Habari za wote!
Jamani ni muda hatujajuliana hali, hatujabadilishana mawazo na mambo kama hayo. Nafikiri ni wakati sasa kujumuika pamoja katika kuimarisha udugu, na urafiki wetu kwa kukutana pamoja kama ilivyokuwa ada.
Ni siku ambayo tutakuwa tunafurahi kwa kupongezana kwa kufikia malengo yetu, ni siku ambayo tutakuwa tunafurahi na kutiana moyo kwa mambo ama mipango iliyopangwa ili iweze kutimia na mambo kama haya. Ki-ujumla itakuwa siku ya kupongezana, na kutiana hamasa.
Kauli mbiu iwe "KUKUTANA KWETU NI ZAIDI YA KUFURAHI"
Ni imani yangu kuwa wote mtaupokea ujumbe huu kwa hali chanya.
Hili ni wazo langu tu. Sijui wadau mnasemaje kwa hili?
Tags:
Majukumu yamezidi.. @ Alfan
Nitarudi badae kidogo.. teheee, tufahamishane mapema kabla tiketi za fastjet hazijapanda bei.. hahahaa @ Alfan
Hahahahahahahah..Usijali mkuu
Dixon Kaishozi said:
Nitarudi badae kidogo.. teheee, tufahamishane mapema kabla tiketi za fastjet hazijapanda bei.. hahahaa @ Alfan
Kama bado na mm nimo.
© 2023 Created by Tulonge.
Powered by