Tulonge

Mbunge Ester Bulaya yu tayari kufa katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Mara, Esther Bulaya

Huu ni ujumbe alioutuma kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii facebook akiwapa wadau taarifa kuhusu mpango wake wa kuongelea dawa za kulevya Bungeni

Baada ya kuzungumzia suala la dawa za kulevya mbunge huyo alisema yupo tayari kufa lakini hawezi kuogopa kusimama kidete kupinga biashara ya dawa za kulevya. Baada ya kulizungumzia suala hilo bungeni, alipokea zaidi ya jumbe za simu 2,000 za kumpongeza na chache kati ya hizo zikiwa za vitisho toka kwa watu asio wajua.

Mbunge huyo aliongeza kuwa, endapo atauawa kutokana na jambo hilo basi itakua ni mpango wa Mungu. Anaamini wataibuka kina Ester wengine ambao wataendeleza mapambano hayo. Alisema ni sawa alivyoondoka Amina Chifupa, lakini wameibuka wengine wanaoendeleza mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

Views: 1631

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by habiba mustafa mlawa on November 11, 2013 at 9:37
umeona ee zainab
Comment by Zainabu Hamis on November 7, 2013 at 18:26

Wajua hawa politicians wanasaka sana umaarufu ili kujijenga kisiasa, sasa isiwe mrembo anautaka umaarufu. Jamani umaarufu mtamu jamani. Chezea umaarufu wewe.

Comment by ANANGISYE KEFA on November 7, 2013 at 12:26

alipambana amina chifupa alipofikia hatua ya kuwasilisha majina ya wafanyabiashara ya madawa ya kulevya bungeni akafarika, akaibuka rais kikwete akadai naye majina anayo lakini mpaka sasa yupo kimya, juzi tu hapa kaibuka mwakyembe akadai yeye tayari ni maiti kwa hiyo haogopi kitu kikubwa alichofanya ni kutuonyesha picha za makuli wa airport na sasa naye kimyaaaaaaa, haya na wewe dada yetu esther tunasubiri jipya lako.

Comment by Severin on November 6, 2013 at 23:36

Mi macho mawazo yangu yapo kwa huyo mheshimiwa jinsi alivyo mrembo,nani mwenye namba yake ya simu jamani?

Comment by CHA the Optimist on November 6, 2013 at 17:19
Tunataka vitendo-Bla Bla hapana!
Comment by CHA the Optimist on November 6, 2013 at 17:19
Tunataka vitendo-Bla Bla hapana!
Comment by Mama Malaika on November 6, 2013 at 12:57
Hao wanao kutishia maisha yako Ester wanasahau kuwa kila mja ataonja mauti. Mie niko nyuma yako.
Comment by Christer on November 6, 2013 at 10:15

Haya haya haya hayaaaaaaa

Comment by Mjata Daffa on November 6, 2013 at 9:02

washa moto mama usiogope ulizaliwa siku moja utakufa siku moja, pambana usiogope tuko nyuma yako ukifika 

Comment by habiba mustafa mlawa on November 6, 2013 at 8:53
Alikufa Amina chifupa na hakuna aliyeunga mkono itakuwa wewe Esta all da best

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*