Padre Mmoja Akiwa Kwenye Gari Alisimamishwa Na Trafic Police,Police Akiwa Anahitaji Rushwa Alianza Kuuliza Maswali Mengi, Mara Mbona Gari Lako Linatoa Moshi Mwingi? Mbona Gari Lako Matairi Yameisha, Hatimaye Polisi Akamuamuru Padre Waende Nae Kituoni.
Njiani Polisi Alimuuliza Padre, Umesema Wewe Ni Padre, Je Unabiblia Ndani Ya Gari, Padre Akajibu Ndio Ninayo, Polisi Akamuambia Padre, Pack Gari Pembeni Na Unipe Biblia.
Padre Akapaki Gari Na Kumpa Biblia Yule Polisi,
Polisi Akasita Kupokea, Akamwambia Kasisi 'Fungua Na Usome Matayo 5:25-26
Mistari Hiyo Inasema Hivi "Mtu Wa Mungu Akasoma "Malizaneni Na Aliyekukamata Kukupeleka Mahakamani.. ..Malizaneni Upesi.. Yamalize Mambo Haya Mngali Bado Njiani Kabla Hajakukabidhi Kwa Hakimu.. Ambaye Aweza Kukuhukumu Na Kukukabidhi Kwa Bwana Jela Ili Akutie Gerezani. Amin Nakwambia Hautaachiwa Hadi Umetoa Senti Ya Mwisho... Mtu Wa Mungu Akampa Yaliyo Yake Kaizari.
Polisi Akatabasamu Na Kusema 'Msifanye Migumu Mioyo Yenu.. Nenda Na Amani.
Tags:
Hahahahahaha! Trafiki noma kweli huyu hata Padre kamtoa upepo!!!???@ Bonielly
ha ha ha ha ha.....ya kaizari mpe kaizari na yamungu mpe mungu
Sawa kabisa @ Chaoga
hahaaaa, ningekuwa mimi ni padre ningemwachi hiyo biblia.
Hahahahhaahahaa ni kweli huo mstari una maneno hayo? Padri katoa rushwa bila kupenda. Eti nenda na amani.
Hahahahha.. DIsmas huyo mstari upo na kausoma mwenyewe Padri ikabidi awe mpole tu..hahaha
Msifanye migumu mioyo yenu....!
Hahahaaa.. huyu Trafiki anatumia Biblia vibaya! hahahahaa
© 2022 Created by Tulonge.
Powered by