Tulonge

Watuhumiwa 11 wa jengo lililoanguka Dar kizimbani

Mtuhumiwa namba moja wa mashtaka 24 ya kuua bila kukusudia, Raza Hussein Ladha (kushoto) akipelekwa chini ya ulinzi wa polisi kuingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam jana. Picha na Michael Jamson

Dar es Salaam. Mfanyabiashara Radha Hussein Ladha wa jijini Dar es Salaam, Diwani katika Manispaa ya Kinondoni, Ibrahim Mohamed maarufu kama Kisoki (59) na wenzao 9, jana walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 24 ya kuua bila ya kukusudia.


Katika kundi hilo pia wamo vigogo wa Manispaa ya Ilala ambao ni Mhandisi Mkuu, Mhandisi Charles Salu (48), Mhandisi wa Majengo Godluck Sylivester (35) Mbaga na Mkurugenzi Mkuu wa Mkaguzi wa Majengo, Willibrod Wilbard (42).


Washtakiwa wengine ni Mhandisi Mohamed Swaburi (61), Mhandisi Mshauri, Zonazea Oushoudada (60), Mkadiriaji Majenzi, Vedasto Nziko (59), Msanifu Majengo, Michael Hema (59), Msajili Msaidizi AQRB, Albert Mnuo na Ofisa Mkuu Mtekelezaji OQRB, Joseph Ringo.


Akisoma hati ya mashtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi, Devotha Kisoka, Wakili wa Serikali, Tumain Kweka akisaidiana na mawakili wenzake watano, alidai kuwa washtakiwa walifanya makosa kinyume na kifungu cha 195 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho 2002.


Kweka anasadiana na wenzake Benard Kongora, Ladslaus Komanya, Neema Haule, Joseph Maugo na Mutalemwa Kishenyi.


Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao kwa pamoja Machi 29, mwaka huu katika Mtaa wa Indira Gandhi, Wilaya ya Ilala waliwaua bila ya kukusudia Yusuph Mohamed, Kulwa Khalfan na Hamada Mussa.


Mbali na watu hao, pia wanadaiwa kuwaua bila ya kukusudia Kessy Manjapa, Khamis Mkomwa, Boniface Benard, Suhail Ally, Salmani Akbar, Seleman Haji, Seleman Mtego, Sikudhani Mohamed, Ahmed Milambo, Salum Mapunda, Suleiman Rashid na John Majewa.


Wengine ni Mussa Mnyamani, David Severin Herman, William Joackim, Abdulrahman Mwiha, Emmanuel Christian, Mmanyi Ngadula, Adivai Desiki, Emmanuel Greyson na Augustino Kasiri.
Washtakiwa wote hawakutakiwa kujibu chochote kwa sababu mashtaka yanayowakabili Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza hadi Mahakama Kuu.


Mawakili wa utetezi wakiongozwa na Wakili wa Kujitegemea, Jerome Msemwa waliiomba mahakama kutoa dhamana kwa wateja wao kwa sababu mashtaka ya kuua bila ya kukusudia yanayowakabili yanadhaminika.


Wakili wa Serikali, Kongora alipinga maombi hayo, huku wakili mwenzake Komanya akisema kuwa wakati huu si wa kutoa dhamana kwa kuzingatia mazingira ya tukio lililosababisha kuwepo kwa kesi hiyo.


Kutokana na hoja hizo, Hakimu Kisoka aliiahirisha kesi hiyo hadi Aprili 16, mwaka huu atakapotoa uamuzi iwapo washtakiwa wapate dhamana ama la.
Naye Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ametangaza kiama dhidi ya wamiliki wenye maghorofa yaliyojengwa kinyume cha utaratibu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye Ofisi ndogo ya Bunge, Profesa Tibaijuka alisema kwa kuanzia angesaini hati ya kuamuru kubomolewa kwa jengo lililokuwa karibu na lile lililoanguka wiki iliyopita na kuua idadi kubwa ya watu.
Alimwonya mmiliki wa jengo hilo anatakiwa kufanya ubomoaji mara moja tena kwa gharama zake.


“Serikali ikibomoa jengo hilo ina maana atatakiwa kulipia gharama za zoezi hilo,” alionya Profesa Tibaijuka, ambaye aliapa kuanza leo ukaguzi wa maghorofa mbalimbali ya jijini Dar es Salaam.

Chanzo: mwananchi.co.tz

Raza Hussein Ladha (kulia) na watuhumiwa wenzake kumi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo. (picha: Habari Mseto blog)

Views: 720

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Longumok L. Mollel on April 6, 2013 at 10:32

 R.I.P mliofariki kwa kuangukiwa ghorofa

Comment by eddie on April 5, 2013 at 15:47

Hao wachina ndio kabisa mimi siwaamini katika ujenzi. Maana nikiangalia tools zao ambazo si durable mijengo itakuwaje sasa?

 Hi vikaribuni nilisikia huko uchina kuna nyumba ilimezwa na sink hole.

 

Comment by Mama Malaika on April 5, 2013 at 14:12

Kusema ukweli, mie nyumbani TZ naogopa sana kununua nyumba ambayo zimejengwa kuanzia kipindi cha mzee ruksa, wahandisi na wakandarasi wanachakachua sana sana. Na hata hao wachina nimeona wanajenga majengo TZ wengi wao hovyo.

Wote wamechangia jengo kuanguka lakini huyo mkaguzi ndio awe mshtakiwa number moja kwani anahusika na ukaguzi wa stages zote za ujenzi. Na pia office za jiji kitengo cha watoa vibali vya ujenzi lazima nako wafuatiliwe kwani kuna wataalamu (quantity surveyors, etc.) kwenye kitengo tunapopeleka application forms kuruhusiwa kujenga nyumba/jengo kwani lazima uambatanishe mchoro wa jengo unalotaka kujenga toka kwa architecture wako ajili ya ukaguzi kabla hujapewa Building Permit. Sasa kama mahesabu ya kwenye mchoro yalikuwa hayajajitosheleza na wao wakatoa Building Permit kwa kupokea hongo basi waburuzwe mahakamani.

Comment by Mama Malaika on April 5, 2013 at 13:30

Dixon... Hujakosea hata kidogo, huyo Tibaijuka inapaswa awajibishwe. Angekuwa hapa UK angeshikwa shingo kabali na kuondoka madarakani ili siku ya pili jengo kuanguka ili kuachia uchunguzi na case ifanywe huku kukiwa na uongozi mpya na sio yeye tena.

Comment by eddie on April 5, 2013 at 11:57

Yaani hawa jamaa wameniudhi kweli.

Yaani nazidi kujiuliza ni yupi hasa amefanya kosa kubwa kati yao, maana kila mtu hapa ana sehemu yake ya kazi, unaweza ukakuta mmoja hakufanya inavyotakiwa basi wote wanasomba lawama.

 Kama ni architect basi huenda cheti amenunua, maana kama angeenda shule kule wanafundishwa STRENGHT OF MATERIALS , ni sawa na seremala kutengeneza kiti ambacho kina miguu ya mabua ya mtama, ukikalia kiti hicho utajikuta uko chini.

 Maana hilo ghorofa lazima mahesabu yakae vizuri ili kuhakikisha pillars na nondo zakezinastahimili uzito ambao uko kwenye uwiano.

Comment by eddie on April 5, 2013 at 11:29

Yaani hilo jengo halijaisha linaangunga, na hapo bado havijawekwa vitu kama furnitures na appliances du!

Omy ukaguzi kama unafanywa na mtu ambaye ameamka na konyagi kichwani au ananuka chibuku usitegemee kama kutakuwa na usalama wa jengo!

Nidhamu inatakiwa iwe ya hali ya juu!

Comment by Omary on April 5, 2013 at 0:07

Nikawaida ya viongozi wa TZ kuchukuwa hatuwa baada ya maafa sijui siku zote wanakuwa wapi? kufanya kazi iliowaweka kazini yaani wanakuwa kama mkasi haufanyikazi mpaka ushikwe kwa nyuma viongozi wetu wanajisahau sana sio mara ya kwanza jengo kuanguka kama sikosei mtaa wa zanaki karibu na hosptal ya Dr Khan kuna jengo lilijengwa likaanguka wakati wanafanya umaliziaji wa mwisho kwa taalifa waliotowa liliwa mtu 1 sijui kweli? sina hakika na mpaka leo sijui kesi iliendaje? ila kwakuwa halikuuwa watu wengi hawakufanya ukaguzi sasa ndio wanajidai kufanya ukaguzi, kuna majengo yapo masaki yalijengwa mpaka kuisha kila kitu eti wakaanza kuyabomowa wanasema yapo karibu na bahari na nimarefu wakapelekwa mahakamani wakashindwa ikawalazimu wayajenge tena shem walizobomoa wakajenga na ni pesa zetu wananchi zilizotumika kujenga bado tu hawajajifunza ndiomana wananchi wanakosa imani nao kwa mambo yao kiukweli hata mimi hainiingii akilini jengo lijengwe mpaka kuisha then uje ubomowe siku zote uko wapi? kama selekari yetu ingesimamia vema sheria zake wasingewachukulia hatuwa wamiliki wakuchukuliwa hatuwa ni watendaji wakuu waliokalia viti bila faida wakati watu wanatafuta kazi mpaka wanakimbia mjikwendakusaka kazi sehem nyengine yaani mie inaniuma kweli pia inatowa imani na kutia hasira ukiangalia watu wasio na hatia wanavyopoteza maisha na kuacha watoto wasio na baba kwa maafa ya kizembe MUNGU wahukumu watendaji wasiowajibika kilichobaki nikumuachia MUNGU maana hakuna wakuwahuku.

Comment by eddie on April 4, 2013 at 11:32

Hawa lazima waozee gerezani. Wezi wakishikwa barabarani huuawa kwa kipigo, hawa wameua wanastaili kufungwa na kulazimishwa kufanya kazi ngumu hadi mwisho wa maisha yao.

Comment by Dixon Kaishozi on April 4, 2013 at 10:26
Huyu pro. Tibaijuka namkubali sana! Shida ni kwamba viongozi wetu wanakurupuka pindi tatizo au maafa yanapo tokea. Sasa alikuwa wapi siku zote kufanya ukaguzi? leo mjengo umeua ndiyo ANAAPA kufanya ukaguzi wa majengo marwfu dar! Nikisema na yeye ajuishwe na hao wengine nitakuwa nimekosea?
Comment by Christer on April 4, 2013 at 9:59

Poleni ila mmeuwa watu wengi sana.

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*