Tulonge

Mbeya: Mzee aliyezikwa hai afukuliwa na kukutwa mfu kisha kuzikwa tena kwa utaratibu mzuri

JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu 12  akiwemo Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mshewe wakituhumiwa kwa kosa la kuua mtu kwa kumzika akiwa hai.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa lilitokea juzi majira ya  saa 08:30  mchana  novemba 6 mwaka huu  katika kijiji cha Mshewe, kata   ya  Mshewe , tarafa ya  bonde la Usongwe wilaya ya  Mbeya vijijini Mkoani hapa.
Alimtaja marehemu kuwa ni Alison maarufu kwa jina la  Hanahela Mwakabana(80) kyusa, mkulima, mkazi wa kijiji cha Mshewe ambaye  aliuawa na kundi la wananchi  walioamua kujichukulia sheria mkononi.
Alisema wauaji hao walikuwa  wakiongozwa na   Julius  Katisha Ngole ambaye ni mwenyekiti wa kijiji cha Mshewe baada ya  kumfukia ndani ya  kaburi akiwa hai.
Alisema  chanzo cha mauaji hayo ni tuhuma za kishirikina baada ya  marehemu kutuhumiwa kumuua mtoto wake Juma Hanahela(48) kyusa, fundi ushonaji, mkazi wa kijiji cha Mshewe aliyefariki dunia  Novemba 5, mwaka huu kwa maradhi ya  kiharusi ambayo alianza kuugua Oktoba 29, Mwaka huu na kulazwa hospitali teule ya  Ifisi.
Kamanda Diwani alisema mbinu iliyotumika ni  watuhumiwa   baada ya  kumaliza kuchimba  kaburi walimwambia marehemu aingie ndani ya  kaburi ili apime kama linatosha kumzika mtoto wake ndipo walipomfukia, kisha kuchimba kaburi lingine pembeni na kumzika mtoto wake  Juma Hanahela.
Kwa mujibu wa Mjomba wa Marehemu ambaye alikuwa shuhuda wa tukio hilo,Edward Mwaikasu aliliambia JamboLeo kuwa wakati taratibu za mazishi ya mtoto wao zinaendelea aliwashauri kumwita mchungaji yeyote wa kanisa lililokaribu jambo ambalo liliafikiwa na Mwenyekiti wa Kitongoji.
Alisema wakati wakisubiri taratibu hizo kufanyika Mwenyekiti alisikika akimtuhumu Marehemu kuwa ndiye aliyemuua mwanae hivyo adhabu inayostahili dhidi yake inaandaliwa na lazima naye ashughulikiwe.
Alisema wakati Mwenyekiti akiongea hivyo waliokuwa wakichimba kaburi kwa ajili ya kumzika Marehemu walimwita wakitaka asaidie kuchimba shimo ambapowalimtaka kuingia ndani ya shimo na kutoa udongo ambapo baada ya kufanya hivyo walianza kumrushia udongo na kumfukia.
Alisema kutokana na tukio hilo Mwenyekiti alishauriwa apige simu polisi akidai kuwa Marehemu alifanya tukio msibani hivyo wananchi wenye hasira kali wamemuua hivyo nay eye kukubaliana na ushauri huo.
Kutokana na tukio hilo Jeshi la Polisi linawashikilia  watuhumiwa kumi na mbili 12 kuhusiana na tukio hili wakiongozwa na Mwenyekiti Julius Katisha Ngole(52) msafwa, wote wakazi wa kijiji cha mshewe.
Kamanda Diwani alisema  taratibu zinafanywa ili watuhumiwa wafikishwe mahakamani na pia mwili wa marehemu ufukuliwe na kufanyiwa uchunguzi  wa kitabibu ili uzikwe upya kwa heshima na taratibu zinazopaswa. 
lakini mpaka hivi sasa mwili haujaweza fukuliwa  na pia wananchi wametoweka kijijini hapo hivyo shughuli za kiuchumi kuzorota.
JUHUDI ZA KUENDELEA KUUFUKUA MWILI WA ALIEZIKWA HAI ZAENDELEA
NI KAZI NI NZITO NA INAHITAJI UVUMILIVU
MWILI WA ALIEZIKWA HAI WAANZA KUONEKANA
MSAMARIA MWEMA ALIYEJITOLEA KUUTOA MWILI BAADA YA KUUKUTA 
MWILI WA MAREHEMU MWAIKASU AMBAYE ALIZIKWA AKIWA HAI UKIENDELEA KUIBULIWA KABURINI
KATIKATI MJANE WA ALIYEZIKWA HAI
MWILI UKIWA TAYARI KWA KUZIKWA UPYA
NDUGU WAKIWA NA SIMANZI 
MOJA YA WANAUSALAMA AKIWASHUKURU NDUGU KWA UVUMILIVU WALIYOUONYESHA KATIKA MSIBA HUU MZITO

ULITOKA KWA UDONGO UTARUDI KWA UDONGO NDIYO NDUGU WA MAREHEMU WALIVYOKUWA WAKISEMA

SHUGHULI YA KUZIKA UPYA IKIENDELEA


SHUGHULI YA MAZISHI IMEKAMILIKA KWA AMANI NA UTULIVU LAKINI HAKUNA WANAKIJIJI WALIYOJITOKEZA KATIKA MSIBA HUU HOFU KUKAMATWA NA DOLA


Picha na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu

Views: 603

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by habiba mustafa mlawa on November 11, 2013 at 9:27
majanga, dunia imebadilika sana watu wanatoa hukumu wanajivisha mamlaka ya Mungu
Comment by ANGELA JULIUS on November 8, 2013 at 7:43

MUNGU MWENYEWE NDO ATAKAYEHUKUMU HILI NIMEWALAANI WOTE WALIOHUSIKA NA ISSUE HII DAH NI MAJONZI MAKUBWA SANA HUWEZI KUAMINI KAMA HILI TUKIO NI BINADAMU AMETENDA NA ALIYEBEBWA NDANI YA TUMBO LA MWANAMKE MIEZI 9 UWIIIIII

Comment by Omar on November 7, 2013 at 20:52

Shituka! huko tunapokwenda kunatisha! itakuwa ni ndoto watu kutenda mema kabisa.

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*