Tulonge

Uwezekano wa Lulu kotoka kwa dhamana kesho

Taarifa za uhakika nilizozipata kwa sasa ni kwamba kuna uwezekano mkubwa mwigizaji Lulu akatoka kwa dhamana kesho january 25 2013.

Uhakika wa Lulu kupata dhamana ulikua jana jumatano january 23 lakini ikawa imeshindikana kutokana na kuahirishwa kwa sababu jaji alipata dharura na pia kiwango cha pesa za dhamana kilikua hakijatimia.

Chanzo cha kuaminika kilichoongea na millardayo.com kimesema dhamana ya kumtoa Lulu ambae amekua chini ya ulinzi kuanzia April 2012 ni milioni 20 za kitanzania.

Lulu amekua akishikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mwigizaji Steven Kanumba, endelea kuipitia millardayo.com kwa stori zaidi.

Chanzo: millardayo.com

Views: 611

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Tulonge on January 24, 2013 at 19:16

Teh teh teh teh Majata Daffa umenichekesha.kwani una uhakika kuwa Lulu alimuua jamaa.Mbona umeandika kama vile Lulu hana haki ya kuwa huru ila ni fedha ndo zitapelekea yeye kuwa huru?

Comment by David Edson Mayanga on January 24, 2013 at 17:25

Kesho hawezi toka labda kama sheria ya nchi kaiweka yeye ila kwajuma tatu sawa ,twamuombea mungu tu awezetoka kwani mulendani noma pia Lulu ukitoka kwadhaman siujisaha unajua wengi wakiwandani ya jera kushinda huwa rahisi sana kwasababa usikukucha hujipanga wakitoka nje ya dhamana inakuwa wanajisahau kabisa hadikiperekea kushindwa hata kutoaushahidi wautete waowenyewe hadikurekea kuwa wakafungwa ,kwahiyo kutoka kwadhamana siokumaliza esi ila nikujipanga ukiwamtaani nakumuomba mungu kwani pia hata kanumba twampenda sana tuwenaye leo hii ila mungu kampenda zaidi

Comment by Kayay Faiz Junior on January 24, 2013 at 17:19

Dhamana ni haki ya mtuhumiwa endapo kama vigezo na taratibu za dhamana zimekamilika..." lakini je wana hakiki vipi hali ya kiusalama anapo kuwa uraiani...?

Comment by Mjata Daffa on January 24, 2013 at 17:06

Mimi nilijua ipo siku lulu atatoka, kwa sababu katika Nchi hii kuna watu wako juu ya sheria wanao uwezo wakuzipindisha wanavyo weza. kwa uzuri wa Lulu nilijuwa mapedegeee watavunja Bank kumnusuru Mtoto. hakuna kinachoshindikana mbele ya pesa. HONGERA LULU ila hiyo siku ikifika haki lazima itendeke. Hatuta msahau KANUMBA kwa sababu tulimpenda na lazima wajue nyuma yake tupo wengi

Comment by JOHN KIMARO on January 24, 2013 at 15:54

Mimi ninatafuta kujua hatima ya Lulu baada ya uwezekano wa kupata dhamana kuonekana. Hii sikukuu imeleta balaa kwa Lulu. Mawakili wake lazima wazungumze na mahakama kuona kama mashauri yaliyokuwa yasikilizwe kesho yanaweza kupewa kipaumbele siku inayofuata. 

Comment by Tulonge on January 24, 2013 at 15:41

ahahahaaaa mkuu John naona unawakatisha tamaa kabisa washabiki wa Lulu

Comment by JOHN KIMARO on January 24, 2013 at 15:38

Taarifa ni nzuri lakini kwa Lulu ni kitendawili!

Comment by Tulonge on January 24, 2013 at 15:35

Mkuu John hata mimi nililifikiria hilo la sikukuu ya kesho, ila niliona niwajuze wadau nyepesi nyepesi zilizopo kwenye mitandao mingine.

Comment by JOHN KIMARO on January 24, 2013 at 15:29

Bahati mbaya mahakama haikai kesho kwa vile ni sikukuu ya Maulid. Sijui huyu atasikilizwa tena lini! 

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*