Tulonge

Picha 5 ya shule iliyofungiwa huko Mwanza

Wanafunzi wakiwa Darasani

Shule ya Sekondari ya Mount Zion ina jumla ya vyumba 7 vya madarasa ambavyo ilisajiliwa navyo kuhudumia wanafunzi 160 lakini sasa hivi wanafunzi wameongezeka na kufikia 515 ambapo madarasa mengine yana wanafunzi mpaka 119 na wengine wanakalia ndoo badala ya viti.

Bwenini

Ni ndani ya moja ya vyumba vya wasichana ambacho ndani yake kuna matandiko haya na masanduku 13 ikimaanisha ndiyo idadi ya wasichana wanaolala hapa.

Mkuu wa Wilaya ya Ilemela akizungumza huku machozi yakimlenga kutokana na alichokiona shuleni hapo,  aliagiza hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya Mkurugenzi wa shule hiyo ya Mount Zion Ilemela.

Chanzo: millardayo.com

Views: 1100

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Christer on February 25, 2013 at 12:26

Pia wazazi nao sijui vipofu? hivi unampelekaje mtoto kwny shule km hii na ukawa comfortable kbs kuwa mtoto wako yuko shule? au ndo unampeleka unaishia reception/ front office bila hata kujua mtoto analala wapi? etc Mi nalia na wazazi wa hawa watoto, hivi wako sawa kweli? watoto wanalazwa darasani tena chini?

Comment by ABRAHAM PONERA on February 23, 2013 at 13:21

Kufunga shule sio suluhisho la kuondoa tatizo, Ndipo unaweza kugundua udhaifu wa viongozi(watendaji waliopo madarakani). Hiyo shule imepitia hatua zote za usajili mpaka ikaanzishwa wakaguzi walikagua nini hapo? Watoto hao wataishia mitaani, Nashauri viongozi(Watendaji) wafanye jitihada za kuinusuru hali hiyo ili kuwasaidia watoto hao waweze kuendelea na masomo.

Comment by Omary on February 22, 2013 at 22:51

Haya ndio maisha yetu sasa wamefunga hiyo shule je? watoto watasoma wapi? bi mkubwa hapo mwenye madaraka utafanya nini? au ndio utaishia kufunga shule na kuondoka? hayo ndio maisha halisi ya watoto wa wapiga kura na wengi hapo wajitahidi kuuza majogoo yao wengine wanafikia hata kuuza shamba ili mwanae aende shule then inafungwa halafu watoto wanarudishwa home wakafanye nini zaid ya kupewa mimba? kama kweli wanaakili wanatakiwa kufanya kitu hapo ili watoto wasirudi nyumbani yaani me nitafanya maandamano tena peku sivai hata kata mbuga kama mjomba mpoto

yaani me huwa napenda sana kumsikiliza mpoto huwa anawagonga sana na maneno yao ila hawakomi hawa viongozi sijui hawamsikii?! au wanapuuzia inatia uchungu kweli.

Mr tulonge tufanye mpango wa kufunguwa kashule ketu wenyewe najuwa wewe umeshawahi kuwa mwalimu me nitatunza madhingira ya shule watoto wanaotosha wakijaa hatuongezi hata kwa bakora ili tuwaonyeshe mfano hawa.

Comment by Mama Malaika on February 22, 2013 at 22:15

Nikiangalia hiyo picha juu kabisa sura hizo za watoto zinanitia uchungu sana, sura zina kiu ya elimu. Sirikali na education system vimewa let down hawa watoto. Sielewi kwanini sirikali ilitoa kibali wakati hakuna vitanda vya kulala, halafu hako kachumba kaduchu kenye magodo matatu utasema ni storage room vile.

Hilo bweni kubwa utasema kambi ya wakimbizi jamani, sasa hivyo vyoo watoto walivyojengewa sijui vina hali gani???

Comment by HAMIDU URASSA on February 22, 2013 at 15:23

hivi huko kuna wabunge kweli? na kama wapo inakuwaje wanataka lipwa mishahara mikubwa wakati watoto wao wanapata tabu ya madawati na mabweni? shule imekuwa kama wanasom wakimbizi kumbe ni watanzania wenzetu!!! jamani serekali tazame swala hili kw macho  mawili""""

Comment by Tulonge on February 22, 2013 at 15:10

Ni private hii

Comment by Mama Malaika on February 22, 2013 at 10:33

Just shaking my head! Je ni private school au ya kata? Wanangu macho yamewatoka hawaamini kama ni shule....

Comment by Tulonge on February 22, 2013 at 3:22

Kwa mtindo huu Division 0 lazima zitafikia 90%

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*