Tulonge

Tulonge Funga Mwaka Party yaja, kama mkereketwa wa urafiki mtandaoni, unaombwa kuhudhuria bila kukosa tukio hili muhimu ili kuimarisha urafiki wetu. Tukio hili litakuwa siku ya Jumamosi ya pili ya mwezi wa kwanza ya mwaka huu wa 2012 yaani siku ya tarehe ya 14. Eneo ni moja kati ya haya (A) Msasani Club-karibu na ofisi za makao makuu ya Zantel, ama Ubalozi wa Marekani (B) Msasani Club, pale karibu na kituo cha WARIOBA. Ni vyema vilevile tusaidiane kuhusiana na location yaani (A) ama (B). Kwa yeyote atakayejisikia kujumuika pamoja na wadau naomba athiitishe kupitia mjadla huu, ama kuwasiliana kwa namba hizi 0784822269/0715822269 (namba zangu). Ama 0713520629 (namba za mkuu wa mtandao huu-Dismas Hiza).

Kumbuka, lengo la tukio hili ni kuwaleta wanatulonge pamoja.

Kumbuka kuja na vijisenti, maana naambiwa hapa na Dismas  kuwa mhasibu wetu wa kijiji kakimbia na pesa. Kwa hiyo serikali ya kijiji ina hali ngumu kiuchumi, hivyo kila mshiriki itamlazimu ajihudumie.

Ni matumaini yangu tutakuwa pamoja siku hiyo.

Asanteni sana.

Views: 639

Replies are closed for this discussion.

Replies to This Discussion

Bora msasani club karibu na kituo cha Warioba, nadhani hapo kuna eneo kubwa la kufukuza kuku na kuvuta kamba teh teh teh. Nataka nimuone Chaoga anavyo fukuza kuku.

Kwa warioba ndio pazuri pale zantel labda tukacheze sebene.

Tuombe Mungu atuwezeshe ili tuone kama tutaweza kujumuika. Itaanza saa ngapi??? ILi ikiwezekana tukaombe ruhusa kwa familia zetu kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

jamani naombeni hivi wazo langu litaleta watu wengi naamini mimi natamani kufika, tufanyeni mwezi wa pili pangeni jumapili yeyote ile, maana mimi trh 14, kunashughuli na sitaweza kufika huko kwakweli nitaumia sana, yani nikikosa bora ile scad ya iran mnigeuzie mimi, wazo langu,

Asante kwa mualiko, natumai tutajumuika pamoja.

sasa bonielly nawe umepewa wiki mbili za kujiandaa kwa siku hiyo moja tiari unasuasua....Teh. mkianza hizo za mwezi wa pili siju itakua tena ni funga mwaka au fungua mwaka au ndo itakua tena valentine!!!.....tarehe imeshajulikana bana wee bonielly nenda mkasababishe shughuli hiyo....haaa.   shauri yako usipokwenda ujue wenzio wanakwenda..kidole kimoja....!!1...hahahahaaaa....

asante kwa mualiko ........kuku wapo??

NAKUJA NA BONNIELLY

Silas jitahidi ujumuike pamoja na wadau.

Kwa kweli nitajitahidi kuja. Hiyo siku ila hujaniambia ni saa ngapi?

Kuanzaia saa tisa mpaka hapo utakapochoka.

Silas A. Ntiyamila said:

Kwa kweli nitajitahidi kuja. Hiyo siku ila hujaniambia ni saa ngapi?

nimejaribu kuweka mambo zawa nadhani nitakuja na angela kwenye ka rv4 kake, lbd itokee dharura, lkn mgeni wangu kuna m2 atanipokea sasa naomba mjitahidi kumjulisha dick nitafurahi zaidi akifika, yani ni my brother sana,

RSS

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*