Tulonge

Mkono wa Mwanamke albino uliokatwa Sumbawanga wapatikana

Juzi, vyombo vya habari viliripoti kuhusu, “Mwanamke albino anyofolewa mkono”.Taarifa mpya zilizopatikana kama zinavyoonekana pichani juu, ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya (wa tatu kulia) akibubujikwa na machozi jana usiku hali akushuhudia Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa, Peter Ngusa (kulia) akiwa ameushikilia mkono ulionyofolewa hivi karibuni kutoka kwa mwanamke mwenye ulemavu wa ngozi (hayupo pichani) na kufukiwa porini kijijini Miangalua wilayani Sumbawanga.

Pichani juu ni Madaktari wa hospitali ya Mkoa Rukwa juzi, wakijaribu kumwekea damu bi Maria Chambanenje (39) aliyevamiwa na kukatwa mkono na watu wasiofahamika, huku wakichukua mkono wake.

Mama huyo ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino) alikatwa mkono na watu wasiofahamika baada ya mumewe kwenda kulala kwa mke mwingine. Usiku watu wasiojulikana kuingia katika nyumba hiyo na kumkata mkono na kuondoka nao.

Kwa mujibu ya wakazi wa eneo hilo, mauaji kwa imani za kishirikina yanarejea kwa kasi.

Via: wavuti.com

Views: 524

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by emanuel Lyanga L. on February 18, 2013 at 21:32

duh, huyu mama mlemavu hata hivyo haitoshi wanadamu wakaamua kumwongezea ulemavu pole dada hukuta uumbmwe hivyo mungu atalipa.

Comment by ANANGISYE KEFA on February 16, 2013 at 11:08

Dah! inatia uchungu kweli, pole sana dada yangu

Comment by MGAO SIAMINI,P on February 16, 2013 at 10:12

POLE BINTI,ILA MCHEZO  WA KUWAUA ALBINO UMEANZA MIAKA KIBAO KWENYE JAMII ZETU ZA KITANZANIA MAANA SISI TULIAMBIWAGA ALBINO HUWA HAWAFI WANAPOTEA SASA SERIKALI ISITIBU HILI TATIZO KWA MUDA MFUPI IANDALIWE PROGRAMU YA MAFUNZO HADI MASHULENI,KAMA ILIVYO TOHARA KWA WANAWAKE,UKIMWI NK LITAPUNGUA NA BAADAYE LITATOKOMEA.

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*