Tulonge

Habari za wote!

Jamani ni muda hatujajuliana hali, hatujabadilishana mawazo na mambo kama hayo. Nafikiri ni wakati sasa kujumuika pamoja katika kuimarisha udugu, na urafiki wetu kwa kukutana pamoja kama ilivyokuwa ada.

Ni siku ambayo tutakuwa tunafurahi kwa kupongezana kwa kufikia malengo yetu, ni siku ambayo tutakuwa tunafurahi na kutiana moyo kwa mambo ama mipango iliyopangwa ili iweze kutimia na mambo kama haya. Ki-ujumla itakuwa siku ya kupongezana, na kutiana hamasa.

Kauli mbiu iwe "KUKUTANA KWETU NI ZAIDI YA KUFURAHI"

Ni imani yangu kuwa wote mtaupokea ujumbe huu kwa hali chanya.

Hili ni wazo langu tu. Sijui wadau mnasemaje kwa hili?

Views: 1620

Reply to This

Replies to This Discussion

Mimi nadhani tukutane mwakani wiki ya 2 au 3 ya mwz Januari.Najua kipindi hiki cha sikukuu wadau watakua bize sana na familia zao. Tena ndugu zetu wachaga hawatakuwepo kabisa hapa mujini, c mnawajua.

Hilo ni wazo langu, cjui wadau wengine.

kweli na ni nzuri ipangwe tarehe na mahari

wk ya 2 au 3 mwake.

Natumaini itapangwa vizuri na sisi wa mikoani tuweze kushiriki..

Ha ha ha ha! Dismas una utani na Lucie pamoja na Dickson.

Ukweli wiki ya kwanza au ya pili itakuwa nzuri sana. Ila uhamasishaji uwe mkubwa zaidi ili mambo yawe mazuri zaidi. Nakumbuka ile ya mara ya mwisho ilikuwa nzuri sana japo tulikuwa mtu kumi tu. Sipati picha tukiwa mtu zaidi ya kumi itakuwaje.

Tujenge utamaduni wa kujuliana hali kwa kukutana moja kwa moja, yaani ana kwa ana; Na si tu kuishia kusalimiana na kutaniana online.

I hope kutakuwa na mambo ya kipekee kwa tukio hili la kihistoria.

Zawadi za Key-holders toka PamoJah We Can Inc. kwa wote watakaoshiriki au kutokea katika tukio hili la kihistoria zitatolewa haijalishi watu wangapi watashiriki katika tukio hili. Hata Kama kutakuwa na washiriki 1000 (elfu moja), key-holders za nembo ya PamoJah We Can zitatolewa bureeeeeee!

PamoJah We Can jamani!

Nimalizie tu kwa kusema "KUKUTANA KWETU NI ZAIDI YA KUFURAHI"

Pamoja sana Cha, nimeipenda hiyo yako

Ni jambo zuri kwa kweli, siku hiyo nitavaa T - Shirt ya Pamojah tunaweza.

Ni wazo zuri,lakini sijajua zaid,kuhusu tulonge vision,Mission for the coming years,kwani tunapokutana tunapaswa kuutanua mtandao wetu zaid,pia kujikita katika nyanja ya Elimu,Afya na mengineyo,ikiwezekana tuwe paternaship na Taasisi nyinginezo kayika kufanya kazi za jamii,kuliko tu kupeana matukio ya hapa na pale!sijui mnaonaje MEMBERS!

Wazo zuri Masha

Masha waryoba said:

Ni wazo zuri,lakini sijajua zaid,kuhusu tulonge vision,Mission for the coming years,kwani tunapokutana tunapaswa kuutanua mtandao wetu zaid,pia kujikita katika nyanja ya Elimu,Afya na mengineyo,ikiwezekana tuwe paternaship na Taasisi nyinginezo kayika kufanya kazi za jamii,kuliko tu kupeana matukio ya hapa na pale!sijui mnaonaje MEMBERS!
FUNGA MWAKA/FUNGUA MWAKA.
Mimi nashauri ifanyike baada ya mwaka mpya kwasababu kipindi hiki cha maandalizi ya sikukuu wadau wengi wanasafiri sehemu mbalimbali hasa wale ndugu zetu wa kanda ya k hivyo basi kwa kutojumuika nao itapunguza msisimko au mnasemaje wenzangu? Kukutana ni zaidi ya kufurahi.
Jaman Mathias !wanaosafiri kipindi hiki ni kila upande Wa Tanzania wa2 wanakwenda makwao.tatizo wachaga au watu wa kaskazni wamesambaa sehemu kubwa ya Tanzania ,ndio maana wanaonekana wao ni watu Wa kuhesabiwa kila mwaka.Wana tulonge tukutane kuanzia jan 15 2013 endapo MUNGU atatuweka hai.Nina Hakika likizo za mashule na za baadhi ya maofisi zikiwa October ,December wasafiri watapungua sana

Natamani na mimi ningekuwepo Tanzania ili nipate hudhuria party :-)

Reply to Discussion

RSS

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*