Tulonge

Na Vitus Ngiliule

Wakati nikiwa bado nimeshikilia ile simu mkononi sielewi nini cha kufanya, ghafla nilishtushwa na sauti iliyotokea upande wangu wa kushoto, hakika alikiwa ni Hidaya akisema, “Erick, nilishakwambia ya kuwa nipo kwa ajili ya kukusaidia hebu naomba uwe na imani na mimi”, aliongea huku akinitazama kwa makini sana. “nimekuelewa dada Hidaya “, nilimjibu kwa mkato huku nikitetemeka sana. Alitikisa kichwa kisha akaegamia siti yake. Niliichukua ile simu kisha nikaiweka kwenye mfuko wangu wa suruali, haya yote niliyafanya kwa kutumia mkono wangu wa kulia kwani ule wa kushoto ulikua bado umeshikilia ile pini.

Tulipokaribia kuingia maeneo ya ubungo, ghafla basi letu lilisimama tena lakini sikufahamu kilichokua kikiendelea kwa wakati huo, nilijaribu kusimama na kutazama mbele ndipo nilipoona msongamano mkubwa wa magari hivyo nikafahamu fika ya kuwa ile ilikua ni foleni ya magari. Tulikaa takribani muda wa dakika ishirini na tano hivi ndipo basi letu likaendelea na safari.Ilikuwa inaelekea majira ya saa tisa alasiri. Safari yetu iliendelea na hatimaye tukaingia kituo cha mabasi ubungo, basi letu lilisimama kuashiria kuwa ndo mwisho wa safari ndipo abiria wengi wakaanza kutelemka na kushusha mizigo yao. Wakati mimi na yule dada tulikuwa bado tumekaa kwenye siti, nilijaribu kunyanyuka kutoka kwenye siti yangu kisha nikamuomba yule dada nipite ili nishushe begi langu la nguo, aliishia kunitazama tu kisha akaniuliza, “unapokwenda unapajua?“. Lilikua ni swali ambalo limeambatana na ukweli ndani yake, “hapana dada yangu, napafahamu kwa jina tu lakini sikuwahi fika”, nilimjibu huku nikiingiza mkono wangu mfukoni kutoa ile simu ili niendelee kumtafuta kaka. Lakini jambo la kustaajabisha ile simu haikuwako mfukoni, nilijaribu kuangalia mifuko yangu ya nyuma ya suruali pamoja na ile sehemu niliyokuwa nimekaa lakini sikuweza kuiona. Nilishusha pumzi kisha nikakaa tena kwenye siti yangu, niliishiwa nguvu kabisa nikajihisi kama vile nimechanganyikiwa.

Wakati nikiendelea kujiuliza jinsi ile simu ilivyopotea, ghafla yule dada alinishika mkono wangu wa kushoto uliokuwa na ile pini kisha akaninyanyua na kusema, “Erick tunaweza kwenda sasa wala hata usiwe na wasiwasi.Mimi nitakuwa mwenyeji wako kwenye hili jiji”, nilihamaki na kuuliza, “kwani wewe unaishi wapi dada yangu”, kisha akanijibu kwa kusema ya kuwa anaishi maeneo ya mbezi beach. Niliishia kutikisa kichwa tu kana kwamba napafahamu lakini kumbe sikufahamu. Watu wote walikuwa wamekwisha telemka hivyo nikadhani ya kuwa tumebaki wawili tu mle ndani ya basi lakini nilipojaribu kutazama upande wa siti za nyuma, ghafla nilimuona yule kaka aliyekuwa amevalia suti nyeusi na miwani mieusi  akinitazama akiwa amekunja uso.


Itaendelea jumatatu ijayo…!

Views: 679

Replies to This Discussion

jamani.. fanya iwe ndefu ndefu kidogo... Dah!!!

Hahahhahaha Dixon, c ww peke yako unayehitaji hivyo.Anakatisha utamu c o?

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*