Tulonge

Mwanafunzi wa sekondari ajinyonga kwa mtandio

MWANAFUNZI wa kidato cha tatu wa Shule ya Sekondari Mbezi Inn, Daines Richard (15) amekutwa chumbani kwake akiwa amejinyonga kwa mtandio aliokuwa ameutundika darini. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela amesema tukio hilo lilitokea Januari 18 mwaka huu Mbezi Kimara.

Alisema sababu ya kujinyonga inasadikiwa kuwa ni baada ya baba yake kumwambia aoshe vyombo na yeye alikataa hali iliyosababisha mzozo kati yake na baba yake.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Tumbi Kibaha na upelelezi unaendelea.

Wakati huo huo, moto umezuka ghafla katika maeneo ya Kigogo Mkwajuni kwenye nyumba ya Protas Ernest (33) na kuteketeza chumba kimoja katika nyumba ya vyumba vinne pamoja na vitu vyote vilivyokuwamo ndani.

Kenyela alisema tukio hilo lilitokea Januari 18 mwaka huu na inasadikiwa kuwa chanzo cha moto huo ni mshumaa uliowashwa na mwenye nyumba.

Moto huo ulizimwa na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji cha Jiji kwa kushirikiana na wananchi wa eneo hilo.

Alisema thamani ya mali zilizoteketea kwa moto bado haijafahamika na hakuna madhara yoyote kwa binadamu.

Chanzo: mtanzania.co.tz

Views: 445

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on February 3, 2013 at 0:56

Watoto siku hizi hasa baadhi ya maeneo ya Dar wamekuwa mabishoo sana. Miaka 15 abishana na baba yake kisa kukosha vyombo? Haya matumbo tunazaa mengi hadi mijusi, mtoto umzae kwa uchungu, umelee na kumuhangaikia eti kafikisha miaka 15 anakusimamia kujibisha nawe kama mtoto mwenzie. Hasara tupu sijui tunakwenda wapi?

Comment by Christer on January 22, 2013 at 9:14

Kwanza mtoto wa miaka 15, unapata wapi nguvu ya kubishana na baba yako jamani? alafu mtoto wakike usipoosha vyombo nani sasa ataosha? babako ndo aoshe kweli? hata km ungekuwa wa kiume, unatakiwa umtii baba yako. mmmh tunaozaa tuzae ila tujifunge mikanda ktk malezi maana watoto wa sasa sio wa enzi zetu jamani. aya umeamua kutangulia nenda sie tutakukuta maana hata sikuhurumii, nawapa pole wazazi wako kwa kuwaachia maumivu. Pole sana Ernest kwa kuunguliwa nyumba

Comment by william massawe on January 21, 2013 at 13:00

hako katoto dizaini kalishaanza kugongwa na midingi yenye umri wa babake!!.sasa kuona mdingi anamzengua,akajaribu kumechishaaa,akaskotiii akaona,mbona mshua ananizungua wakati ana umri kama shuga dadi wangu!!!

Comment by Tulonge on January 20, 2013 at 19:34

Hawa watoto wa siku hizi ni balaa.Mimi nikiwa na umri wa miaka 15 sikuwa hata najua ishu za kujinyonga.

Binafsi sikuwa na uwezo wa kumbishia Baba yangu, cjui  watoto wa siku hizi wapo wipi? au ni malezi mabovu?

Comment by Masha waryoba on January 20, 2013 at 16:00
Pole kwa Familia ya huyo kijana!ni mdogo sana,Taifa limepoteza nguvu kazi!lkn maadili kwa vijana yameshuka sana,kuna ulazimu wa kutoa elimu ya ushauri nasaha mashuleni na kwenye Jamiii,kwani kujiua siyo njia ya kusolve ttz.

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*