Tulonge

Moto wawaka Bungeni: Mawaziri Nchimbi, Nahodha, Kagasheki na Mathayo washauriwa kujiengua nafasi zao


Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamisi  Kagasheki amejiuzulu wadhifa wake baada ya mjadala mkali wa Bungeni mjini Dodoma hivi sasa. Habari zaidi kwa kirefu zitakuja baadaye.
Hii inatokana na Operesheni Tokomeza iliyolenga kuondoa ujangili uliokithiri nchini. 

Tangu kuanza kwa operesheni hiyo, kumekuwa na malalamiko mbalimbali kutoka kwa wabunge, wanaharakati na wananchi dhidi ya askari waliokuwa wakiiendesha yakiwamo ya watu kujeruhiwa, kuchomewa nyumba, mifugo kuuawa, kupigwa na uporaji.

Operesheni hiyo ilikuwa ikiendeshwa kwa pamoja na askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Polisi, Usalama wa Taifa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa).

Operesheni hiyo ilizuiwa baada ya suala hilo kutinga bungeni na watunga sheria hao kuweka kando tofauti zao za kiitikadi na kuungana wakitaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki na Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Mathayo David Mathayo wawajibike.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk David Mathayo David, naye pia amegoma jiuzulu baada ya kutoa utetezi wake mrefu. Amedai pia kuwa ameonewa.


Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda ametaka uthibitisho usio na shaka kwa waliohusika wote na taasisi zao kuchunguzwa kiundani ili hatua stahiki zichukuliwa. Kuendelea kulinda rasilimali na hifadhi za Taifa ameutaja kuwa ni  muhimu. Pia amesema ameongea na Waziri mmoja mmoja kuwa ni busara ushauri wa wabunge utekelezwe. Amebainisha kuwa hata baada ya kuongea na Rais.  mkuu wa nchi ameridhia tume iundwe na kila aliyehusika awajibike.
Amesema Rais ameshauri
 kutengua uteuzi wa mawaziri wote wanne ( Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Shamsi Vuai Nahodha, Wazir wa Mambo ya Ndani Dkt Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt David Mathayo, na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamisi Kagasheki) kama ambavyo wabunge walivyopendekeza.Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe  James Lembeli (pichani juu) amesema kuwa kamati yake imeridhishwa na matokeo ya ripoti ya kamati iliyosababisha hayo yote, na kwamba maelezo ya taarifa ya kamati kimsingi yote yamekubalika.
Kuhusu kumhusisha Dkt Mathayo ni kuwa  Rais alishatoa maagizo tisa miongoni likiwepo swala la kushughulikia wafugaji wanaohamahama. Amesema pia Rais aliagiza pia kuwa wafugai wawe wa kisasa, pia kutafuta missing link ya mifugo isipotee na pia kutafuta masoko nje ya nchi, ambapo amesema mengi hayajatekelezwa.
Ameweka bayana kuwa chimbuko kubwa ni Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, na kwamba Waziri hakuwa anapewa taarifa za mara kwa mara.
Ameomba kipengele kiongezwe kuwa Katibu mkuu na watendaji wake wakuu  waliohusika kuandaa Mpango kazi wa 'Operesheni Tokomeza' wawajibishwe.
Amesema rushwa iliyoko ndani ya wizara ya Maliasili na Utalii inatisha.
Spika amuomba Mwanasheria mkuu kutumia kifungu kuongeza muda. Naye ameomba  kuundwa tume ya kisheria ya mahakama.
Spika Mhe. Anne Msekwa ameahirisha Bunge (saa tatu na dakika nne usiku huu) hadi saa tatu kesho asubuhi.  Juu ni Dkt Emmanuel Nchimbi na chini ni Mhe Shamsa Vuai Nahodha


Chanzo: Issamichuzi Blog

Views: 593

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on December 22, 2013 at 18:57
Just shaking my head! Iwapo Waziri anaona hakutendewa haki, je hao victims baada ya kutotendewa haki yeye alichukua hatua gani kuhakikisha victims wanatendewa haki? Kuna watu wamezaliwa bila common sense.

Zainabu Hamis.... Far from being indifferent, African politicians wako obsessed with their status. Ndio maana kulazimishwa kuachia ngazi ni kuonewa.
Comment by Zainabu Hamis on December 22, 2013 at 17:32

This is Africa. Wanasiasa wanang'ang'ania madaraka kana kwamba wana hati miliki ya utawala.

kwa nchi zilizo smart, hata prime minister angeshajiuzulu.

Comment by ABRAHAM PONERA on December 21, 2013 at 21:05

tatizo ni kukosekana kwa sifa za utawala bora, ambapo mawaziri na makatibu wakuu walikuwa wanaona vitendo hivyo au hata kusoma katika magazeti kilichowafanya wasisitishe hiyo operesheni ni nn? hebu Rais awatoe na mawaziri wengine walioshindwa kuzisimamia wizara zao mf. kawambwa - elimu, ghasia-tamisemi, nk.

Comment by CHA the Optimist on December 21, 2013 at 17:44

Yes, unayosema ni kweli Mama Malaika--nilimsikia Tundu Lissu akisema kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, mtumishi wa umma akiboronga, maana yake ni kwamba hata boss wake ameboronga kwa hiyo inatakiwa wote wawajibike. Ni mmoja tu kati ya watuhumiwa watano aliyeonesha ukomavu wa kisiasa (Ndg. Kagasheki) wa kujing'atua kabla hajang'atuliwa; lakini wengine wote kuanzia waziri mkuu, hadi hao wengine ambao mmoja wao alidiriki kusema hakutendewa haki, walionesha uroho wa madaraka.

Comment by Mama Malaika on December 21, 2013 at 1:00
viongozi wa Tanzania wakumbuke kuwa Cheo ni Dhamana na hakuna aliyezaliwa na cheo cha uwaziri wala ukatibu wa wizara. Nchi za wenzetu kukitokea uozo kwenye wizara fulani basi waziri husika anajiwajibisha sababu yeye ndiye nahodha na abeba jukumu la wizara.
Kama huko Dodoma viongozi hawataki kujiuzulu kwa kile wanachosema wameonewa basi mheshimiwa raisi avunje baraza lote kuanzia mawaziri hadi makatibu wa wizara ku-reboot the entire cabinet halafu tione...

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*