Tulonge

Wadau wa Malangali High Shool ni tukio gani linalokufanya uikumbuke Malangali hadi leo??

Je una chochote kinacho kufanya uikumbuke malangali hadi muda huu. Ni kipi hicho,hebu tushirikishe. Kama una picha ya tukio hilo unaweza tuwekea pia.2po pa1

Views: 465

Replies to This Discussion

tukio ambalo sitakuja kulisahau, kuna cku walikuja kututembelea wanafunzi wa boarding watatu please sitawataja majina yao, sasa baba mwenye cjui na uganga wake cku hiyo aliamkaje na haijawai kutokea akaniita mimi, mimi nikakauka baadaye kamwita mwenzangu akaitika baadaye akamuuliza je humo katika vyumba vyenu kuna watoto wa kiume? mwenzangu akasema ndio baba akauliza ni wavulana wa boarding akajibu ndio wakati anamuuliza yule mwenzangu mie nilishakuwa nimeenda chumbani kwa mwanae mmoja yeye alikuwa akisoma Itengule Sec. nasikilizia hapo baadaye akatuita wote kwa sababu pale tulikuwa tumepanga wasichana wanne sisi watatu tulikuwa tunakaa chumba kimoja mwenzetu mmoja alikuwa na chumba chake na ndiko huko hao wanafunzi wa boarding tulikokuwa tumewakaribisha.

 

Dingi akasema haya ingieni humo ndani kule waliko wale wavulana, wakati huo mimi nimeminya kule chumba cha yule mwanae nasikilizia tu dakika kama chache nasikia kipigo tena kipigo hasa, baada ya muda kidogo baba ba wale wenzangu nje, wakati huo mimi sasa nilishachnaganyikiwa cjui nifanyeje du mbona balaa. baba hakufanya ajiza kaenda kumwita balozi nae balozi akaja baba akamweleza mimi nashindwa kuwaelewa hawa watoto wamekuja kusoma lakini wanawakaribisha wavulana wa boarding muda wa usku kwa nini na wao wanatakiwa kuwa shuleni kaelezaeleza pale tukaulizwa hawa wavulana walikuja kufanya nini mmoja kati yetu akajibu kwa kumtaja mvulana fulani kuwa huyo ni bwana Aggy yaani mimi sasa, baba sasa wewe Aggy umekuja kusoma au ndo umekuja kuchakachuliwa? ukiangalia kweli walimsindikiza mwenzake alikuwa anakuja kwangu ndo anafukuza mzigo na hajaupata na kipigo juu acha, ilikuwa bonge la soo, nitaendelea wiki ijayo. Jumatatu njema

Hahahahahaa sawa Agnes,umenichekesha balaa
Ila Aggy nahisi umetuficha baadhi ya mambo,ni kweli huyo jamaa alikua anakufukuzia na alikua hajafanikiwa?Mbona kama nina wacwac na hili teh teh teh.
kaka Dis ndo alikuwa anafukuzia tu, yaani alikuwa kwenye application maombi yalikuwa bado hayajajibiwa.

Duh safi kukumbushana maisha ya kidato,huwa ni maisha hayatakiwi kusahaulika,mi nadhani ningelikuwa na mengi ya kukumbushia hapa kama ningelikuwa mmoja wa Malangali High School.

RSS

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*