Tulonge

Sakata la Gesi Mtwara/Lindi: Tazama moja kati ya mabango ya wananchi

Giza linaendelea kutanda mingoni mwa Wananchi wa Mikoa ya Kusini hasa Lindi na Mtwara kuhusu mgogoro wa gesi kwenda Kinyerezi. Wengi, wakiwemo Wanasiasa wandani ya Mikoa hii na hata nje wamekuwa wakijiuliza nini hasa kiini cha mgogoro huu; Je! Ni ubinafsi wa Wananchi wa Mikoa hii kutaka kujilimbikizia rasilimali zao peke yao? Ni shinikizo la wanasiasa kujitafutia umaarufu? Maslahi ya nchi kama inavyodaiwa na viongozi wa Serikali? Au ni Ubinafsi wa wachache, hasa Raisi Kikwete kama inavyodhaniwa na wengi wa Wananchi?


Via: wavuti.com

Views: 1056

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on February 3, 2013 at 0:59

Duh! Nilikuwa sijaingia Tulonge siku nyingi hadi hii imenipita. Watanzania sasa wameanza kuamka toka usingizini

Comment by Christer on January 22, 2013 at 9:36

Mnyonge mnyongeni, chake mpeni

Comment by Dixon Kaishozi on January 21, 2013 at 15:21

Hapo kwenye hiyo picha kwa chini ya  "heading"  inayosema UJENZI WA BOMBA LA GESI Panasomeka hivi POAC yalaumu kufichwa mkataba!!!!! Acheni wa Mtwara wadai haki yao... ipo siku patakuja himbika!!!

Comment by Dixon Kaishozi on January 21, 2013 at 15:18

Kama mnakumbuka niliwaeleza kuwa Mikataba ya Rasirimali za nchi yetu imefichwa sana!!! Kama alivyosema ndugu yetu Masha waryoba "Kamati ya hesabu za Mashirika ya Umma(PAC)ni juzi tu imebaini Udanganyifu kwenye mkataba wa uchimbaji wa gas hiyo!!"  na hiyo ni gesi tu.. Huko kwingine kukoje ?

Comment by william massawe on January 21, 2013 at 12:46

mimi nilishawahi kufanya kazi GEITA GOLD MINE.....kwa takribani miaka minne!....kusema ukweli,ninawaunga mkono wanainchi wa MTWARA kwa asilimia 100..kwani,pale GEITA wanainchi wanaozunguka mgodi wako hoi kabisa!!wengine wanakufa kwa sumu ya  kuoshea maji{kijiji cha NYAKABALE},wengine wamezuiwa na mgodi kupata huduma muhimu kama matibabu pale mjini GEITA,hata shule zilizopo pale GEITA zinatia uchungu sana,kwani,hazina vifaa muhimu!!!!!!!!!!!!!wanainchi wapitao ndani ya mgodi wanakutana na chamoto kwani wengine wanaumwa na mbwa wakali wa mgodini!!!!!!!!....mahakama za mwanzo kama nyankumbu,wa2 wanakalia mabenchi hata rangi,computer pia hamna!!!!!!!!!!!!!,HAUWEZI KUAMINI WANAINCHI HAO WANATEGEMEA SANASANA MKAA,NA MAZAO MENGINE KAMA ILIVO KWA SEHEMU NYINGINE ZISIZO NA MADDINI!!!!....kwa asiyeyaona mambo haya kwa macho yake,HAKIKA HAWEZI KUELEWA HAWA WA2 WA MTWARA WANAPIGANIA NINI!!!.............mimi ninasema hivi,iwe wanaelekezwa na wanasiasa,iwe ni utasha wao,au vovote vile iwavo,WANA HAKI!!!!!!!!!!!!!!!!

Comment by MGAO SIAMINI,P on January 21, 2013 at 12:07

Tatizo serikali haina hoja ya nguvu kueleza uma wa tanzania sababu yakinifu kwa nini gas lazima iende Dar.wanatumia nguvu na kauli za kibabe hili litawashinda wameshindwa kusimamia rasilimali za taifa watanzania wamechoshwa na wizi wao.

Comment by Gratious Kimberly on January 20, 2013 at 21:41

Chadema wanapata vichwaa!......ielewe mitaa!....teh

Comment by Masha waryoba on January 20, 2013 at 20:56
Ukiona Moshi unafukuta,ujue Moto uko kwa ndani!!Tumechezea mikataba ya Madini,hatimae Gas!Dharau viburi,vimewajaa viongozi wetu!!Kamati ya hesabu za Mashirika ya Umma(PAC)ni juzi tu imebaini Udanganyifu kwenye mkataba wa uchimbaji wa gas hiyo!!mnyonge mnyongeni lkn haki yake mpeni!!hivyo.Wanainchi wa mtwara wapaswa kusikilizwa!ubabe,nguvu havisaidii,kwani Mwisho wa Siku,ni Hasara kwa Taifa,Coz watachoshwa na hali hiyo hatimaye mwishoni ni kulipua bomba la gas,ili wote wakose!!!hahaha!Viongozi wafikiri mara mbili,mbona insue ni ndogo sana kuisolve!!!!!
Comment by Tulonge on January 20, 2013 at 20:45

Hii ishu isipoangaliwa kwa umakini italeta balaa

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*