Tulonge

Na Vitus Ngiliule

 

Ghafla yule mtu alisimama na kuanza kuja ule upande wa siti yetu, sikuendelea kumtazama kutokana na ile hofu niliyokuwa nayo. Hapa sasa nililikaa tayari kwa chochote kilichokuwa kinakuja kutokea. Yule mtu alikuja moja kwa moja na alipofika maeneo ya siti yetu alisimama kisha akavua miwani yake na kuanza kututazama akiwa amekunja uso.Alifanya hivi kwa muda wa sekunde kadhaa kisha akaivaa ile miwani na kuanza kutembea kwa kasi sana kuelekea chini. Nilibaki nimeshikwa na butwaa nisielewe huyu mtu alikuwa na nia gani na sisi. Mara tu baada ya yule mtu kushuka nilichukua lile begi langu la nguo. Yule dada naye akachukua ile briefcase yake nyeusi kisha tukaanza kutembea kuelekea ule mlango wa kushukia kwani watu wote walikuwa tayari wamekwisha shuka hivyo mle ndani tulibaki mimi tu na yule dada.

Tulipofika chini nilijaribu kutazama pembeni nikaona gari moja nyeusi imepaki pembeni kidogo kutokea kwenye lile basi tulilokuwamo, sikuweza kuitazama vizuri lakini ilionekana kama aina ya Nissan patrol. Yule dada alinishika mkono na kuanza kuniongoza kuelekea kwenye ile gari na tulipokaribia ule mlango wa mbele na ule wa nyuma upande wa kushoto ilifunguka kwa ghafla kisha yule dada akaniamuru niingie kupitia ule mlango wa nyuma na yeye akaingia kupitia ule mlango  wa mbele. Mara tu baada ya kuingia ile milango ilijifunga. Nilichukua lile begi langu la nguo kisha nikaliweka upande wangu wa kulia kwenye ile siti iliyokuwa wazi.

Haikuchukuwa muda ile gari tuliyokuwamo ilianza kuondoka kuelekea lile lango kuu la kutokea, nilijaribu kutazama mbele ili nimuone dereva  aliyekuwa akiendesha ile gari lakini alikuwa amenipa mgongo  hivyo niliweza kumuona kupitia ile site mirror ya mbele. Nilistaajabu sana baada ya kumuona huyo dereva kwani alikuwa ni yule kaka mwenye suti nyeusi na ile miwani mieusi  tuliyekuwa naye kwenye lile basi. Mapigo yangu ya moyo yalizidi kunienda mbio sana lakini nikajifariji kwamba liwalo na liwe.

Ilikuwa inaelekea majira ya saa tisa alasiri wakati tukiwa njiani kuelekea nyumbani kwa huyo dada, mle ndani ya gari palikuwa kimya sana kwani hakuna mtu yeyote aliyekuwa akimsemesha mwenzie. Tuliendelea kukata mitaa ya jiji la Dar hivyo nikajikuta nimeshapoteza mwelekeo sielewi mashariki ni wapi wala magharibi kutokana na ugeni wangu katika hili jiji.

Haikuchukua muda mara tu baada ya kumaliza baadhi ya mitaa, ghafla ile gari ilisimama na nilipojaribu kutazama mbele niliona geti kubwa jeusi lenye picha ya yule dada niliyekuwa naye. Ghafla lile geti lilifunguka pasipo hata kupiga honi kisha ile gari ikaingia moja kwa moja hadi mle ndani na lile geti likajifunga nilijaribu kutazama nje kupitia kioo cha nyuma ili nimuone huyo aliyefungua lile geti lakini sikumuona mtu yeyote.

Itaendelea jumatatu ijayo..

Views: 607

Replies to This Discussion

huu mwendo wa pole pole tutaendanao mpaka nione mwisho wake.. tehe

teh teh Dixon hukati tamaa c o? Ila nimeongea na muhusika, kasema atazidisha urefu kidogo

RSS

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*