Tulonge

Bodi ya Mikopo yawaburuza mahakamani wanafunzi ambao hawajarejesha mikopo

Wanafunzi 18 wa vyuo vikuu nchini wameburuzwa mahakamani baada ya kubainika kushindwa kerejesha mkopo uliowawezesha kupata elimu ya juu kutoka Bodi   ya Mikopo (HELSB).

Washitakiwa hao walioshitakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam wanadaiwa zaidi ya Sh. milioni 148.

Wanadaiwa fedha hizo ambazo walikopa kati ya mwaka 1994 na 2009 na kukubali kurejesha kwa muda ambao walikubaliana na masharti ya bodi hiyo.

Inadaiwa kwamba kwa mujibu wa kifungu cha 6 C na H  cha sheria ya Bodi ya Mikopo namba 9 ya mwaka 2004, inatamka kwamba bodi iliaminiwa kusimamia  utaratibu mzima wa kutoa na urejeshaji wa mikopo iliyotolewa na serikali tangu Julai 1994:  Kwa mujibu wa kifungu namba 19 cha sheria ya bodi na miongozo yake, inatamka kwamba kila aliyefaidika na mkopo baada ya kukamilisha elimu yake atarejesha mkopo wa Serikali kupitia Bodi. Wadaiwa walikumbushwa kurejesha madeni kupitia vyombo vya habari, lakini walikaa kimya, hivyo bodi inaomba waamuliwe kulipa.

Bodi ya Mikopo inaomba kila mdaiwa alipe fedha alizokopa na adhabu asilimia 10 ya mkopo, alipe fidia kama mahakama itakavyoona inafaa na pia walipe gharama za kesi.

Wadaiwa katika kesi hiyo wanatakiwa kulipa jumla ya Sh. 135,132,275 ambazo ni madeni waliyokopa kwa ajili ya kuwawezesha kupata elimu ya juu na Sh. 13,513,227 ni adhabu ya kuchelewesha malipo.

Walioburutwa mahakamani ni Adam Coresh, Ally Mwenda, Anna Lymo, Hasma Tullango, Catherine  Mhina, Clement Kihamia, Dorin Lyatuu, Farida Zuku, Felix Mosha, Flora Peter, Frank Daniel, Harieth Mazengo, Happynes Saria, Hollo Ngeme, Mwanahamisi Abood, Ndebemeye Philipo, Ndeni Anande na Turphina Matereke.

Chanzo: Nipashe

Views: 668

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Yassin M Mchondo on February 18, 2013 at 18:40

Kijana kama hujatafutwa ujue una bahati nimeanza kulipa mkop wangu last year december na nitaumaliza baada ya miezi 20 utakuwa umeisha ila je Akina Chenge,Mkapa na wengine wameshalipa

Comment by Tulonge on February 13, 2013 at 10:32

Hhahaahahhaahhaaa Mgao umenena

Comment by Tulonge on February 13, 2013 at 10:31

Teh teh teh Dixon mimi sijamuona mtu anayeitwa Dismas kakomenti hapa.

Comment by MGAO SIAMINI,P on February 13, 2013 at 10:23

Sema kwa vile tulijaza mkataba lakini nyuma zaidi je hawadaiwi? mikopo yenyewe tumepata kwa shida mpaka tuandamane tupigwe na polisi sahizi tena mahakamani jamani

Comment by Dixon Kaishozi on February 13, 2013 at 10:00

Tehe... mpaka sasa kuna watu watatu wa humu kijijini hawapo kwenye list ya kulipa na wamejitaja wenyewe... Severin, Dismas na Kunambi... Hebu nipeni number ya bodi niwatumie majina haya..

Comment by Tulonge on February 12, 2013 at 20:27

Yani mimi huwa nasikia sikia tu ishu za kulipa mkopo.....sijui nini na nini. Hata sielewi, na hela niliitafuna.

Comment by Dixon Kaishozi on February 12, 2013 at 19:08
Turudi nyuma lakini.. hivi toka 2004 Mpaka 2009 Nihao tu watu sijui 12tu ndo walio kopa?... HAPO KUNAKITU SI BURE. WHY HAO TU????
Comment by ANGELA JULIUS on February 12, 2013 at 17:42

dah comment zenu zimeniua mbavu kumbe severini nawewe upo haya ngoja usipoipa kile kitu changu naenda kukutilia utambi bodi ya mikopo

Comment by KUNAMBI Jr on February 12, 2013 at 17:33

Mweeeh me wananitafuta mpk leo hawajanipata,maana jina nlilokua natumia Chuo na ninalotumia Kazini tofauti mpk waje wanigundue naona watanifunga kabisa

Comment by Mama Malaika on February 12, 2013 at 17:31

Severin yako kali. Ha haa haa haa haaa...

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*