Tulonge

Tulonge Funga Mwaka Party yaja, kama mkereketwa wa urafiki mtandaoni, unaombwa kuhudhuria bila kukosa tukio hili muhimu ili kuimarisha urafiki wetu. Tukio hili litakuwa siku ya Jumamosi ya pili ya mwezi wa kwanza ya mwaka huu wa 2012 yaani siku ya tarehe ya 14. Eneo ni moja kati ya haya (A) Msasani Club-karibu na ofisi za makao makuu ya Zantel, ama Ubalozi wa Marekani (B) Msasani Club, pale karibu na kituo cha WARIOBA. Ni vyema vilevile tusaidiane kuhusiana na location yaani (A) ama (B). Kwa yeyote atakayejisikia kujumuika pamoja na wadau naomba athiitishe kupitia mjadla huu, ama kuwasiliana kwa namba hizi 0784822269/0715822269 (namba zangu). Ama 0713520629 (namba za mkuu wa mtandao huu-Dismas Hiza).

Kumbuka, lengo la tukio hili ni kuwaleta wanatulonge pamoja.

Kumbuka kuja na vijisenti, maana naambiwa hapa na Dismas  kuwa mhasibu wetu wa kijiji kakimbia na pesa. Kwa hiyo serikali ya kijiji ina hali ngumu kiuchumi, hivyo kila mshiriki itamlazimu ajihudumie.

Ni matumaini yangu tutakuwa pamoja siku hiyo.

Asanteni sana.

Views: 583

Replies are closed for this discussion.

Replies to This Discussion

Asanteni kwa mualiko.. Nasikitika tena SANA kwa kushindwa kuudhuria... NILIJITAHIDI SANA TENA SANA!! Nilikuwa safarini kipindi "posti" hii imewekwa, kwani nilikuwa najua party ni tarehe 7 jan kama ilivyopendekezwa kwa mara ya mwisho baada ya kuhairishwa tena! So tarehe 4 nikawa tayari nipo dar kwa maandalizi ya party lakini bahati mbaya nikapata taarifa ni tarehe 14 tena!! IMENISIKITISHA SANA KWANI SITOWEZA FIKA, ila NAWATAKIA PARTY NJEMA NA NATUMAINI WATAKAO WEZA KUFIKA WATATUWAKILISHA VYEMA!! kila la kheli tupo pamoja!!

Dickson ni kweli kumetokea mkanganyiko. Ila next time nafikiri mambo hayatokuwa mabaya. Tuko PamoJah kiroho.

Yeah.. Yote ni mema kwani lengo kubwa ni kufanikisha party ili wanakijiji waweze kukutana na kufahamiana uso kwa uso na kubadilishana mawazo. Natumaini wakati mwingine sisi ambao tumeshindwa kufanikisha hili kwa sasa tutafanikisha wakati mwingine!!

Cha the Great said:

Dickson ni kweli kumetokea mkanganyiko. Ila next time nafikiri mambo hayatokuwa mabaya. Tuko PamoJah kiroho.

Dah! hata me nasikitika sitakuwepo kwani nipo mwanza kama kuna mwanakijiji aliopo mwanza tunaweza kuwakilisha huku nasi tukakutana japo tukala mchemsho wa samaki pamojah nikimkosa mwanakijiji hapa mwanza nitapita Arusha nitamtafuta Kaka Dixon kama itawezekana nitaonananae Inshaallah.

RSS

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*