Tulonge

Video:Binti Mtanzania aliyekamatwa Misri akituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya

Kwa mujibu wa tovuti ya SalmaMsangi.com, yupo binti kwa jina Fatma almaarufu huko Ilala, Dar es Salaam kwa jina la Brown Berry ambaye inasemekana amekamatwa nchini Misri kwa tuhuma za kusafirisha madawa ya kulevya.

Link ya video (imepachikwa hapo chini) iliyowekwa na mmoja wa watoa maoni kwenye mtandao wa Instagram baada ya SalmaMsangi kuweka maelezo na picha ya mtuhumiwa, inaonesha mfuko wa plastiki ukiondolewa chini ya sanduku dogo ukiwa na kitu kama “unga” ndani yake.

Habari zaidi kutoka kwenye blogu ya William Malecela zinasema amepigiwa simu na ndugu wa mtuhumiwa
baada ya taarifa za binti yao kusambaa katika mitandao ya kijamii, na kusema kuwa ni kweli kuwa ndugu yao amekamatwa ila si kweli kuwa amehukumiwa kunyongwa nchini Misri siku ya Ijumaa, Juni 7, 2013 kwani bado hata hajahukumiwa.

Inaelezwa pia kuwa ingawaje asili ya Fatma ni Tanzania, uraia wake ni wa Oman kwa mujibu wa pasipoti aliyokamatwa nayo.

Via: wavuti.com na peruzibongo blog

Views: 814

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by salum kitila on June 6, 2013 at 21:39

mmh

Comment by KUNAMBI Jr on June 6, 2013 at 14:24

janga tena kubwa tu ndo wakome lkn

Comment by David Edson Mayanga on June 6, 2013 at 11:11

ILA MABINTI SIKU HIZI WAMEIBUKIA SANA KUWA NA BIASHARA HALAMU KAMA HIZI TENA WANAJIFANYA KUWA WANAWEZA KUMBE BIASHARA HALAMU NYIE WAKINA DADA NYIE HAYA YAMEWAKUTA JAMA ILA  POLE SANA

Comment by David Edson Mayanga on June 6, 2013 at 11:07

MAMA YANGU WEE

Comment by ANGELA JULIUS on June 6, 2013 at 7:29

Kama mzazi tumbo linaniuma in a different ways.

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*