Tulonge

Frank Maige alisoma Malangali High School 2001-2003. Alifariki tarehe 1 Aprili 2013 baada ya kupooza sehemu ya mwili. Zifuatazo ni baadhi ya picha za shughuli ya mazishi yake toka hospitali ya Muhimbili Dar hadi Makaburi Kinondoni.

Frank enzi za uhai wake

Mwili wa marehemu ukitolewa chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Muhimbili kwenda Kanisani kwa ibada. Kanisa lipo hapo hapo Muhimbili.

Tukiingia kanisani kwaajili ya Ibada

Watu ndani ya kanisa wakiendelea na ibada

Historia fupi ya marehemu ikisomwa

Mwakilishi wa wanafunzi wa Malangali Godfrey akiongea kwa niaba ya wanafunzi wa Malangali High School

Mwakilishi wa Chuo Kikuu Dodoma ambapo pia Frank alisoma Shahada ya Ualimu

Jeneza lenye mwili wa marehemu likiwa kanisani

Ulifika wakati wa kutoa heshima za mwisho. Jeneza likiwa limefunuliwa. Huyo aliyesimama pembeni ni Simon Ndee ambaye alikua rafiki wa karibu sana na Frank. Walisoma pamoja Malangali High School na UDOM

Baada ya heshima za mwisho, mwili ulifanyiwa maombi ili kuanza safari ya makaburini (Kinondoni)

Mwili ukitolewa nje ya kanisa kuelekea makaburini

Hapa ndipo Frank alipo pumzishwa

Mungu alitoa, na sasa ametwaa. Jina lake lihimidiwe.

AMEN

Views: 648

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*