Tulonge

December 2012 Blog Posts (126)

Picha ya daladala ikiteketea kwa moto Iringa

Hii ni taarifa iliyoripotiwa na iringa-yetu.blogspot.com kwamba zaidi ya abiria 20 wanusurika kufa katika ajali ya gari aina ya daladala inayosafirisha abiria kati ya Mkwawa na Kihesa Kilolo baada ya daladala hiyo kuungua moto na kuteketea kabisa chanzo kikiwa ni hitilafu ya injini.Ilitokea saa saba mchana december 30 katika maeneo ya Mshindo karibu kabisa na…

Continue

Added by Tulonge on December 31, 2012 at 13:10 — No Comments

Askari JWTZ aliyepiga picha na Mbunge Godbless Lema atokomea

Mtu aliyejitambulisha kuwa askari wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ),kambi ya Monduli,Arusha akiwa na wabunge wa Chadema,Godbless Lema (Arusha Mjini) na Joshua Nassari (Arumeru Mashariki) baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na wabunge hao katika Mji mdogo Mererani,Simanjiro mkoani Manyara.JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limesema…

Continue

Added by Tulonge on December 31, 2012 at 10:30 — 3 Comments

Msanii Steve Nyerere anusurika kifo kwa ajali ya gari Wami

Msanii nyota wa filamu na mchekeshaji maarufu nchini, Steve Mangele maarufu kama Steve Nyerere, amenusurika kifo katika ajali ya gari iliyotokea juzi maeneo ya Mto Wami. Msanii huyo pamoja na wenzake watatu akiwamo msanii mwingine wa filamu, Chikki Mchoma, walikuwa wakisafiri kwa gari dogo aina ya

 

Toyota Verossa kutokea Arusha kuhudhuria sherehe ya mwenzao…

Continue

Added by Tulonge on December 30, 2012 at 0:20 — 1 Comment

Watu 8 wafariki Kenya

Familia zilizoathiriwa kwa mujibu wa Gazeti la Standard Nchini Kenya wakipekuwa mali yao baada ya maporomoko hayo ya Ardhi

Watu wanane wamekufa baada ya nyumba kadha kufukiwa na maporomoko ya ardhi katika eneo la bonde la Kerio, magharibi mwa Kenya, jana usiku.

 

Maporomoko ya ardhi yamesababishwa na mvua kubwa…

Continue

Added by Tulonge on December 29, 2012 at 23:22 — No Comments

Rais Kikwete ampa pole Padre Mkenda wakati akiuguza majeraha ya kupigwa risasi.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae mjini Zanzibar anayeuguza majeraha katika taasisi ya mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) jijijini Dar es salaam leo Jumamosi Dsemba 29, 2012 kufuatia kupigwa risasi sehemu za mdomoni na watu wasiojulikana mapema wiki hii wakati akisubiri kufunguliwa geti la nyumbani…

Continue

Added by Tulonge on December 29, 2012 at 21:38 — No Comments

Kesi ya ‘Lulu’ yasajiliwa rasmi Mahakama Kuu

Kesi ya mauaji ya kutokukusudia inayomkabili msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael `Lulu’, imepokelewa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na kusajiliwa kwa namba 125 ya mwaka 2012.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana mahakamani hapo, kesi hiyo imepokelewa kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na inasubiri kupangiwa Jaji na tarehe ya kuanza kusikilizwa.

Awali Lulu alikuwa akikabiliwa na mashitaka ya kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba, kwa…

Continue

Added by Tulonge on December 29, 2012 at 21:35 — No Comments

Ilisemekana ingekua hivi Dec 21, 2012, na hapo ungekua mwisho wa Dunia. Iliishia wapi hii wadau?

Wadau nadhani mnakumbuka kulizuka utabiri kuwa tarehe 21 Desemba 2012 ndiyo ungekuwa mwisho wa Dunia. Ilisemekana kuwa Dunia ingegongwa na kusababisha kutobaki kwa kiumbe hai chochote kwenye sayari ya Dunia. Ni nini kilisababisha hali hiyo isitokee.

Added by Tulonge on December 29, 2012 at 2:47 — 10 Comments

Aliyeuawa na askari wawili Kasulu azikwa, askari hao kufikishwa mahabusu

Askari polisi wawili wa kituo cha polisi Herushingo tarafa ya makere wilaya Kasulu wanashikiliwa na polisi wakituhumiwa kusababisha kifo cha mkazi wa kijiji cha Herushingo Gasper Mussa baada ya kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake na kumuweka mahabusu.

Added by Tulonge on December 29, 2012 at 2:23 — 2 Comments

Kijana ajiua kwa kuchoshwa na matezo ya Ukimwi

Kijana mdogo wa miaka 18, mkazi Dar es Salaam, Abdallah Salum, amekutwa amejinyonga chumbani kwake akidai amechoshwa kusumbuliwa na ugonjwa wa Ukimwi.Kamanda wa mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Engelbert Kiondo, alisema jana kuwa Salum, mkazi wa Charambe wilaya ya Temeke alikutwa amejinyonga juzi kwa kutumia kamba ya katani aliyoitundika kwenye kenchi.

Alisema kijana huyo aliacha ujumbe uliosema; “ugonjwa huu wa Ukimwi umenisumbua sana.”Kamanda huyo alisema mwili wa…

Continue

Added by Tulonge on December 29, 2012 at 1:52 — 2 Comments

Kigoma: Polisi wawili wanashikiliwa kwa kumpiga hadi kumwua mwanakijiji

Jeshi la Polisi mkoani Kigoma linawashikilia askari wake wawili kwa tuhuma za kumpiga na kusababisha kifo cha mkazi wa kijiji cha Herushingo, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma, Gasper Mussa.

Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, Fraiser Kashai, aliwataja askari hao kwa waandishi wa habari mjini hapa kuwa ni mwenye namba NCC 8622 Koplo Peter na G.1236 Konstebo Sunday. Alisema wawili hao wanadaiwa kumpiga Mussa walipokuwa kwenye kilabu cha pombe usiku wa Sikukuu ya…

Continue

Added by Tulonge on December 28, 2012 at 7:06 — No Comments

Kuhusu sakata la kupigwa risasi: Padri Ambrose azungumzia hali yake, Zanzibar kuwasaka wahusika.

Serikali ya mapinduzi Zanzibar imesema inashirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vya serikali ya muungano kuwabaini waliohusika na tukio la kupigwa risasi na watu wasiojulikana paroko wa parokia kanisa katoliki la Mpendae Zanzibar padri Ambrose Mkenda.

Added by Tulonge on December 28, 2012 at 2:54 — No Comments

Jumba la aliyekua Rais wa Nigeria 'Olusegun Obasanjo' lanusurika kuteketea kwa moto

Obasanjo’s mansion

"caused by an electrical fault, torched a section of former president Olusegun Obasanjo’s office within his mansion in Abeokuta, Ogun state on Thursday evening.

The fire, which started a few minutes after 5pm has however been put out following efforts by men of the Nigeria Security and Civil…

Continue

Added by Tulonge on December 28, 2012 at 2:30 — 2 Comments

Hukumu kesi ya Lema yaibua mapya

MBUNGE wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema 

MWANAZUONI aliyebobea katika sheria, Profesa Issa Shivji na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Francis Stolla wamekosoa hukumu ya Mahakama ya Rufani, iliyomrejesha bungeni, Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti…

Continue

Added by Tulonge on December 28, 2012 at 1:11 — No Comments

Waumini KKKT waapa kumtetea mchungaji aliye timuliwa

Askofu Thomas Laizer

Waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati, wamekuja juu na kuahidi kuandamana kupinga hatua ya kanisa hilo kumvua cheo na kumfukuza Mchungaji Philemon Mollel aliyekuwa Kiongozi wa Usharika wa Ngateu katika Jimbo la Arusha Magharibi.Hatua ya waumini hao…

Continue

Added by Tulonge on December 28, 2012 at 1:02 — No Comments

Uchunguzi wabainisha kuwa Whitney Houston aliuawa

JUU: Whitney Houston enzi za uhai wake akitumbuiza. CHINI: Mwili wa Whitney ukiwa kwenye jeneza ukipakiwa kwenye gari maalumu. KULIA: Mchunguzi wa kujitegemea, Paul Huebl.

Paul Huebl anasema amewapatia FBI ushahidi unaoonesha mwimbaji Whitney Houston mwenye miaka 48 aliuawa kufuatia deni la dawa za kulevya mwezi Februari, mwaka…

Continue

Added by Tulonge on December 28, 2012 at 0:50 — 2 Comments

Paroko aliyepigwa risasi Zanzibar aletwa Dar es Salaam kwa matibabu

Paroko wa parokia kanisa katoliki la Mpendae Zanzibar padri Ambrose Mkenda ambaye alipigwa risasi na watu wasioujulikana amepelekwa jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi huku polisi ikiendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Added by Tulonge on December 27, 2012 at 0:18 — 1 Comment

CHADEMA yaijia juu JWTZ kuhusu mwanajeshi aliyepiga picha na Godbless Lema

Mbunge wa Ubungo na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika.

SIKU moja baada ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kutangaza kumsaka mtu aliyepiga picha na Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema akiwa amevalia sare za jeshi hilo, chama hicho kimeibuka na kulijia juu jeshi hilo.Hata hivyo,…

Continue

Added by Tulonge on December 27, 2012 at 0:13 — No Comments

Mwanafunzi afia gesti akitolewa mimba

MWANAFUNZI wa kidato cha tatu katika shule ya Sekondari ya Tongoni nje kidogo ya jiji la Tanga, (jina tunalihifadhi) amekutwa amekufa ndani ya nyumba ya kulala wageni alikopelekwa kutolewa mimba bila mafanikio.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe mwanafunzi huyo alikutwa amekufa juzi…

Continue

Added by Tulonge on December 27, 2012 at 0:05 — 8 Comments

Monthly Archives

2014

2013

2012

2011

2010

1999

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*