Tulonge

Museveni Akataa Kuidhinisha Mswada (Adhabu Kali) Dhidi Ya Mashoga Akiogopa Nchi Wafadhili Kusitisha Misaada Kwa Uganda

Pichani; Campaigners toka Uganda wakiwa kwenye Parade mjini London (2013) kuhusu Homosexuals.

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amekataa kuidhinisha mswada na amemuandikia spika wa bunge barua na kumkosoa kwa hatua ya kupitisha mswada huo December 2013.

Mswada huo unatoa adhabu kali kwa watu watakaopatikana na hatia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja ikiwemo kufungwa jela maisha na pia ni uhalifu kwa mtu yeyote kukosa kuripoti visa vya mapenzi ya jinsia moja.

Mwandisi wa BBC mjini Kampala Cathrene Byaruhanga anasema kuwa mswada huo pia unapendekeza kuadhibiwa kwa watu wanaozungumzia maisha ya wapenzi wa jinsia moja bila ya kuwakashifu kwani wanaweza kufungwa jela.

Kwa mujibu wa gazeti la Monitor, Rais Museveni amesema kwamba mswada huo ulishinikizwa zaidi kupitishwa na wabunge licha ya kuwashauri kusubiri hadi serikali itakapoutathmini.

Rais anaelewa kwamba ikiwa atauidhinisha mswada huo na kuufanya sharia baadhi ya nchi za kigeni zitasisha msaada kwa Uganda.

Raisi Museveni na viongozi nchini Uganda walikuwa mstari wa mbele kutaka iwepo adhabu kali kwa wapenzi wa jinsia moja na kusema kuwa hawana akili timamu kitu kilichopelekea nchi wafadhiri ikiwemo UK kulaani adhabu hizo kuitishia serikali ya Uganda kusitisha misaada kwa Uganda kitu ambacho kimefanya Raisi Yoweri Museveni kukataa kuidhinisha mswada huo.

Katika uamuzi wake aliotoa sasa, Rais Museveni amesema kuwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja ni watu wenye akili timamu na wanaweza kuokolewa kutokana na tabia hiyo.

Source: BBC, Jan. 17, 2014

Views: 554

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on January 29, 2014 at 20:10
Ha haa haa haaa.... CHA ni mie usimshutumu Dismas wa watu. Nili copy na ku-paste toka kwa BBC bila ku edit.

Hebu anzisha hilo darasa la kiswahili upesi maana nachanganya na kilugha mara chitumbuka, chiyao, chichewa. Teh teh teh....
Comment by Zainabu Hamis on January 27, 2014 at 20:42

ha ha ha! na mimi nimeona badala ya "mwandishi" imeandikwa "mwandisi" au labda ni msamiati mpya katika Kiswahili.

Comment by CHA the Optimist on January 27, 2014 at 19:35

Maoni yangu hayatofautiani na Superb Lecturer--Mama Malaika.

 

Comment by CHA the Optimist on January 27, 2014 at 19:33

Mwandisi wa BBC mjini Kampala Cathrene Byaruhanga anasema kuwa mswada huo pia unapendekeza kuadhibiwa kwa watu wanaozungumzia maisha ya wapenzi wa jinsia moja bila ya kuwakashifu kwani wanaweza kufungwa jela.

Dismas, hii taarifa uli-copy na ku-paste toka BBC au uli-edit?

Umeona hapo nilipo-underline?

Comment by Mama Malaika on January 18, 2014 at 13:17
Viongozi Africa ni dhaifu (kwa ngozi nyeupe) na walafi kupindukia. Museveni na ubabe na ukali wake wote kapoa kama togwa. Na huyu bwana mdogo David Cameron (UK) anawaburuza kweli viongozi wetu Africa maana mwaka 2011 alimtishia Jacob Zuma dhidi ya ushoga na mzee Zuma kesha lainika.
Comment by Mjata Daffa on January 18, 2014 at 11:32

Hatuna viongozi Afrika wote ni vibaraka wa wazungu, Mseveni njaa ndio inamsumbua mbona mwanzo alilaani vitendo vichafu vya ushoga?

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*