha kabisa humu ndani

muda c mrefu utasikia sauti ya kicheko tena pepkeangu kama mwehu so nakuwa nimeshajisahaulisha yaliopita

sasa leo nikipotezep kijiji hiki itakuwajep?! Noo   Tulonge pls Anzisha kamfuko ka kijiji haraka iwezekanavyo

maana kama ujuavyo wengine pesa tunazipata kwa manati so walau kamfuko kakiwepo tunatupia japo mia 5 ukipata tena unatupia 300 mwisho wa siku kijiji kinajiendesha chenyewe najuwa life ilivyongumu kwa sasa hata ukitoa 1000 utakuwa umepunguza bajeti japo ya maji mchana maana uhai 700 sasa. so Tulonge jipange me nitakukera sitakubali kijiji kipotee yaani utakuwa unakimbia geto lako maana kila ukitoka job unanikuta mlangoni nanguojea kudai kijiji changu.

jamani chiswahili kigumu Mama me huwa najifunza mengi sana hapa kijijini haya endeleeni na ujumbe ufuatao

maana nilikosea maneno nilioyarudia

Kila kilichozaliwa kitaonja mauti.

OMARY umenifurahisha sana na nimekuelewa uzuri. Hata mie najifunza mengi na kupata habari za nyumbani.

 

Omary said:

jamani chiswahili kigumu Mama me huwa najifunza mengi sana hapa kijijini haya endeleeni na ujumbe ufuatao

maana nilikosea maneno nilioyarudia

Reply to Discussion

RSS

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*