Tulonge

Ripoti: Madai ya wanafunzi IFM siyo ya kweli

Dar es Salaam. Kamati iliyoundwa kuchunguza vitendo vya udhalilishaji na kuporwa vitu vyao  wanavyofanyiwa wanafunzi  wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), wanaoishi  katika hosteli zilizopo Kigamboni Manispaa ya Temeke imebaini hakuna wanafunzi waliofanyiwa vitendo hivyo.

Kamati hiyo iliyoundwa na Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Polisi jijini Dar es Salaam, Suleiman Kova baada ya kuwahutubia wanafunzi hao katika Viwanja vya Machava, ilijumuisha wanafunzi wanne wa IFM na wakuu wa upelelezi kutoka kanda hiyo .

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Englebert Kiondo, alisema kamati hiyo ilichunguza kwa kina madai hayo ya wanafunzi, lakini hakuna na hata moja walilobaini kuwa na ukweli .Alisema suala la ulawiti walilodai wanafunzi, walijaribu kufuatilia kwa ukaribu  kutumia dawati la jinsia  ikiwamo kuwauliza wanafunzi hao ni nani alifanyiwa kitendo hicho, lakini hamna hata mmoja aliyejitokeza kusema amefanyiwa.

“Tuliwauliza wanafunzi ni nani amefanyiwa kitendo kama hiki ili tujue cha kufanya, lakini hakuna aliyejitokeza kukiri kuwa alilawitiwa tofauti na walivyodai hivyo wakati wa maandamano ,” alisema Kamanda Kiondo.

Chanzo: mwananchi.co.tz

Views: 638

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Dixon Kaishozi on March 26, 2013 at 8:50

Dah!! Pole Sana kaka!!! Hawa watu niwazushi tu. Wanafuatilia mambo yao/wakubwa tu!

Comment by Omary on March 26, 2013 at 0:50

Bora kwa wadada kidogo wanaweza kujitowa muhanga ila kwa mwanaume kujitokeza inataka moyo sana maana hata ikijitokea tayari imeshakuwa na hutapata kitu hata huyo aliefanya hivyo hatapatikana na wewe utakuwa ushajianika bora kupiga kimya kuna siku niliibiwa pikpk jamaa akawa anakimbia nayo na mimi nipo kwa mguu bahati difenda ya police hii nikaona MUNGU kaniona nikawaambia tumkimbizeyule jamaa anakimbia na pikpk yangu walichonijibu waniambia kuna watu wanawafuatilia mie niende tu kituoni nikariport wao watafuatilia wakishamaliza mimi nikafanya jitihada za kimwenye ila nilikuwa nimeshachelewa alishapote wakati narudi naikuta difenda ile imepaki sehem wanaenda kuvizia wauza gongo sijaenda kuriport wala nini nilipiga kimya maana haikuwa na maana kuriport tena kama walishindwa kunisaidia kwenye tukio toka hapo imani na police ilinitoka kabisaaa hilo nalisema toka moyoni hawakuwa na msaada kwangu.

Comment by Longumok L. Mollel on March 25, 2013 at 13:58

Wanataka  yawe matangazo au

Comment by Hashim Said on March 25, 2013 at 13:47

Natamani siku moja wawili (mwanamke na mwanaume) kati ya wanakamti, mmoja abakwe na mwingine alawitiwe ndo watajua ukweli wa wanafunzi wa IFM

Comment by Mama Malaika on March 25, 2013 at 12:47

Iwapo watoto wa vigogo wangebakwa ungesikia shughuli na siajabu wangehukumiwa wengi hata wasio na makosa. Lakini kwa kuwa waliobakwa ni watoto wa wavuja jasho basi Sirikali ya TZ na kamati zake bubu daima watasema madai sio ya ukweli, wanafunzi waongo.

Comment by Hashim Said on March 25, 2013 at 12:21

Madai ya wanafunzi wa IFM ni yakweli kabisa!

Kama alivyotangulia kusema ndg. Mgao na mwenyekiti Tujlonge, ni vigumu sana mtu kujitokeza mbele ya kamati kwamba alilawitiwa au alibakwa sababu ni aibu. Kwahiyo mtu anaona kwamba tayari ishatokea na aliyemfanyia hamjui , anaamua kupiga kimya. Mimi binafsi nasema madai yao ni ya kweli sababu mdogo wangu alinipigia simu usiku huohuo wa tukio na kesho yako ndo nikavisikia kwenye vyombo vya habari.

Comment by MGAO SIAMINI,P on March 25, 2013 at 10:05

suala la kulawitiwa na kubakwa hata kwenye jamii watu hawasemi wala hata kesi hawapeleki polisi kwa utamaduni wetu ni jambo la aibu na linafedhehesha sio  rahisi sana kutaja kwa mahojiano.

Comment by Mjata Daffa on March 25, 2013 at 8:56

Inawezekana ikawa kweli au uzushi tusi comment 1 kwa 1 maana wakati mwengine mtu anapodai jambo lake anaweza kuongeza chumvi some time inabidi tuiamini serikali tusiwe negative wakati wote. mm pia nmesoma IFM nayajua mazingira ya chuo changu mengine ni aibu kuyataja hapa

Comment by Dixon Kaishozi on March 25, 2013 at 8:25

Hawa ni wazushi tu.. ukisha jitangaza alafu iweje ?

Comment by Tulonge on March 25, 2013 at 6:56

Ila inahitaji moyo mgumu kujitangaza kuwa ulibakwa/lawitiwa

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*