Tulonge

Ndege 3 za Serikali zaenda kwa Milioni 1.5/-

Waziri wa Kilimo na Chakula na Ushirika, Christopher Chiza ameelezwa kuwa ndege ndogo tatu za Taasisi ya Serikali kupitia Wizara ya Kilimo zilizokuwa zikitumika kunyunyizia dawa ya wadudu zimeuzwa kwa jumla ya shilingi milioni moja u nusu kutokana na ukosefu wa vipuri.

Waziri alipokea taarifa hiyo iliyowasitusha watu wengi wakiwemo viongozi alioongozana nao alipokwenda kukagua shughuli za taasisi hiyo katika karakana iliyopo Arusha.

Afisa Mfawidhi wa taasisi hiyo Gideon Magusi alisema ndege hizo aina ya 5H-MRP Piper Super Cable na Cessna 145 zilianguka kwa nyakati tofauti.

Alisema ndege moja ilianguka Sitalike, Mpanda mwaka 1986 na nyingine ilianguka katika kiwanja cha ndege Mwanza 1992 ikiwa katika safari ya kikazi ya kudhibiti ndege aina ya Kweleakwelea, na ndege nyingine ilianguka Igunga, Tabora wakati wa operesheni ya kudhibiti nzige.

Baada ya kufanya utaratibu wa kulipwa fidia na shirika la bima la Taifa, NIC. Hata hivyo NIC kupitia kwa Katibu mkuu wa Wizara ya Kilimo, ililipa fidia ya shilingi laki tano kwa kila ndege na kuchukua mabaki, hivyo Serikali ilipata shilingi milioni moja na laki tano kwa ndege zote tatu.

Kutokana na taarifa hiyo, Chiza aliyeonesha kuchukizwa, aliagiza kuwa ndege zote zinazomilikiwa na taasisi hiyo zikiwepo mpya na zitakazonunuliwa, kukatiwa bima kubwa na inayokidhi.

Alisema ni jambo la kushangaza kuwa kampuni zilizokuwa zikikodi ndege hizo zilipwa fedha nyingi kupitia NIC huku Serikali ikiambulia shilingi laki tano.

Via: wavuti.com

Views: 600

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Dixon Kaishozi on January 17, 2013 at 11:46

Haka kamchezo bwana!!! we acha tu.. Hao walionunua wao wanatoa wapi vipuri ? Kuna mkuu mmoja wa mkoa wa mwanza alijiuzia gari aina ya  Toyota Land-cruiser VX kwa tsh. 2mil.. akidai ni mbovu na serikali kumunulia nyingine ya kazi.. hivi sasa ipo nyumbani kwake kaipaki na anatumia kwa matumiz yake binafsi... Hii ndiyo Tz zaidi ya uijuavyo!!!! 

Comment by Christer on January 7, 2013 at 10:00

Mmmmh

Comment by jemadari mimi on January 5, 2013 at 10:25

Hatuwezi kuendelea kwa kuwa na watendaji wabovu wanaojali matumbo yao na familia zao,ifike mahali tuwe na sheria za kuwabana hawa viongozi na ikiwezekana ,tuambiwe ni nani haliyefanya madudu hayo na hatua zipi zilichukuliwa juu yake.

Comment by Mama Malaika on January 4, 2013 at 23:13

Ama kweli bongo tambalale. Just 1.5mil tsh (£600) for three small planes??? Hapo lazima mtu kachakachua hata kama ndio walikosa vipuli wasingeuza bei chee hivyo, hasa kwa ndege za Cessna zina sifa nzuri kuishi miaka mingi na inatengezeka kiurahisi. Huo ni mradi wa mtu, wamepeana na siajabu wanatafuta au mtu ana vipuli na muda si mrefu viji ndege hivi vitakarabatiwa na kutumiwa kwa biashara kukodisha watu wanaotaka kujiendesha wenyewe au watalii (private).

Nchi imefirisika matumizi mabaya ya pesa na mali za sirikali sababu ya ufisadi.

Comment by Longumok L. Mollel on January 4, 2013 at 15:53

    serikali inafanya wanahujumu mali nyingi za watanzania , kwa kuwa viongozi hawana uchungu na  mali hizo.viongozi  wajuu hawalipi kodi, hivyo hata wakipeana bure wao hawana hasara. Kujua kuwa ni uzembe kwa nini hawakukatia ndege hizo bima kubwa kabla?

Comment by Masha waryoba on January 4, 2013 at 13:31
Hiyo ni mali ya umma!Fedha iliyotumika kununua hizo ndege ni ya walipakodi,wavuja jasho nchi hii!!viongozi yawapasa kuwa makini,ilitakiwa hizo ndege ziwe zimekatiwa bima Kubwa inayoendana na thamani ya ndege hizo.Ujanja ujanja mpaka lini Tz!!?tubadilike

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*