Tulonge

12 wafariki na 30 kujeruhiwa katika ajali ya basi Tanga

Basi la Abiria la Kampuni ya Burudani linavyoonekana baada ya kupata ajali mbaya sana leo iliyopelekea kupoteza maisha kwa watu 12 huku wengine zaidi ya 30 wakiwa kwenye hali mbaya.ajali hiyo imetokea leo eneo la Kwaluguru,Kwedizinga  wilayani Handeni,Mkoani Tanga.


WATU 12 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa vibaya baada  ya basi la abiria walilokuwa wakisafiria la Kampuni ya Burudani linalofanya safari zake kati ya Korogwe mkoani Tanga kwenda Jijini Dar es Salaam kuacha njia na kupinduka. Ajali hiyo imetokea mapema leo asubuhi majira ya saa 1.30 katika eneo la Kwaluguru,Kwedizinga  wilayani Handeni,Mkoani Tanga.Akithibitisha kutokea ajali hiyo,Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga,Constantine Massawe alisema kuwa ajali hiyo iliyohusisha gari lenye namba za usajili T 610 ATR aina ya Nissan,imetokea leo na kusababisha vifo vya abiria 12 na wengine zaidi ya 30 wako kwenye hospitali ya Wilaya ya Korogwe,wakiendelea kupatiwa matibabu.Kamanda Massawe aliendelea kusema kuwa  dereva wa basi hilo ajulikanaye kwa jina la Luta Mpenda(35) ni miongoni mwa watu wanaosadikiwa kufa na kwamba miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya wilaya ya Korogwe ya Magunga.“Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya magunga na hali zao bado siyo nzuri sana lakini na miili ya marehemu pia imehifadhiwa magunga”,alisema Kamanda Massawe.Hata hivyo alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa basi hilo ambapo alipofika kwenye kona ya eneo la Kwalaguru gari lilimshinda na  kupinduka. 


Wakazi wa Wilaya ya Korogwe wakiwa wamefurika kwenye Hospitali ya Magunga walipohifadhiwa marehemu na majeruhi.


Wauguzi wa Hospitali ya Magunga wakiendelea kutoa huduma kwa majeruhi wa ajali hiyo.


Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo akitokea chumba cha maiti cha Hospitali hiyo
Chanzo: Issamichuzi Blog

Views: 986

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on December 16, 2013 at 13:40
Pole sana wana Korogwe!
Omary....... Tangaza nia tuanze kukupigia campaign mapemaaaa.....
Comment by Mjata Daffa on December 14, 2013 at 9:57

Kumbe unakumbuka harakati zetu mdogo wangu, hawo ndio watakao tuweka madarakani leo nakwenda muhimbili kutembelea majeruhi.

Kwa jicho la kisiasa tumepoteza kura 12 tayari.

Comment by Omary on December 14, 2013 at 4:16

Doh! haya kweli ni maafa Mungu zilaze roho za marehemu mahala pema peponi Amin, na Mungu waafu wagonjwa wote Kaka Daffa pole sana imetugusa wote ila apangalo Mungu hatuwezi kulipinga.

Wapiga kura wetu hao wa 2015 kabla sijatangaza nia lol.

Comment by ANGELA JULIUS on December 13, 2013 at 16:06
KAKA MJATA POLE SANA,
KAKA JEMADARI KWELI KABISA USEMAVO KWA KIASI FULANI ABIRIA HUWA TUNA HIZO TABIA.
NAWAOMBEA MAREHEMU WOTE WAPUMZIKE KWA AMANI NA MAJERUHI KUPONA HARAKA AMINA.
Comment by jemadari mimi on December 13, 2013 at 14:11

Kwanza ningependa kutoa pole kwa wale wote waliopatwa na ajali hiyoo na pia kuwaombea majeruhi waweze kupona haraka na kuendelea na shughuli zao.Lkn hapa ningependa kutoa dukuduku langu kwa upande wa abiria ambao tunasafiri kila siku na mabasi[iwe daladala au mabasi ya mkoani] tumekuwa chanzo ya yote haya ,abiria tunafurahia sana mwendo kasi na hata kumsifia dereva kwamba ni fundi wa kukimbia.Utakuta abiria wanabishana kuhusu gari walilopanda ni bovu na tena halina kasi,abiria kiukweli hatuna umoja wa kuamua jambo tunapokuwa safarini,tumekuwa watu wakulalamika tu pindi linapotokea tatizo kama hili

Comment by Mjata Daffa on December 13, 2013 at 8:23

Poleni sana wanakorogwe!!!!

wadau leo yamenikuta, mm ni mtu wa korogwe na Burudani ndio gari letu linalo tuleta DAR na kuturudisha Korogwe. wote waliopoteza maisha wananihusu kwa njia moja au nyingine. 

MUNGU awalaze pema waliotutangulia na awape nafuu waliopata majeraha AMEEN.

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*