Tulonge

Naibu Waziri Elimu katika kashfa ya vyeti

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo anadaiwa kutumia ujanja katika wasifu na elimu yake ambapo katika maisha yake ya kielimu ametumia majina manne tofauti.

 

Philipo Augustine Mulugo ndiyo jina lake halisi ambalo alilisomea mpaka alipohitimu darasa la saba kwa mara ya kwanza 1988, lakini kutokana na kwamba hakufaulu kwenda sekondari alirudia darasa hilo.

 

Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi kwa takriban miezi mitatu sasa umebaini kuwa 1989, Mulugo alirudia darasa la saba katika Shule ya Msingi Rukwa ya mkoani Mbeya akitumia jina la Hamimu Hassan.

 

Imebainika kuwa kabla ya kuhitimu darasa la saba kwa mara ya pili, alibadili jina hilo (kutoka Hamimu Hassan) na kuwa Hamimu Augustino ambalo aliendelea nalo wakati akisoma elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari kutwa ya Mbeya (Mbeya Day) mwaka 1990.

 

Hata hivyo, Mulugo mwenyewe akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam alipuuza tuhuma hizo kwa kusema kuwa ni njama za kisiasa zinazofanywa na maadui zake. Mulugo anasema madai hayo yamekuwa yakitolewa mara kwa mara na amekuwa akiyajibu kwa kuwaonyesha vyeti vyake halali vya shule.

 

“Hayo madai ni ya muda mrefu, wewe sijui utakuwa mtu wa 20 kuuliza swali kama hilo. Mimi vyeti ninavyo na hata ukitaka ushahidi nitakuonyesha,” alisema Waziri Mulugo na kuongeza:

 

“Haya mambo kabla hata sijachaguliwa kuwa Mbunge, tulivyokuwa bado kwenye mchujo wa ndani, usiku wa manane watu walisambaza huu uvumi na nilivyoenda kwenye kikao nikatoa vyeti vyangu, wakaviona.”

 

Waliomfundisha

Baadhi ya walimu waliomfundisha Mulugo, watu waliofanya kazi naye pamoja na wakazi wa Kijiji cha Udinde alikozaliwa, maelezo yao yanathibitisha mabadiliko ya majina ya Mulugo kwa nyakati tofauti pia ngazi mbalimbali za kielimu.

 

Uchunguzi unabainisha kuwa baada ya kuhitimu kidato cha nne, alifaulu kwenda Shule ya Sekondari ya Wavulana, Songea ambako alisoma kati ya 1994 na 1996 akiendelea kutumia jina la Hamimu Mulugo.

 

Baada ya kuhitimu kidato cha sita, uchunguzi ulibaini kuwa Mulugo alirejea Mbeya na 1998 alilazimika kubadili tena jina pale alipotumia cheti cha mtu aitwaye Dickson Mulungu, kuombea kazi ya kufundisha katika Shule ya Sekondari ya Southern Highlands.

 

Habari zinasema Mulugo alichukua hatua hiyo ili kumshawishi mmiliki wa shule hiyo mfanyabiashara, Gulnoor Dossa (sasa ni marehemu), kumpa nafasi ya kufundisha shuleni hapo.

 

“Mulugo alilazimika kutumia cheti cha rafiki yake aliyekuwa akiitwa Dick Mulungu ambaye alipata daraja la pili katika Shule ya Sekondari ya Songea Boys, hivyo ikawa rahisi kwake kupata kazi ya ualimu katika shule hiyo,” alisema mmoja wa waliofanya kazi naye shuleni hapo (jina tunalihifadhi kwa sasa).

 

Aliongeza kuwa Mulugo alianza kama mwalimu wa kawaida, lakini baadaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Shule (headmaster) wakati hakuwa hata na cheti cha ualimu. Alichukua nafasi hiyo ya ukuu wa shule baada ya aliyekuwapo kufariki dunia.

 

“Unajua wale wahindi (wamiliki) walikuwa ni wafanyabiashara kwa hiyo hawakufuatilia kiwango cha elimu ndiyo maana walimpandisha tu madaraja bila kujali kuwango cha elimu,” alisema rafiki yake huyo na kuongeza:

 

“Nilimshauri aachane na cheo hicho kwani kama ungefanyika ukaguzi wa Serikali na kumkuta bila vyeti vya ualimu angechukuliwa hatua, hivyo alinisikiliza na akaachia nafasi hiyo na kujipa cheo cha umeneja wa shule.”

 

Chanzo: mwananchi.co.tz

Views: 590

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Dixon Kaishozi on March 26, 2013 at 16:32

Cha !!! hao ni Mapompompo tupu!!! Niliangalia "live" wakati wanatoa tuzo za maajabu saba ya ASILI ya AFRICA - Serengeti ikiongoza kwa wanyama wanavyo hama kwenda kenya na kurudi, ikifatiwa na Ngorongora alafu Mlima Kilimanjaro!!!!

Kilicho niacha hoi, yani nipo mwenyewe naangalia TV,, lakini naona aibu vile WAKURUGENZI WA HIFADHI YA NGORONGORO, TANAPA NA MLIMA KILIMANJARO walivyokuwa wanatiririka KIINGEREZA !!! Sikujua huo ukurugenzi waliupataje!!!!

Hiyo hotuba waliyokuwa wanatoa wakati wanapokea hizo tuzo!!! Mungu mwenyewe ndiyo anajua!!!

Comment by Mama Malaika on March 25, 2013 at 18:56
Cha umesema kweli. Nyumbani kazi za kupeana kujuana, ukiwa na vyeti huthaminiwi, nchi za watu unathaminiwa
Comment by Mama Malaika on March 25, 2013 at 18:50
Cha..... Umeniacha kichwa nakuna. Waziri hajui Muungano wa Tanganyika & visiwa ulifanyika lini?
Comment by CHA the Optimist on March 25, 2013 at 16:59

Mjata, kuhusu Usalama ni jina tu. Hawajui nini wanachotakiwa kufanya, ndiyo maana kuna mambo yanatokea katika nchi hii kana kwamba hiyo idara ya usalama haipo, ama ipo likizo, ama ilishakufa siku nyingi.

Yaani they .................................

...........................STILL LOADING.........(network busy---try again later).........(try to restart your device...or refresh page to continue).........

Comment by CHA the Optimist on March 25, 2013 at 16:54

Hii ndio Tanzania, walio na sifa hawapewi nafasi kwa ajili ya kufanya kazi fulani, na wasio na sifa kama huyu naibu waziri ndio wanaopewa nafasi. Tatizo si waziri, tatizo ni aliyemteua.

Waziri gani wa Elimu hajui hata Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulifanyika lini? Waziri gani hajui matokeo ya Tanzania ni muungano wa nchi na visiwa vipi?

Ndiyo maana wanafunzi wa form four wali-fail mitihani yao ya mwisho. Sasa kama Waziri hajui historia ya nchi, itakuwaje kwa wanafunzi wa walio chini ya wizara ya waziri "kihiyo"

Nchi hii lazima tuibadilishe kisiasa, tukiendelea na hii serikali ya CCM, tutaishia kuwa wasindikizaji katika hii dunia inayosonga mbele kimaendeleo kwa kasi.

Comment by Longumok L. Mollel on March 25, 2013 at 13:53

Hii

Comment by Mama Malaika on March 25, 2013 at 12:33

Ama kweli bongo tambalale. Halafu huyu ndio Naibu Waziri wa moja kati ya wizara 5 muhimu TZ, nawapa pole wazazi. Kwa mtaji huu elimu inazidi kutiririka...........

Comment by MGAO SIAMINI,P on March 25, 2013 at 10:24

Huyu jamaa ukimsikiliza kwenye mahojiano mbalimbali na namna anavyotekeleza majukumu yake utagundua uwezo wa kufikiri na kutatua migogoro ni mdogo mimi niliwahi kumtilia mashaka mapema kweli baada tu ya uteuzi wake kuwa naibu waziri,alikua anaifungia shule fulani haikuwa na vigezo.Tatizo kubwa tulilonalo watanzania wenye uwezo na hasira ya maendeleo wako nje ya mfumo kwa sababu wanatakiwa watu wa jamii ya kina mulugo 'ndio mzee'.Enzi za mwl Nyerere ilikua huwakuti wakina mulugo kwenye madaraka makubwa.

Comment by Mjata Daffa on March 25, 2013 at 9:06

Doh aibu ila wapo wakina mulugo wengi, sasa baada ya kugundua hili nininkinafuata? jamani hivi hawa watu wa usalama hamshauri Raisi vizuri au Raisi anachagua mawaziri kwamatashi.

Comment by Dixon Kaishozi on March 25, 2013 at 8:33

.............. Loading................

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*