Tulonge

meli ya uchunguzi wa uchimbaji wa mafuta Kilwa, coz kuna mafuta mengi sana hapa

Views: 205

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by KUNAMBI Jr on November 24, 2011 at 10:29

Mama malaika nahisi tushafikia huko maana tz kila siku machafuko haswa yakichochewa na vyama pinzani now raia washachoka sasa tuombe mungu tuone nn kitatokea.

Comment by Mama Malaika on August 3, 2011 at 11:33

Kumbai Jr.... wageni wanafanya Tanzania mabwege makusudi sababu ya viongozi na serikali ya Tanzania inawabeba. Serikali ina power kila sababu za kuwapa 24hrs wageni waondoke na kuwatimua kama vile Nyerere alivyofanya 1967 au alivyofanya Idd Amin wa Uganda kuwatimua waganda wote wenye asili ya kiasia (Wahindi), waarabu na wazungu nchini Uganda kipindi cha utawala wake.

 

Iko siku wananchi watachoka na kuamua kuingia mtaani kwa kishindo kupata/kuchukua haki yake kwa kutumia bullet instead of ballot.

Comment by KUNAMBI Jr on August 2, 2011 at 11:59

ki ukweli hata me imenisikitisha sana hii,lkn hawa wageni kwa nn watufanye sie kama mabwege tena kwenye nchi yetu wenyewe,au ndo sasa kila mtu afe na chake???

Comment by Dixon Kaishozi on August 2, 2011 at 11:08
"You cannot break the will of the people when their time to demand their right comes!!!" hapo ndipo patakavyo chimbika hapa kwetu!!
Comment by chaoga on August 2, 2011 at 9:11
kunambi hiyo habari ya dinossaur nimeisikia juzi redioni kwamba mifupa inatunzwa huko makumbusho ya ujerumani, eti sisi mpaka tukiwa na uwezo wa kuyahifadhi hayo mabaki ndio tutarudishiwa... sasa sijui tunafaidika vipi nitamuomba mwanakijiji mwenzetu magere afuatilie habari hii
Comment by Mama Malaika on August 1, 2011 at 15:15

Ukipata muda soma hii link... si siri nimeshikwa machozi na sikujua kama Tanzania nchi niipendayo Dec. 2011 inasheherekea miaka 50 ya Uhuru lakini bado kuna watu wanaishi maisha mashaka na wana nyanyaswa ndani ya ardhi na nchi yao waipendayo.

Niko kwenye campaign ya hawa ndugu zetu....

 

http://allan.lissner.net/someone-elses-treasure-tanzania/#comment-6444

 

Comment by Mama Malaika on August 1, 2011 at 15:01

Hii yauma sana.. naona itafikia kipindi watu tushikane mashati kwani Tanganyika itakuwa huru pale mafisadi wote wataposhikwa watapotoweka machoni. Hapo wenyeji wazaliwa wa Kilwa hawatoambulia chochote kama vile wenzao wanaoishi vijiji vizungukavyo Niger Delta. Nimesoma kwenye gazeti moja la nje kuwa serikali ya Tanzania imefanya ku-sign mkataba kuruhusu wawekezaji wazungu wataanza kuchimba madini ya Uranium toka katikati ya Selous Game Reserve bila kujali EIA (Environmental impact assessment). Kama kweli mizimu wanafanya miujiza basi mie nasubiria mzimu wa Frederick Selous uje uwakomeshe.

Ujue hawa wezi wanaoletwa na viongozi walafi wa serikali ya Tanzania. Kiongozi wa nchi anasafiri eti kwenda tafuta wawekezaji.... kama sio kwenda tafuta wezi? Wawekezaji wazuri wanajileta wenyewe na hawafatwi kama wale wanaokuja Tanzania na ndio maana wenzetu wa Congo wanapata kodi nzuri/kubwa toka kwa wawekezaji wao wa madini. Wazungu wezi watakomba vyote na kutuachia mashimo wakati kwao dhahabu na almasi wameiacha ardhi hawachimbi. Barrick Mining Co. huko kwao Canada kaskazini kuna almasi na dhahabu ya kumwaga lakini wanakuja Tanzania kukomba vya bure bure bila hata ya kulipa kodi ipasayo. Mwl. Nyerere kuweka Azimio la Arusha hakuwa mjinga kwani aliona mbali kuwa hawa watu (wageni kipindi hicho 1967) watatuzidi akili.

Comment by KUNAMBI Jr on May 15, 2011 at 15:32

hilo nalo neno mkuu @Dixon

but one day itatokea miujiza tu, hapahapa kilwa ndo sehemu ambayo wale wanyama waliotoweka miaka milioni moja huko nyuma kwa jina maarufu Godzila au Dinnousoses kama sijakosea spelng walipofia, kuna mabaki ya mifupa yao katika kijiji kimoja kinaitwa Mbwemkuru-Mipingo,hiyo ni sifa tosha ila sie tumelala tu,mpk mifupa imeibwa na kupelekwa ujerumani kwenye makumbusho ya huko sasa hii si ni hatar jaman........................

Comment by Dixon Kaishozi on May 11, 2011 at 22:30
Sisi tutabaki kuwa watoa mali ghafi kwenda nje alafu tunauziwa product kwa gharama ambayo hatuiwezi.. inauma sana.
Comment by KUNAMBI Jr on May 11, 2011 at 7:41

mafuta kama yanayochimbwa uarabuni @Severine

Asante sana dada Belita

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*