Tulonge

Taarifa kamili kuhusu Chadema kuwavua uongozi Zitto, Dk Kitila na Mwigamba

Kamati kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema imewavua Uongozi Viongozi wake watatu baada ya Kugundua waraka wa Siri uliowahusisha na mpango wa kukipasua Chama vipande vipande. Viongozi waliovuliwa Uongozi ni Zitto Kabwe ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Dr Kitila Mkumbo na Samsoni Mwigamba aliyekuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini. Hatua hiyo ilichukuliwa katika kikao cha kamati kuu kulichokuwa kimefanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam.


Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari Mh Tundu Lissu amesema katika Waraka huo kulikuwa na mtu anayejukana kama MM ambaye ni Naibu Katibu mkuu Zitto Kabwe, M1 ni Dr Kitila Mkumbo, M3 ni Samsoni Mwigamba na M2 hajajulikana ambaye ni mtumishi wa makao makuu ya Chadema. Mh Lissu amesema Dr Kitila Mkumbo alikana kabisa kumfahamu M2. Mh Tundu Lissu amesema Waraka huo uliojulikana kamanWaraka wa Ushindi unavunja katiba ya Chama kwa sababu umepandikiza chuki za kidini, majungu na kukashifu viongozi wa Chama kinyume na katiba ya CHADEMA. Mh Tundu Lissu amesema tuhuma zote zilizoko katika waraka huo hazijawahi kuwasilishwa kwenye kikao chochote halali cha chama kinyume na matakwa na masharti ya katiba yetu. Mh Tundu Lissu Amesema Kamati Kuu imeamua kuwavua nyadhifa zao zote watu wote waliotajwa katika waraka huo ambao ni Zitto Kabwe, Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba.


Pia kamati kuu imeunda kamati ya kuchunguza na kufuatilia mhusika mwingine M2 ambaye anadaiwa ni Mtumishi wa Makao Makuu ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yake.

Kamati Kuu imeagiza wahusika wote waandikiwe barua za kujieleza ni kwanini wasivuliwe uanachama kwa makosa hayo makubwa waliyofanya.


Pia Kamati Kuu imeagiza mchakato wa kumvua Zitto nafasi yake ya Unaibu wa Kambi ya Upinzani Bungeni.
Lissu amesema Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe na Dr. Kitila Mkumbo waliomba kujiuzulu nyadhifa zao zote baada ya waraka wao kukamatwa lakini Kamati Kuu iliwakatilia baada ya kuona kuwa kukubaliana na maombi yao hayo ilikuwa ni kama kuwaacha wajiuzulu kwa heshima ambayo hawaistahili hata kidogo.
Wakati huo huo kamati kuu imemteua Mh Tundu Lissu kuwa Mwanasheria mkuu wa Chama.

Chanzo: ChademaBlog

Views: 740

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by ANGELA JULIUS on November 30, 2013 at 8:58

CHA NAONA UNANICHOKOZA MWENZIO KIUKWELI KWENYE SIASA SIMO ILA CHADEMA SERA ZAO NAZIKUBALI VILIVO NA KAMA KWELI WANAMAANISHA MUNGU AWASAIDIE WAJE WAITOE NCHI MAHALI ILIPO.

KUHUSU HAWA VIONGOZI WAO KUENGULIWA MADARAKANI KWA KWELI SINA LA KUSEMA UKWELI WANANUJUA WAO BINAFSI ILA KWA KWELI SIASA NI MCHEZO MCHAFU SANA NA KAMA UKIUCHEZA KUWA MAKINI NA STEP ZAKO.

Comment by Zainabu Hamis on November 28, 2013 at 20:35

Hivi wewe CHA ni mwanasiasa nini?
duuuhhhh. kweli wewe balaa, kabla ya kutoa maoni yangu kwenye mjadala wowote ntakuwa kwanza naangalia CHA umesema nini. maana usije siku moja ukanishushua kama unavyowashushua wengine. ha ha ha ha.

Na mimi naungana na wewe, pamoja na DIXON, ila inaonesha mko affiliated na CHADEMA. Nice sana, japokuwa mimi siko affiliated na chama chochote.

Comment by CHA the Optimist on November 28, 2013 at 20:19

Dixon baadhi ya watu uwezo wao wa kufikiri, unaishia kujenga nyumba ya kuishi na kununua gari, kingine zaidi ni kuwa na mke/mme na watoto--mengineyo hawawezi kufikiri.

Ila tutafika  tu; ni wenzetu, lazima tuwaeleweshe ili kuondoa ukungu walio nao machoni au hata vichwani.

PamoJah Daima!

Comment by Dixon Kaishozi on November 28, 2013 at 20:08
Mi nashindwa kuwaelewa baadh ya watu.. hivi chadema ni mtu au ni taasisi? Asante CHA kwa kutoa ufafanuzi.. maana watu wanavyo ongea utadhani hao waliotolewa kwenye uongozi nio walio shika chama. Ina maana ingetokea Mwenyezi Mungu akawapenda zaidi ndiyo ungekuwa mwisho wa chama ? Mawazo yao ni zaidi ya mgando..

PamoJah!!
Comment by CHA the Optimist on November 28, 2013 at 19:57

CHADEMA ni taasisi; kuondokewa na mtu mmoja hakuwezi kuiua (CHADEMA). Kusema kuwa kuondoka kwa ZITTO kutapelekea chama kufa au kuzorota ni mawazo mgando au mawazo finyu!

Leo hii hata aondoke DK. SLAA, au MBOWE watu ambao wanaonekana kuwa wana ushawishi mkubwa, bado chama kitasimama na kusonga mbele.

ZITTO si muhimu sana kama ambavyo baadhi ya wadau wanafikiria.

Jamani kabla ya maoni muwe mnatafakari kwanza.

PEOPLES' POWER!

Comment by Monica on November 26, 2013 at 22:53
MM ni kama Yuda eskariot,yaani zito Kabwe ni balaa,usaliti upo kila mahali,ukifuatilia Kwa makini ni kweli alitulizwa na fedha za walipa kodi,tunalazimishwa tununue mashine na kulipa kodi kumbe fedha zetu wanafaidi wachache.mmmmmmmmmmm,mwisho Wa ubaya aibu,sipati picha zito ataifichaje sura yake,anadanganya wenzake wanasusia posho kumbe yeye anapokea mamilioni toka CCM,yaaaaaaaaaaaaaaaaaani,chadema fichueni mienendo yake yote ili watu Wa jimbo lake na wnachadema wote waujue ukweli wote ,wenye mawazo finyu wasijesema kaonewa,Eeeeee mwenyezi mungu tusaidie,
Comment by CHA the Optimist on November 26, 2013 at 18:13

Hatutaki vibaraka CHADEMA, yoyote atakayebainika kuwa msaliti atoswe tu! Tunataka walio halisi, na safi.

Peoples' power

Comment by habiba mustafa mlawa on November 25, 2013 at 9:39
wamtoe waone chama kinatakavyokufa
Comment by Dixon Kaishozi on November 24, 2013 at 15:16
Kweli kikulacho ki nguoni mwako.. hawa jamaa walikua watu muhimu sana kwenye chama kumbe ndio mapepo yenyewe..
Comment by audax mwaseba on November 23, 2013 at 22:19

Maamuzi mazito hayana budi kuchukuliwa ili kufikia maendeleo stahiki!

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*