Tulonge

Na Vitus Ngiliule

Baada ya kuhitimu elimu ya darasa la saba, nilipata wazo la kwenda Dar kwa kaka yangu. Katika kipindi hiki chote nilikua nikiishi na mama, kwani baba alifariki nikiwa na umri wa miaka miwili tu. Hivyo sikuweza kubahatika kumuona sura yake katika umri ambao mtoto anakua na uelewa wa kuweza kuwatofautisha watu..

Nilimshirikisha mama juu ya hiyo safari yangu, naye aliafiki na kunitakia baraka. Ilikua ni mida ya jioni wakati nikimshirikisha mama kuhusiana na hiyo safari. Mara tu baada ya kumaliza mazungumzo niliingia chumbani kwangu na kuanza kupaki nguo zangu, na nilipomaliza nilimuomba mama simu ili nimjulishe kaka kuhusiana na huo ujio wangu.

Nilifanikiwa kuwasiliana naye na alifurahi sana, pia akanisihi niondoke na simu ya mama kwa ajili ya mawasiliano mara tu nitakapofika jijini. Nilimfahamisha mama juu ya lile wazo la kaka la kuondoka na ile simu, kama ilivyo kawaida wazazi wetu hasa upande wa akina mama hujawa na huruma iliyo ambatana na upendo. Pasipo kinyongo chochote mama alinikabidhi ile simu nikalala nayo pale chumbani kwangu..

Kulipopambazuka mama aliniamsha nikaoga kisha nikavaa nguo zangu kwa ajili ya safari. Mara tu baada ya hapo mama alichukua akiba ya fedha yake kisha akanikabidhi kama nauli pamoja na ile ya kula nikiwa safarini. Ilikua ni kiasi cha shilingi elfu kumi na tano tu..
Mara baada ya kufika kituo cha mabasi yaendayo mikoani, tulifanikiwa kukata tiketi ya basi la shabiby lililokua likiondoka mida ya saa moja asubuhi. Tulimjulisha na kaka pia juu ya hilo. Mda ulipowadia basi lilianza kuondoka, nilimpungua mama mkono kupitia dirishani naye akanipungia. Ndani ya basi nilikaa upande wa siti ya watu wawili. kwa kuwa nilikua upande wa dirishani, yule niliyekua nimekaa naye alikua upande wangu wa kushoto. Hivyo sikuweza kumtazama vizuri kwani mda wote nilikua nikitazama nje kupitia dirishani, lakini kuna kitu kilinishtua sana kwani nywele zangu zilikua zikinisisimka isivyo kawaida. Nikapata wazo la kugeuka na kumtazama mtu niliyekaa naye. Mara tu nilipogeuka nilikutanisha macho na dada aliyekua na sura ya mvuto wa kipekee, kiukweli tangu kuzaliwa kwangu sikuwahi kumwona binti mwenye mvuto kama yule dada, alionekana kama shombeshombe fulani hivi wa kihindi.

Mara tu baada ya kugonganisha macho, nilijawa na aibu kisha nikatazama chini. Wakati nikijibalaguza kana kwamba nilikua simtazami ndipo ghafla nikasikia sauti nyororo ikipenya masikioni mwangu,”Erick mbona unawasiwasi hivyo, tatizo ni nini”, nilishikwa na kigugumizi kwani sikuwa nimezungumza naye chochote ,lakini cha kushangaza jina langu alilifahamu vipi, ”hapana dada yangu wala mimi sina wasiwasi”,nilimjibu kwa sauti ya woga. Hakuishia hapo akaniambia kwamba nimjulishe kaka yangu pindi tu nitakapofika Dar. Nilijiuliza maswali mengi sana huku nikijisemea kimoyomoyo,”amejuaje kama naenda kwa kaka yangu”. Lakini ghafla alipaza sauti na kusema,”unajiuliza nimejuaje,sikiliza Erick mimi si kama binadamu wengine unaowafikiria, hakika hi indo mara yangu ya kwanza kuonana mimi na wewe”,wakati akiyazungumza yote haya, alikua akinitazama usoni na macho yake yenye mvuto wa kipekee. Sio siri mapigo yangu ya moyo yalizidi kunienda mbio isivyo kawaida..

Itaendelea Jumatatu ijayo…

Views: 894

Replies to This Discussion

Story nzuri,yaani I am waiting 4partie 2 of this story please.

RSS

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*