SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA WATANZANIA WOTE JUU YA AJALI YA MELI HUKO ZANZIBAR.
Si rahisi kueleza uchungu mkubwa tulionao wana Tulonge juu ya ajali ya meli iliyotokea huko Zanzibar usiku wa kuamkia tarehe 10/09/2011 na kusababisha ndugu zetu kupoteza maisha.
Kwa niaba ya Wadau wa Tulonge napenda kuungana na Watanzania wote katika maombolezo ya msiba huu mkubwa uliotukuta. Salamu za rambirambi ziwafikie wote waliopoteza ndugu zao na watanzania wote. Pia tunawapa pole wale waliyo nusurika katika ajali hiyo kwa msukosuko mkubwa walioupata katika kufanya jitahada za kuokoa maisha yao, wazidi kumshukuru Mungu kwa kuwanusuru.
Mungu azidi kuwatia nguvu na moyo wa uvumilivu wale wote waliopoteza ndugu zao.
Mwenyezi Mungu awalaze pema peponi wote waliopoteza maisha.
Dismas,
Tags:
Bwana Alitoa Na Bwana Ametwaa. Jina la Bwana lihimidiwe. Amen!
Dah! kiukweli haya maafa yamenigusa sana ukizingatia kuna rafiki yangu 1 alikuwepo na hakufanikiwa kupona
MUNGU ailaze roho yake mahala pema peponi Amen.
huu ni msiba wa wa Tanzania wote nilipata msituko mkubwa sana baada ya kupata taalifa hizo kwani nilijuwa ndani ya chombo kilichozama kuna m2 ninaemfahamu na mpaka sasa tunaamini kapoteza maisha kwani hata kwenye maiti zilizo okolewa hakuwemo inasadikika yumo ndani ya chombo hapo hakuna maisha tena chombo kimekuwa kaburi lao.
© 2022 Created by Tulonge.
Powered by