Tulonge

Mfanyabiashara wa Mwanza aua kisha kujiua Ilala Bungoni DSM

Mfanyabiashara wa jijini Mwanza, aliyefahamika kwa jina la Gabriel Munisi amefanya mauaji kwa watu wawili na kujeruhi mmoja kisha kujiua kwa kujipiga risasi katika tukio lililotokea leo asubuhi eneo la Ilala Bungoni jirani na Klabu ya Wazee jijini Dar es salaam.

Tukio hilo lililo husishwa na wivu wa mapenzi limetajwa kufanywa na Munisi baada ya kuabini nyendo za kusalitiwa na mpenzi wake aliyetajwa kwa jina la Christina Nando.

Akiwa kwenye gari lake Munisi aliwafyatulia risasi marehemu waliokuwa wakitoka getini wakiwa kwenye gari lao hivyo kumpiga risasi dereva wa gari hilo, Francis Samwel, Christina Nando na watu wengine wawili waliokuwapo ndani ya gari hilo ambapo mmoja ni mama mzazi wa Christina.

Kwa mujibu wa taarifa za awali zinasema watu wawili walifariki dunia papo hapo kutokana na tukio hilo na wengine wawili kujeruhiwa.


TAARIFA ZAIDI

Mapema leo asubuhi milio ya risasi zaidi ya kumi ilisikika eneo la Ilala Bungoni karibu na baa maarufu ya Wazee (Club ya Wazee), watu watatu wakiripotiwa kufariki kutokana na tukio hilo linaloelezwa kuwa limetokana na wivu wa kimapenzi.

Dereva mmoja wa tax kituo cha Bungoni ambaye alikuwa shuhuda wa kwanza, alisema mapema leo asubuhi alipata mteja aliyehitaji kupelekwa sehemu, ila kabla hawajafika huko walipokuwa wanataka kwenda jamaa ambaye ndiye alikuwa ni muuwaji alimuomba akatishe safari na kumtaka ampeleke sehemu nyingine.

Kwa mujibu wake dereva huyo aliendelea kusimulia, alimpeleka jamaa mpaka aneo la tukio hilo kwenye nyumba iliyopo pembeni mwa Hotel mpya iitwayo MM.

Mara baada ya kufika hapo, jamaa alitoa sh. 5,000 na kumkabidhi dereva ila cha kushangaza ni kitendo cha jamaa huyo kutoa bastola wakati akiwa anaelekea kwenye geti la nyumba, aliendelea kusimulia dereva huyo.

Wakati jamaa anaelekea getini mlango ulifunguliwa na gari aina ya Toyota Surf ilitoka ikiwa na watu wanne ndani, mwanaume mmoja ambaye ndiye aliyekuwa akiendesha gari mama mmoja na wadada wawili.

Jamaa akiwa na bastola alianza kuwashambulia watu waliokuwa ndani ya gari hilo na kumpiga risasi dereva na mdada mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Carol, hii ni kwa mujibu wa dereva huyo na mara baada ya kuona hivyo hivyo ikabidi akimbie.

Vyanzo vingine vinaeleza kuwa katika tukio hilo jamaa pia limpiga risasi ya mgongoni mama wa mwanamke aliyemuua na pia alimpiga msichana mwingine risasi ya mguu.

Mtuhumiwa na dereva aliyekuwa akiendesha gari walifariki palepale huku msichana mmoja akielezwa kufariki akiwa njiani kuelekea hospitali.

Bado haijafahamika moja kwa moja chanzo cha mauwaji hayo licha ya watu wengi ambao nilipata bahati ya kuongea nao wakilihusisha tukio hilo na mambo ya kimapenzi.
Chanzo: kajunason.blogspot.com

Views: 778

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by ANGELA JULIUS on November 21, 2013 at 14:35

MJATA UMESEMA KWELI NAKUUNGA MKONO

Comment by Mjata Daffa on November 21, 2013 at 8:57

MONICA kweli hujajua kwa nini mungu kaumba mwanamke na mwanume kweli? bila ya pea ya ME na KE wewe ungepatikan vipi? mungu hakoseagi Monica.

alichofanya mungu nikutupa muuongozo wakujua baya na zuri kisha akutupa uhuru kuchagua njia ya kufuata then atakuhukumu kwa hiari yako.

Fanya zuri ulipwe PEPO au fanya baya ulipwe MOTO full stop.

Monica bila mwanaume huenda ungekuwa unasema huvyo tu barabarani hiyo ni nature dada.

Comment by Monica on November 20, 2013 at 20:16
Mapenzi ya uzeeni hayo,katika makuzi ya binaadamu kuna hatua za kupitia,wanasaikolojia wanasema mtu akiruka hatua yeyote lazima airudiee,inawezekana jamaa aliruka hatua Fulani za malovee,sasa kapata dozi ambayo ni adimu hataki kushare,.sijui mungu alifiliria nini kuumba Wanawake na wanaume,.balaa tupu
Comment by Dunda on November 20, 2013 at 18:36

Inaelekea ule ujumbe wa kuwa na mpenzi mmoja bado haujawafikia walengwa 

Huruma sana

Comment by ANGELA JULIUS on November 20, 2013 at 16:46

DAH KWA KWELI HII HABARI IMENIHUZUNISHA TENA YANI NYINYI WANAUME WA KICHAGA MBONA MNAONGOZA KWA WIVU WA MAPENZI NA KUUA WAPENZI WENU NA MAMA WAKWE ZENU? NIMEJIULIZA SANA DAH IMETOFAUTIANA KIDOGO NA YA UFOO SARO.

UBINADAMU UPO WAPI MAISHA HAYA NIMEJIULIZA SANA MUNGU TUNUSURU KADRI YA MAPENZI YAKO AMINA

Comment by Mjata Daffa on November 20, 2013 at 8:53

DOH!! WAME MFOOSARO MASIKINI

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*