Tulonge

Na Vitus Ngiliule

Nilihisi moja kwa moja kuwa ile pini yule dada ndiye aliniwekea kwenye mkono wangu, lakini jambo la kushangaza nilipojaribu kumtazama alionekana bado amelala usingizi kabisa. Nilizidi kuwa na maswali mengi sana kichwani mwangu.Niliichukua ile pini na kuihamishia mkono wangu wa kulia kisha nikaendelea kuitazama kwani ilikua ikinivutia sana  machoni.Wakati macho yangu yakiwa bado yanaitazama ile pini,ghafla nilihisi nashikwa bega langu la kushoto, nilipogeuka nilikutana uso kwa uso na yule dada, aliangua kicheko huku tukiwa tumetazamana na kisha akaniuliza “vipi Erick..! umepata mzigo wangu?”, nikamjibu kama mtu ambaye hafahamu chochote, “hapana dada idaya”. Mara tu baada ya kumjibu hivyo hakuishia hapo kisha akaniamuru nifungue mkono wangu wa kulia, nilistaajabu sana, aliwazaje kufahamu ya kuwa ile pini nimeihamishia mkono wangu wa kulia. Nilifungua mkono wangu wa kulia huku nikitetemeka sana, mle ndani ya basi kulikuwa na upepo sana uliokuwa ukipitia dirishani, kwani dirisha letu lilikuwa wazi, lakini huwezi amini kwa jinsi jasho lilivyokuwa lilikinitiririka.


Mara baada ya kuufungua ule mkono, ile pini ilionekana kisha akaichukua na kuihamishia mkono wangu wa kushoto kisha akasema, “Erick mzigo niliokuwa nikiuzungumzia ni hii pini, naomba uitunze kama mboni ya jicho lako”, nilishikwa na kigugumizi kiasi kwamba nikashindwa kuzungumza chochote. Aliendelea kwa kusema, “najua utakuwa umenielewa, naomba ulizingatie sana hilo”, nilitikisa kichwa ishara ya kukubaliana na kile alichokisema, aliacha kunitazama kisha akaegemea siti yake.


Ghafla basi letu lilisimama, kuna abiria waliokuwa mbele ya siti yetu walizungumza kwa sauti na kusema kuwa yale yalikuwa ni maeneo ya kibamba, hivyo nilifahamu fika ya kuwa tumeshakaribia kuingia ubungo. Niliwahi kusimuliwa kuwa ukifika haya maeneo unakuwa umekaribia ubungo, hivyo nilikuwa nina ulewa kidogo japo ni kwa kusimuliwa tu. Wakati basi letu likiwa bado limesimama, ghafla alipanda kijana mmoja akiwa amevalia suti nyeusi na miwani myeusi, kwa kumtazama alionekana akiwa na umri kati ya miaka ishirini na kitu hivi. Hakuwa mtanzania kwani alionekana kama chotara wa kisomari kutokana na rangi yake na muonekano wa nywele zake. Baada ya kuingia ndani ya basi alianza kuja moja kwa moja kuelekea siti za nyuma na alipofika usawa wa siti yetu,alisimama kisha akavua ile miwani yake na kuanza kututazama kwa makini sana, alitikisa kichwa chake kama mtu anayesikitika hivi kisha akaelekea siti moja ya nyuma iliyokuwa wazi.

Niliendelea kujihoji maswali mengi sana kichwani mwangu lakini sikupata jibu ya kilichokua kikiendelea kati yetu sisi na yule kijana. Wakati yote haya yakiendelea Hidaya alikuwa amelala usingizi kabisa, nilijaribu kunyanyua shingo yangu kisha nikageuka nyuma kumtazama yule kaka, nilikutana na jicho kali sana la yule kijana akinitazama akiwa amekunja uso wake. Mapigo yangu ya moyo yalinienda mbio sana  nikashusha shingo yangu kwa haraka sana kisha nikajikausha kana kwamba nilikuwa simtazami yeye. Ilituchukua kama nusu saa wakati basi letu likiwa bado limesimama hayo maeneo ya kibamba, ndipo tukaanza safari. Nilitoa simu yangu tena ili nijaribu kumtafuta kaka lakini mambo yalikuwa ni yale yale, kwani namba yake haikuweza kupatikana..


Itaendelea jumatatu ijayo…!

Views: 542

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*