Tulonge

Maalim Michuzi Jr
 • Male
 • Dar es Salaam
 • Tanzania, United Republic Of
Share

Maalim Michuzi Jr's Friends

 • mohamed selemani kilumba
 • ANGEL NEHEMIAH
 • Oswald
 • BARAKA FRANCO CHIBIRITI
 • Ndekia
 • CataLina Moshi
 • Lucie
 • Majoy
 • Chui Mfalme
 • mwinyi mpeku
 • mtotomzuri
 • ladymwana
 • Belita
 • Mama Malaika
 • Kisusi Mohammed

Maalim Michuzi Jr's Discussions

Wandugu Salamaaaa

Started this discussion. Last reply by CHA the Optimist Sep 25, 2010. 5 Replies

Ni furaha kubwa sana kwangu kuona libeneke la lugha yetu ya kimatumbi inazidi kupamba moto katika mitandao jamii kama hii.shukrani za dhati kwake Dismas kwa kulianzisha libeneke hili la Tulonge kwani…Continue

MTAA KWA MTAA

TCRA yashiriki mbio za mwenge maalum 2021 Ipagala jijini Dodoma

Baadhi ya viongozi wakipata huduma za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Wakati Mwenge wa Uhuru ulipokwenda katika Shule ya Msingi ya Ipagala B jijini Dodoma.
Afisa Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Mabel Masasi  akikabidhi kitabu cha Mwongozo wa Huduma kwa Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Tanzania kwa viongozi wa Mbio za Mwenge Maalum 2020/21 ikiwa ni ishara ya TCRA kuunga mkono kauli mbiu ya mbio za mwenge mwaka huu isemayo "TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu; itumike kwa usahihi na uwajibikaji"
Afisa Mawasiliano Mwandamizi  wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabel Masasi akiwapa maelezo viongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru ulipowasili katika  Shule ya Msingi Ipangala 'B' iliyopo jijini Dodoma wakati wa mbio za Mwenge Maalum 2020/21 ikiwa ni ishara ya TCRA kuunga mkono kauli mbiu ya mbio hizo isemayo "TEHAMA ni msingi wa wa Taifa endelevu; itumike kwa usahihi na uwajibikaji"


Baadhi ya viongozi wakipata huduma za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Wakati Mwenge wa Uhuru ulipokwenda katika Shule ya Msingi ya Ipagala B jijini Dodoma.
Afisa Habari wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Robin Ulikaye akiwapa elimu wanafunzi wa shule ya msingi Ipagala B Wakati TCRA ikiwa katika ushiriki wa kutoa elimu katika mbio za Mwenge wa Uhuru jijini Dodoma.

RITA YAWASHAURI WANAFUNZI WANAOFANYA UHAKIKI WA VYETI VYA KUZALIWA NA VIFO KUZINGATIA MAELEKEZO

  Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

WAKALA wa Usajili Ufilisi na Udhamini(RITA) Umewataka wanafunzi wanaofanya uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa na vyeti vya vifo ili kupata mikopo ya elimu ya juu kuzingatia hatua za uhakiki huo.
 
Akizungumza leo Julai 28,2021 kutoka kwenye banda la RITA katika maonyesho ya 16 ya Elimu ya juu, Sayansi na Teknolojia, Ofisa Habari wa RITA, Grace Kyasi amesema baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakikosea hatua za kutuma maombi yao ya uhakiki wa vyeti.

Ambapo wamekuwa wakitumia njia ya barua pepe ya Wakala ambayo ni info@rita.go.tz badala ya kutuma maombi yao kupitia ukurasa wa huduma mtandaoni unaojulikana kama E-huduma ambapo mwanafunzi anatakiwa aingie kwenye tovuti ya www.rita.go.tz na kisha aingie kwenye kipengele cha E-huduma ili kutuma taarifa zake.
 
Grace amesema kuwa ili maombi ya uhakiki wa vyeti vya mwanafunzi yapokelewe na kufanyiwa kazi kwa ufasaha, mwanafunzi anatakiwa ajisajili kwa kujitengenezea akaunti yake katika ukurasa wa RITA huduma mtandaoni na kisha kuingia katika kipengele cha uhakiki na kutuma maombi ya taarifa zake ili ziweze kushughulikiwa na kujibiwa kwa wakati.
 
Aidha amesema mpaka sasa tayari jumla ya maombi 84,387 yameshahakikiwa na kurudishwa kwa wanafunzi ili kuweza kuendelea na utaratibu wa kuomba mikopo katika ofisi ya Bodi ya mikopo elimu ya juu.
 
"Pia tunapenda kuwakumbusha wanafunzi kutumia simu yetu ya huduma kwa wateja ambayo ni 800117482 iwapo watahisi kupata changamoto yoyote katika utumaji wa maombi yao ya uhakiki." amesema na kuongeza RITA umeshiriki katika maonyesho ya 16 ya Elimu ya juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania(TCU) yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 
Amesema kaatika maonyesho hayo RITA inatoa huduma ya Usajili wa vyeti vya kuzaliwa pamoja na Elimu kwa Umma kuhusu huduma ya Vizazi,Vifo,Ndoa,Talaka,Udhamini,Ufilisi, Wosia na Mirathi hivyo wananchi wote wanakaribishwa kutembelea banda la RITA ili kufaidika na huduma hizo mahususi.
 
Mgeni rasmi katika sherehe za uzinduzi wa maonyesho hayo yaliyoanza tangu tarehe 26 na kutarajiwa kuhitimishwa tarehe 31 Julai alikuwa ni Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Zena Ahmed Said. Afisa habari kutoka RITA, Bi. Grace Kyasi akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda la RITA katika Maonesho ya 16 ya Elimu ya juu, Sayansi na Teknolojia yanayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Ilala leo.

Wananchi wakipata huduma mbalimbali katika banda la RITA viwanja vya mnazi mmoja leo.

NMB Yakabidhi Hundi ya Sh. Milioni 438.4 kwa Waathirika janga la Moto Kariakoo

Benki ya NMB kupitia Kampuni ya Reliance Insurance, imewalipa bima ya Sh. Milioni 438.4 wafanyabiashara 12, kati ya waliounguliwa moto maduka yao katika Soko la Kariakoo, Julai 10 mwaka huu. Wafanyabiashara hawa ni waliokuwa wamekatia bima mikopo na biashara zao kupitia NMB.

Hafla ya kuwakabidhi wafanyabiashara hao hundi hiyo, imefanyika katika Tawi la NMB Kariakoo Business Center, ambako wahanga hao walikiri kuwa hasara na maumivu yao ya kuunguliwa yamepozwa na malipo hayo ya haraka ya bima.

Akizungumza kabla ya kuwakabidhi hundi ya mfano, Mkuu wa Kitengo cha Bima Benki ya NMB, Martine Massawe, alitoa wito kwa Watanzania kujenga utamaduni chanya wa kuzilinda kwa bima mali na pesa wanazotafuta kwa jasho, ili kuepuka maumivu yasiyo na mfariji wakati wa majanga.

“Tuko hapa kwa ajili ya kuwafuta machozi wafanyabiashara waliokata bima nasi kupitia mikopo yao ama waliokuwa na bima za mali bila mikopo, ambao walikuwa sehemu ya wahanga wa moto sokoni Kariakoo.

“Wito kwa Watanzania, moto wa Soko la Kariakoo uwe fundisho kwao juu ya umuhimu wa bima. Moto ama majanga huja bila kuyatarajia, unapokata bima unakuwa umejiwekea kinga kuilinda pesa ama mali uliyotafuta kwa jasho lako.

“Uwepo wa bima hukurejeshea nguvu haraka kana kwamba hakuna janga lililokutokea. Wito huu sio tu kwa bima za mikopo, bali mali zote kwani gharama za bima hizi ni nafuu mno,” Akisisitiza umuhimu na unafuu wa bima hizo, Massawe alitolea mfano wa bima ya moto kuwa hukatwa asilimia 0.25 ya thamani ya mali, na kwamba kama mali ya Sh. Mil. 100, makato yake ya bima ni Sh. 150,000 tu bila V.A.T kiasi ambacho ni rahisi kuliko bima za magari.

Kwa upande wake, Joel Mwakalebela, ambaye ni Meneja Madai wa Kampuni ya Reliance Insurance, aliwapongeza wahanga hao kwa uamuzi wao wa kukata bima, huku akisisitiza Watanzania kutosubiri mikopo ili kukata bima, badala yake watumie huduma hizo ili kujilinda na majanga.

“Tunawashukuru NMB kwa ushirikiano huu mwema uliowezesha malipo ya haraka kwa wahanga hawa. Wito wetu kwa Watanzania ni kutumia huduma zetu, ambazo zinapatikana katika kila tawi la NMB lilipo kote nchini,” alibainisha Mwakalebela.

Akizungumza katika hafla hiyo, Emmanuel Mbise, ambaye ni mmiliki wa maduka 2 yaliyoteketea kwa moto, alifichua kuwa maumivu waliyoyapata wahanga wa tukio hilo ni makubwa, lakini malipo ya bima kutoka NMB, yanawapa hafueni na faraja kubwa.

Naye Sajida Kagasheki, ambaye pia ni mmoja wa wahanga, alikiri kupata faraja kubwa kupitia malipo hayo ya bima, huku akiwataka Watanzania kukimbilia sana huduma za bima hasa kupitia NMB Bancassurance, ambazo ni mkombozi na mfariji wa kweli wakati wa matatizo kama ya moto, vifo, ulemavu, upotevu na kadhalika.
Meneja wa Madai wa Kampuni ya Bima ya Reliance, Joel Mwakalebela akipongezana na mmoja wa wafanyabiashara waliounguliwa na Moto katika Soko Kuu la Kariakoo, Emmanuel Kabadi (kushoto) baada ya Benki ya NMB kukabidhi mfano wa hundi ya zaidi ya Shilingi Milioni 438 kwa wafanyabiashara 12 waliokuwa na Bima. Kushuto ni Sajida Kagasheki mmoja wa wafanyabiashara na Kulia ni Meneja wa Bima wa Benki ya NMB, Adam Nsenga.
Mkuu wa Kitengo cha Bima Benki ya NMB, Martine Massawe akizungumza wakati wa kukabidhi mfano wa hundi kwa wafanyabiashara waliokuwa na Bima waliounguliwa katika Soko Kuu la Kariakoo. Kushoto ni Meneja Madai wa kampuni ya bima ya Reliance, Joel Mwakalebela na kulia ni Meneja wa Bima Benki ya NMB, Adam Nsenga.Mkuu wa Kitengo cha Bima wa Benki ya NMB, Martine Massawe(katikati) akikabidhi mfano wa hundi ya Sh. Milioni 438 kwa wafanyabiashara 12 waliokuwa na Bima waliounguliwa katika Soko la Kuu la Kariakoo, Sajida Kagasheki na Emmanuel Kabadi (kushoto) wakati wa makabidhiano yaliyofanyika katika katika Tawi la NMB Kariakoo Business Center. Kutoka kulia ni Meneja wa Bima wa Benki ya NMB, Adam Nsenga na Meneja wa Kampuni ya Reliance, Joel Mwakalebela.

RAIS DK. MWINYI AWATAKA WADAU KUJITOKEZA KUUNGA MKONO UJENZI WA MABWENI YA WANAFUNZI KAMPASI YA KARUME-ZANZIBAR

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla akizungumza katika hafla ya  uwekaji wa Jiwe la msingi la Ujenzi wa Mabweni ya Chuo cha Kumbukuku cha  Mwalimu Nyerere  Kampas ya Zanzibar. Baadhi ya washiriki katika uzinduzi wa uwekaji wa jiwe la msingi la Chuo cha Kumbukukumbu  cha Mwalimu Nyerere Kampas ya Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla akiweka Jiwe la msingi la Ujenzi wa Mabweni ya Chuo cha Kumbukuku cha  Mwalimu Nyerere  Kampas ya Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema uwepo wa Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu  Nyerere visiwani Zanzibar  ni kielelezo Chanya katika kuenzi na kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa Vitendo.

Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameleza hayo kupitia hotuba alioisoma kwa niaba ya Rais Dk. Hussein Mwinyi  katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la mradi wa ujenzi wa mabweni ya wanafunzi  wa chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere – Kampasi ya Karume Zanzibar.

Ameleza kuwa, Bodi pamoja na uongozi wa chuo hicho wamekuwa wakifanya kazi nzuri kwani tangu kuanzishwa kwa chuo hicho mnamo mwaka 1961 mpaka sasa chuo kimekuwa kinaishi kwa mawazo ya waasisi wa Taifa la Tanzania Hayati Mwalimu J.K Nyerere na Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume.

Alifafanua kuwa, Ni ukweli usiopingika wahitimu wanaotoka katika chuo hicho baada ya kumaliza mafunzo yao hutoka wakiwa wameiva , wenye uwadilifu na uweledi wa hali ya juu jambo ambalo lina umuhimu kwa watu ambao hupewa dhamana katika nafasi za utumishi wa Umma.

Pamoja na mambo mengine, Makamu wa Pili wa Rais amemuomba mkandarasi wa mradi huo ambae ni SUMA JKT kukamilisha mradi huo kwa wakati uliopangwa kwani mradi huo unalenga kutatua changamoto kubwa iliopo kwa wanafunzi ya kukosa makaazi.

Kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Simai Mohamed Said ameupongeza uongozi wa Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kuhakikisha yale malengo waliojiwekea ya kutoa mafunzo ya uongozi na uzalendo kwa jamii yanafikiwa.

Aidha, Mhe. Simai aliukumbusha uongozi wa Chuo hicho mbali na mafunzo ya uongozi na uzalendo wanayoyatoa lakini pia ipo haya yua kuangalia upya uwezekano wa kuwafanya wanafunzi wawe na uwezo wa kufanya vitu vingi kwa pamoja kwa kuzingatia masuala ya Ubunifu na Uvumbuzi kama zinavyofanya nchi nyengine Duniani.

Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila ametumia fursa hiyo kumshukuru na kumpongeza Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa jitihada anazoendelea katika kukuza uchumi wa Zanzibar.

Akigusia changamoto zinazokikabili chuo hicho kwa kampasi ya Karume Zanzibar amesema kumekuwepo kwa changamoto ya baadhi ya watu kuvamia eneo la chuo tangu mwaka 2018 na kumuomba mgeni rasmi kulipatia ufumbuzi suala hilo kutokana na kurejesha nyuma jitihada za chuo hicho.

Akisoma Taarifa ya utekelezaji wa mradi huo  Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la uzalishaji Mali la jeshi la kujenga Taifa (SUMA-JKT) Kanali Absolonon Lyanga Shausi amesema wanaishukuru serikali ya mapinduzi Zanzibar kupitia wakala wa majengo Zanzibar kwa kuisajili SUMA-JKT kuweza kufanya kazi zake Zanzibar na kuahidi kuwa mradi huo utakamilika ndani ya wakati uliopangwa wa kipindi cha miezi 18 huku ikizingatia weledi katika utekelezaji wake. 

Katika kuunga mkono jitihada za kukamilisha mradi wa ujenzi huo Mbunge wa Jimbo la Mpendae kwa niaba ya Turky Foundation amechangia jumla ya Shiliingi Millioni Ishirini (20,000,000/=) ikiwa ni kuitikia wito wa wadau wa maendeleo waliopo Zanzibar kujitokeza kusaidia kufanikisha mradi huo. 

Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)

Julai 26, 2021.


Gifts Received

Gift

Maalim Michuzi Jr has not received any gifts yet

Give a Gift

 

Maalim Michuzi Jr's Page

Profile Information

Occupation
Baba Lishe
Email Address
othmanmichuzi@gmail.com
Phone No
+255 (0) 713 775 869

Latest Activity

Mama Malaika left a comment for Maalim Michuzi Jr
"Happy Birthday Maalim Michuzi!"
Mar 2, 2014
Mama Malaika left a comment for Maalim Michuzi Jr
"Happy Birthday!"
Mar 2, 2013

Maalim Michuzi Jr's Photos

 • Add Photos
 • View All

Comment Wall (23 comments)

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

At 1:12 on March 2, 2014, Mama Malaika said…
Happy Birthday Maalim Michuzi!
At 22:08 on March 2, 2013, Mama Malaika said…

Happy Birthday!

At 21:22 on March 2, 2012, Mama Malaika said…

Happy Birthday!

At 6:49 on July 28, 2011, Lilian said…
At 3:10 on February 15, 2011, Joan said…
Habari yako kaka
At 21:34 on October 28, 2010, Belita said…
MImi nipo kaka Michuzi, hv ww na Issa Michuzi ni diferenti kala one pipo ?hahhaahaha .Ni ndugu yako?
At 14:27 on October 27, 2010, Tulonge said…
Hahhahahahhaaa acha uhuni mkuu, unajifanya umesahau kuwa hujanipa kodi kabisa. Muda wa kukudai umefika acha kuzuga hahahhaaa. Pa1 sana mkuu.
At 21:38 on October 16, 2010, CHA the Optimist said…
PamoJah
At 21:37 on October 16, 2010, CHA the Optimist said…

At 21:57 on October 14, 2010, Moreen said…
Nashangaa huonekani,nikajua wifi amekutaiti sana hadi unashindwa kupumua teh teh teh
 
 
 

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*