Tulonge

Arusha: Mama awachinja wanawe kwa kuzuiwa kuwabatiza

MAMA mmoja mkazi wa Kijiji cha Rhotia wilayani Karatu, anashikiliwa na polisi akidaiwa kuwaua watoto wake wawili kwa kuwachinja.

Hilo ni tukio la pili kubwa la mzazi kuua wanawe baada ya lile la Mkazi wa Kijiji cha Gekrumu wilayani humo, Evance Damiani (43), kuwaua watoto wake wanne, Theophil (11), Ritha (9) na pacha Jigimu na Theodore (6) kisha na yeye kujiua kwa kile kilichodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alithibitisha jana kutokea kwa mauaji ya watoto hao na kueleza kuwa uchunguzi bado unaendelea, “Ni kweli tumepata taarifa hizo kutoka Karatu na uchunguzi wa tukio hilo umeanza ili kujua chanzo cha mama huyo kufanya mauaji hayo,” alisema Kamanda Sabas.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Rhotia, Andrea Mallu alisema mama huyo aliwaua watoto wake usiku wa kuamkia jana.

Mashuhuda waliwataja watoto hao waliochinjwa kuwa ni Mariana Juma (9) mwanafunzi wa darasa la tatu na Patrice Juma (6) anayesoma chekechea, “Imesemekana kuwa aliwachinja kwa sababu watoto wake walizuiwa kubatizwa na Jumuiya ya Kikatoliki ya Yohanne Mseyi,” alisema mmoja wa mashuhuda hao ambaye hakutaka kutaja jina lake liandikwe gazetini.

Habari zimeeleza kuwa mama huyo sasa anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Karatu baada ya kukamatwa na wanakijiji wenzake.

Mallu alidai kuwa mwanamke huyo aliwachinja watoto wake hao wakati bibi yao akiwa katika msiba wa nyumba ya jirani na muda mfupi baada ya kufanya tukio hilo alitoroka.

“Wananchi walishirikiana na kuanza kumsaka na saa 5:00 asubuhi jana walimkuta katika nyumba moja iliyokuwa ikijengwa akiwa amejificha. Alipohojiwa, hakutaka kusema chochote badala yake alitoa karatasi yenye ujumbe kuwa amefanya hivyo baada ya wanajumuiya kukataa kuwabatiza watoto wake.”

Hata hivyo, Mallu alisema kuwa Jumuiya hiyo ya Yohanne Mseyi imekana madai ya mama huyo ikieleza kuwa hakuwahi kuchukua hata fomu zilizokuwa zimetolewa kwa ajili ya ubatizo wa watoto.

Chanzo: berthamollel.blogspot.com

Views: 369

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Christer on January 3, 2013 at 10:47

Hizi ndo dalili za mwisho wa dunia, haya yote yameandikwa kwenye vitabu vitakatifu.

Comment by Omar on January 3, 2013 at 1:32

Shituka huko tunapokwenda kunatisha! itakuwa ndoto watu kutenda mema kabisa.

Comment by Tulonge on January 3, 2013 at 0:44

Kumbe kuna baadhi ya wanawake wana roho ngumu hivi? Yani unachinja watoto wako? Huyu awajibishwe aisee. Hata kama kweli wangemzuia kubatiza watoto wake, hakustaili kuwachinja.

Au hana akili timamu?

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*