Tulonge

Hii hatari: Bondia atandikwa konde hadi akaona majini mbele yake

Bondia Ramadhani Kido akiwa chini baada ya kupigwa konde na Chupaki Chipindi.

BONDIA Ramadhani Kido wa jijini Dar es Salaam, Ijumaa iliyopita aliushangaza umati uliofurika kwenye Ukumbi wa Dar Live, Dar es Salaam baada ya kusema ameona jini mbele yake.

...Akiinuka baada ya konde hilo.

Kido alitoa kauli hiyo baada ya kutandikwa konde zito la kidevuni na mpinzani wake, Chupaki Chipindi wa Iringa.


Katika pambano hilo lililokuwa la raundi sita, Kido alitandikwa konde hilo katikati ya raundi ya kwanza na kuanguka mzimamzima ulingoni, kisha akainuka na kujaribu kuendelea lakini akashushiwa konde jingine kidevuni lililomlaza chini, hivyo kujikuta akipoteza pambano hilo kwa K’O katika raundi hiyo.

Akizungumza na Championi Jumatatu baada ya pambano hilo, Kido alisema kabla hajapigwa konde la kwanza lililomdondosha chini, aliona kitu cha ajabu kama jini mbele yake, kisha akashtukia kishindo kizito kwenye taya lake.

...akiwa chini tena baada ya kupokea konde lingine lililomaliza mchezo.

“Yaani hata sielewi ni kitu gani, nimeona kitu fulani kama jini mbele yangu kimenipitia kwa kasi, kabla ya kusikia kishindo kizito kikitua kwenye taya langu na kujikuta naanguka chini na kupoteza pambano,” alisema Kido.

via: thechoice

Views: 608

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Geoffrey Masai on August 13, 2013 at 14:36

haahaahaahaaa, jini alione peke yake refa hasilione, kama vipi wote wawili walikua nayo.

Comment by KUNAMBI Jr on August 13, 2013 at 14:21

hahah ahah haah haha hana lolote alikua anaona nyota tu huyo baada ya konde zito

Comment by ANANGISYE KEFA on August 12, 2013 at 18:41

michezo ni furaha lakini siyo kwa mchezo wa ngumi

Comment by Tulonge on August 12, 2013 at 16:27

Huwa wanasema michezo ni furaha. Sasa hii sijui ni furaha au nn

Comment by George on August 12, 2013 at 16:19

Hahahahhahahahahahahahahaaaa!!!

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*