Jamani nataka kuja na stahili ya peke yangu katika historia ya Tanzania. Mimi ikifika wakati nikaamua kuwa na mwenza, watu watakunywa na kula bure. Sitohitaji mchango wa mtu yoyote, badala yake nitagharamia sherehe yangu mwenyewe. Sitataka harusi kubwaaa ya kukata na shoka, sitataka watu wengi sana, kwa hiyo sitotaka lawama ya "kwa nini hukunialika".
Tags:
Tehe-tehe-tehe pole dada kwakudhani umekuja na style mpya kumbe zilipendwa, mbona huo ndio ulikuwa utaratibu wa zamani, wakati wazee wetu wakiona hakuwa na vikao au kadi za michango. ningekuelewa kama ungesema unarudia utaratibu wa zamani.
ANY WAY BIG UP kwa uamuzi huo wakuwaiga mababu zetu, usiishie hapo nenda mpaka kwenye mavazi na namna ya kujipodoa huenda ukawa kioo cha jamii
Hongera, nalo neno ila ujiandae kwa utamaduni wa Kitanzania tulozoea au niseme ujamaa ni kuchangia hata kama ni kidogo. So wasipokuja nawe ujiandae kula na kusherehekea peke yako, usilalamike.
Haya!!!
Na mimi sihitaji michango kama Zainabu!
© 2022 Created by Tulonge.
Powered by