Tulonge

Sababu hizi za Msanii R.O.M.A zaweza isaidia SANA Tume ya uchunguzi wa matokeo mabaya ya kidato cha IV 2012

R.O.MA

Ukizungumzia wasanii muziki wa kizazi kipya wenye upeo mkubwa wa kufikiria hapa Tanzania huwezi muacha ROMA. Baada ya matokeo ya kidato cha nne 2012 kuwa mabaya, alimua kuandika sababu zilizopelekea matokeo hayo kuwa hivyo. Tume ya uchunguzi iliyoundwa na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda inaweza kupitia sababu hizi za ROMA ili ziwasaidie katika uchunguzi wao.

ROMA aliandika yafuatayo:-

KWANZA TUANGALIE NI KUNDI GANI LIMEONGOZA KUFELI MTIHANI HUU WA KIDATO CHA NNE, MAJORITY NI SHULE ZA KATA.

- Ongezeko la shule hizi za kata limekuwa kwa kasi sana, lakini shule hizi hazikidhi matakwa ya mwanafunzi kufaulu, hii ni kutokana na ukosefu/upungufu wa walimu/ miundo mbinu ya kufundishia!  

-Walimu wengi wanashindwa kukabiliana na changamoto zilizopo ktk shule hizi hasahasa huduma mbalimbali kukosekana kwa maana nyingi huwa zipo vijijivi sana!!
na tunafahamu kuwa vijijini ndiyo tupo wengi kuliko mjini! Hivo walimu wengi hushindwa kuwepo kwenye maeneo yao au vituo vya kazi walivyopangiwa, na hii hupelekea ukosefu wa walimu!

VIFAA VYA KUFUNDISHIA
Hapa tumekuwa tukilaumu sana MAABABARA! Tumemsikia waziri jana akisema MAABARA ni tatizo kubwa la kufeli! Sio kweli kwamba ni maabara pekee, kwa maana mbona MATHEMATICS, CIVICS, ENGLISH NA KISWAHILI, GEOGRAPHY etc. havihitaji maabara na wanafunzi wanafeli bado! Tukisema vifaa tujumuishe kwa nguvu moja vile vyote vitumikavyo kufundishia, bado hadi leo kuna tatizo la wanafunzi 7 kutumia kitabu kimoja! Mambo ya head master kufuata chaki mjini sikuyatunga tu kichwani!! nimeyashuhudia sana!

MGOGORO KATI YA WALIMU NA SERIKALI
Kumekuwa na kutoelewana kwa madai ya walimu dhidi ya serikali kwa kipindi kirefu, baada ya serikali kushindwa kutekeleza madai haya imepelekea kushuka kwa ari ya kufundisha kwa walimu! Lakini pia nahisi kama utungaji wa mitihani kwa walimu hawa ulikuwa ni kwa njia ya MKOMOENI(MTIHANI MGUMU) ili serikali ione pengo lake, 
hali iliyopelekea kuwakomoa na wanafunzi pia!

MALIPO DUNI KWA WALIMU
Hii hupelekea mwalimu kujihusisha na shughuli mbali mbali za kumuingizia kipato(ujasiriamali)! Sasa kama mwalimu kafungua kibanda chake cha kufuga kuku na kikawa kinamuingizia kipato basi bila shaka ata concentrate na kibanda hicho ilihali akijua mshahara wake wa ualimu uko palepale! Itapunguza kasi ya yeye kufundisha!

MAANDALIZI YA MWANAFUNZI(MSINGI)
Wengi hawaandaliwi kufaulu tokea msingi wao, mwanafunzi analazimishwa kungia sekondari wakati hajafaulu darasa la saba! Hii inapelekea kushindwa kumudu vitu vingi akiwa sekondari maana hana msingi imara! Namuuliza mwanafunzi wa form two mbili toa tatu(2-3?) ni ngapi? ananitolea macho kisha ananijibu haiwezekani? wakati hiyo ni topic ya darasa la 3/4 au 5! Inabidi nichukue muda wa ziada kumfundisha mambo ya darasa la 5,6,7 ndiyo twende sasa form 1!
Huo ni mwaka wa form 3 sasa so anakuwa hamalizi syllabus!!!

WALIPOFUTA MITIHANI YA KIDATO CHA PILI
Hii iliwafanya wasichujwe na kupata ile cream itakayo weza kupata alama za juu kwa vidato vya mbele ya form two kama ilivyo zamani! Mitihani kama hii humpima mwanafunzi akiwa hatua za awali ili kuweza kumuanda na hatua za mbeleni(form 4).

USHINDANI HAKUNA
- Siku hizi hakuna ushindani wa kielimu kama zamani, wanafunzi wanashindana mambo mengine tu ya kijamii na sio masomo kama zamani!
- Gobalization inasaidia sana kama wataitumia vema na ipasavyo ila hiyo hiyo inaweza ikawaharibu pia, hii hupelekea kushindana mambo mengine na kusahau ushindani wa kimasomo!

SYLLABUS
Walimu wanatumia silabasi kufundishia lakini mitihani intoka nje ya silabasi wanayopewa wanafunzi. (HAPA NAONA WENGI WANAWALAUMU TU WANAFUNZI LAKINI SIONI KAMA WALIANGALIA MITIHANI YAO!). Mwanafunzi inamuwia vigumu maana hana tuition anategemea mwalimu, na mwalimu anategemea syllubus, na syllubus haipo kwenye mitihani! Nasoma hiki kinatoka kile nitafaulu vipi?

FAMILIA
Familia pia zichangie kuwafundisha watoto misingi bora ya elimu,tatizo lije mzazi / mlezi naye hana elimu hiyo ni changamoto nyingine!

WALIMU
Walimu hawaandaliwi kuwa walimu bora haswa! Nadhani kwa maana kwa sasa lile ongezeko la walimu siyo kwa ajili ya wito na ndoto zao la hasha! Sio wote wapo hivo! Hii hupelekea wengi kukosa ile taaluma na moyo na wito wa kuweza kudeliver ile knowledge aliyonayo kwa mwanafunzi! Kufundisha ni kipaji unaweza ukawa na akili sana lakini usiwe na uwezo wa kumfanya mwenzio aelewe somo!

NI NUSU YA WALIOFANYA MTIHANI WAMEFELI. TAKRIBANI WANAFUNNZI LAKI 3 NADHANI! TUTAWAPELEKA WAPI NA AJIRA HAKUNA? WANGAPI WATAWEZA ENDELEA NA SHULE / VYUO / AJIRA?

WAZO LANGU:- TUTAZAME MFUMO MZIMA WA ELIMU NA SERA NZIMA YA ELIMU IBADILIKE KULINGANA NA TEKNOLOJIA NA NYAKATI ZA SASA HIVI NA KUYASAWAZISHA MAPENGO HAYO HAPO JUU YOTE!

DUNIA INABADILIKA INABIDI TUBADILIKE NA SISI KATIKA VINGI!

WANAOFAULU WAMEKUBALI KUBADILIKA WENGI WAO!

POLENI SANA WALIOFELI NA HONGERA KWA WALIOFAULU!

Views: 714

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by MGAO SIAMINI,P on February 28, 2013 at 12:04

mwalimu anasahihisha mitihani ambayo ndo maisha ya wanafunzi wanamlipa kama kibarua yaani per script kwa nini asilipwe kwa mujibu wa sheria ya ajira nights kwa siku zote atakazokuwepo eneo la kusahihishia mitihani kama zinavyolipwa kada nyingine zote nchini.kama wataendelea kuleta dharau kwa walimu lazima taifa litakuwa la majuha maana itafika siku hata faulu mtu.maana wazazi wanaleta dharau,serikali na wananchi wanadharau kada ya ualimu.sasa hivi walimu tusiandamane wala kupiga kelele wala lawama lugha hii tunayotumia inaeleweka wacha wamalize utafiti na tume yao mwakani tena 80% sifuri.

Comment by emanuel Lyanga L. on February 25, 2013 at 19:35

KWA KUONGEZEA HAPA KUNA PANDE TATU ZINATAKIWA KUSHUGHULIKIWA SERIKALI, WAZAZI NA WALIMU KAMA KILA PANDE IKITIMIZA WAJUBU WAKE MATOKEO YATAKUWA MAZURI

Comment by Mama Malaika on February 25, 2013 at 12:31

Christer... ni kweli bora tuliosoma zamani, elimu sasa Tanzania imeshuka sana

Comment by Mama Malaika on February 25, 2013 at 12:24

Hizi sababu zote zilizotolewa na kijana huyu juu, viongozi wanazijua sana ila kwa kuwa walisha wageuza watanzania mazumbukuku kwa kuwa ni wapole. Wazazi/walezi wameuza mashamba yao na assets zao kulipia watoto school fees halafu leo wizara elimu/sirikali inaleta upumbafu.

DISMAS... hao ni waongo, ina maana watoto wa mwaka huu tu peke yake hawakushiba? Mie nilipokuwa nasoma tulikuwa hatushibi (shule za sirikali boarding) na bado tulikuwa tunafaulu, na tulifanya subjects nyingi ambazo zimefutwa wanafunzi miaka ya sasa hawasomi

Comment by Christer on February 25, 2013 at 12:10

Teehee WALIMU WA BODA FASTER, Mi hata sielewi watoto wetu watafundishwa na nani! walimu hawa wa serikali hii isiyowasikiliza? bora sie tuliosoma zamani aisee.

Comment by Dixon Kaishozi on February 25, 2013 at 10:34

Nimekumbuka kitu !! Katika pointi aliyoitoa ROMA kuhusu shule za KATA! Tangu awali tumekuwa na upungufu wa waalimu. Serikali ikaongeza hizi shule za kata.. zimekuwa nyingi na kuongeza tatito la waalimu kuwa kubwa zaidi.. ILICHOKIFANYA SERIKALI ikatengeneza WAALIMU WA FASTER!! WAKAITWA WAALIMU WA BODA FASTER!!! walienda kufundishwa ualimu kwa wiki 3 wakaingia darasani kufundisha !!!! Hapo tunategemea nini ?

Comment by Dixon Kaishozi on February 25, 2013 at 10:29

Huwa na shangaa saana!! Hapa kijana ROMA Kaeleza sababu za msingi kabisa ambazo zipo wazi, Inamaana ROMA kaunda tume ndo akapata hizo sababu ? Sisi tumebaki na kuunda TUME!!! Serikali ilichokipinga BUNGENI kwa hoja ya Mh. Mbatia kuhusu sekta ya ELIMU na MFUMO wote wa elimu kuwa MBOVU sasa BOMU lake limelipuka, aliyasema kwa manufaa ya TAIFA letu na si swala la kitaifa na u-vyama!!! WAKAMPINGA KWA NGUVU ZOTE NA HOJA YAKE KUPIGWA CHINI...

Sasa wakisha unda TUME, najua kupata ripoti ni ndoto.. enewei ... Baada ya tume kinachofuata nini ? hao watoto waliofeli inakuwaje ?

Comment by Tulonge on February 25, 2013 at 2:05

Hata wakipita watazichunia tu hizi points za Roma japo ni za msingi. Wenyewe watataka ripoti ya tume yao. Nilisikia walitoa sababu kuwa Wanafunzi hawashibi. Sijui ni kweli huwa hawashibi?

Comment by Omary on February 25, 2013 at 0:36

Hivi hakuna hata mkuu 1 wa nchi anaepitia hapa kijijini akajionea maneno ya ROMA yaliojaa ukweli ndani yake na kama hawayaoni wala kusikiliza nyimbo zake sijui inawezekana wakapelekewa mzigo kama ulivyo? tena umfikie mzee Pinda ili pesa zote za tume apewe ROMA kazi kashaimaliza kija umefanya kazi kubwa sana ambayo wanataka kufanya watu zaidi ya 5 kuchunguza swala ambalo umelifanyia kazi mwenyewe ROMA pongezi kwako kijana wataelewa tuh usikate tamaa kuwaambia ukweli.

Comment by Tulonge on February 24, 2013 at 22:12

Hapa ndo utaona umuhimu wa Elimu kwa msanii wa Muziki. Naishauri Tume iliyoundwa na Mh. Pinda ipitie sababu hizi za ROMA, lazima itagundua mengi ya kurekebisha

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*