Tulonge

Wadau mnamkumbuka Kibakuli wa Kaole Sanaa Group? Huyu hapa

Dar. Mwigizaji wa tamthilia aliyewahi kutamba miaka ya 90 katika kundi la Kaole Sadiki Mbelwa maarufu kama Kibakuli ameibuka upya katika tasnia ya filamu akifanya kazi tofauti kabisa na kipaji chake cha awali.

Akizungumza Kibakuli alisema kwa sasa yeye ni soundman (anayehusika na marekebisho ya sauti katika filamu) kwenye kampuni ya Landline Production na punde anatarajia kurudi tena katika uigizaji.

“Nimekuwa nashika boom na kufanya marekebisho mengine ya sauti katika filamu lakini hivi punde natarajia kurudi tena katika ulimwengu wa filamu watu waendelee kunisubiri tu,” alisema Kibakuli ambaye kwa sasa hana mwili mkubwa kama ilivyokuwa awali.

Kibakuli alikuwa staa kwenye maigizo ya Kaole kama mtoto mnoko wa Muhogo Mchungu ambaye anajua kama baba yake ana nyumba nje lakini hamwambii mama yake mzazi.

Mwishowe na yeye anakuja kumtaka kimapenzi mama yake mdogo.

Kikubwa kilichokuwa kinamtambulisha Kibakuli ulikuwa ubonge wake, tofauti na sasa amekuwa mwembamba na amekuwa mtu mzima.

Kibakuli alianza kuigiza kwenye miaka ya 1999 yupo darasa la sita wakati akiwa na Nyamayao ambaye alikuwa anaigiza kama dada yake.

Via: mwananchi.co.tz

Views: 2333

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by jemadari mimi on June 10, 2013 at 15:44

Jamaa ananikumbusha mbali sana pale kaole sanaa group ilikuwa c mchezo,kulikuwa na waigizaji mahiri sana mf km swebe,kemmy, bambo,max,zembwela,mashaka,mzee upara  na wengineo.

Comment by Mjata Daffa on June 8, 2013 at 11:06

Safi sana Kibakuli unaonekana sasa upo kikazi KWELI KWELI. huo ndio mwili wako original pigana mwangu kuwa bonge sio sifa mambo you Mkwanja

Comment by paul michael on June 7, 2013 at 22:35

afu alikuwa mbishi sana dhidi ya dada ake nyama yao na fadher ake muhogo

Comment by Dixon Kaishozi on June 7, 2013 at 15:22

Hahahahaaa... Dogo alikuwa bega kwa bega na baba yake muhogo mchungo... Kweli majukumu noma!!!

Comment by chaoga on June 7, 2013 at 12:27

UNAFANYA MASIHARA NA MAJUKUM, MIE NIMEYAKUMBUKA MACHO YAKE TU....

Comment by KUNAMBI Jr on June 7, 2013 at 9:39

upepo wote umepungua

Comment by paul michael on June 7, 2013 at 0:26

ule ulikuwa mwili wa kitoto, sasa ni mtu mzima ndio maana yuko hivyo kwa ss

Comment by Tulonge on June 6, 2013 at 23:56

Huwezi amini, enzi hizo dogo alikua MNENE balaa

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*