Tulonge

Ilisemekana ingekua hivi Dec 21, 2012, na hapo ungekua mwisho wa Dunia. Iliishia wapi hii wadau?

Wadau nadhani mnakumbuka kulizuka utabiri kuwa tarehe 21 Desemba 2012 ndiyo ungekuwa mwisho wa Dunia. Ilisemekana kuwa Dunia ingegongwa na kusababisha kutobaki kwa kiumbe hai chochote kwenye sayari ya Dunia. Ni nini kilisababisha hali hiyo isitokee.

Views: 904

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on January 5, 2013 at 21:42

Ha haa haa haa haaa..... Mie wala sikuamini sababu imeandikwa kwenye kitabu cha The Mayan Civilization, kwani Calendar yao waliyotengeneza miaka 3,000 iliyopita (kabla ya Yesu) ndio ilikuwa inakwisha 21 Dec. 2012, na kuanza na Calendar mpya. Baadhi ya watu walidanganya wenzao makusudi kwa manufaa yao kitu kilichofanya Mayan people waishio central & south America kusisitiza kuwa ni mwisho wa Calenda yaotu  na sio mwisho wa dunia.

Mbona hata NASA scientists waliandika kwenye website yao kuwa 21 Dec. 2012 haitokuwa mwisho wa dunia nashangaa kwa nini watu waling'ang'ania na kuamini.

Comment by Kassimu Mwabelo on January 2, 2013 at 20:28

Mambo yote yaliyopo duniani hayashindi kudra ya M/mungu!, wanasayansi na watabiri wapo na wataendelea kuwepo kwani vyote vilivyopo duniani vimewekwa na mungu, ajuaye siku ya mwisho ni M/mungu pekee! kikubwa ni kumcha mungu.

Comment by Georgia Mushashu on December 31, 2012 at 11:33
Asante sana Bwana Samson Andreas Mabilu nimependa maelezo yako. Ni kweli watabairi watabakia kutabiri hili na lile lakini Muumba wa Mbingu na Dunia ndo anayejua huo mwisho wa dunia utakuwa lini. Cha muhimu sana ni kukaa tayari kwani hakuna ajuaye siku wala saa so ni vema kujiweka tayari ikiwa yamebakia masaa machache unaweza shangaa kuona humalizi mwaka ukidhania kuwa ndo mwisho wa dunia kwa wote kumbe ni kwako ambaye unakuwa haupo tena. Kesheni mkiomba tubuni na kumrudia Mungu. Nawatakia wote maandalizi mema ya kufunga na kufungua Mwaka mpya wa 2013 tuombeane uzima mengine yote ni Majaliwa ya Mwenyezi Mungu.
Comment by Omar on December 29, 2012 at 14:30

Hahaha utabiri wa mwisho wa Dunia! Yesu alipoulizwa kuhusu siku ya mwisho kwani alisemaje? yeye alisema kwa habari ya siku ile na saa ile hakuna ajuaye siyo mwana wala malaika ! isipokuwa anajua bwana mungu tu! kwa maneno haya bwana yesu amekubali kuwa siku ya mwisho ipo ila hajui itakuwa lini? hata wanafunzi wake pia waliwahi kumuuliza maswali kama haya, bwana yesu ni nini dalili ya kuja kwako na lini mwisho wa dunia? aliwapa jibu hili tu"Angalieni mtu asiwadanganye maana katika siku za mwisho wengi watakuja kwa jina langu wakisema.....................................

Comment by Tulonge on December 29, 2012 at 12:03

Hahahhaaaaa Kunambi chizi kweli ww, mimi huwa natubu na kuacha dhambi kila siku.Kimbembe kipo kwako

Comment by MGAO SIAMINI,P on December 29, 2012 at 11:26

"The end of science is the beginning of mystery" msiogope

Comment by KUNAMBI Jr on December 29, 2012 at 10:54

Kilichosababisha ni Mungu coz alikua anasubiri Dis atubie midhambi yake yote kwa last chance,sasa sijui ushafanya hivyo ndugu

Comment by Tulonge on December 29, 2012 at 8:38

Umesomeka mkuu Samson, asante kwa kunikumbusha na jina la hilo dude. Nilisahau kuwa linaitwa NIBIRU teh teh teh teh

Comment by Samson on December 29, 2012 at 7:58

Utabiri upo, wanasayansi wapo, ila isisahaulike kwamba mwanasayansi, sayansi yenyewe, Dunia na vitu vingine vyote ni vya MUNGU. Yeye ana amri na mamlaka juu ya vitu vyote, kwa sababu laiti kama ingekuwa sayansi na ama utabiri ndiyo kila kitu bac Dunia ingeshateketezwa kama walivyotabiri wanasayansi lakini kwa kuwa yupo mwenye nguvu zaidi bac anajua NIBIRU kilikuwa kitu gani na kilikuwa kinaelekea wapi na kwanini. Huo ni mtazamo wangu.

 

Comment by Tulonge on December 29, 2012 at 2:48

Au kuna mtu alikwepesha Dunia isigongwe na hilo dude?

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*