Tulonge

Rais Kikwete awakabidhi kadi za kujiunga na CCM baadhi ya wasanii maarufu Tanzania

Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wasanii mahiri wa Filamu hapa nchini,mara baada ya kuwakabidhi kadi za kujiunga na chama cha CCM kwenye maadhimisho ya  miaka 37 ya chama hicho huko Mbeya jana.

Katibu wa NEC, Itikadi,na Uenezi CCM Taifa,Nape Nnauye akiwatambulisha baadhi ya Wasanii nyota wa Filamu hapa nchini,ambao kwa nia thabiti wameamua kujiunga na chama hicho,wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB,Blandina Chagula,Mboto,Irene Uwoya,Single Mtambalike na wengineo.
Wasanii mahiri wa Filamu hapa nchini,wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB wakifuatilia yanayojiri hivi sasa ndani ya uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine,mkoani Mbeya juu ya kilele cha maadhimisho ya sherehe za miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho.

Mmoja wasanii Mwimbaji na Mwigizaji wa filamu,ajulikanae kwa jina la kisani kama Dokii akiimba mbele ya umati mkubwa wa wananchi na wanachama wa CCM waliofika kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama cha CCM,ndani ya uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine,mkoani Mbeya

JB akizungumza machace kwa niaba ya wenzake mara baada ya kutamka kuwa wamejiunga na chama cha CCM.

Wasanii hao wa Filamu wakifurahia jambo jukwaani.

Chanzo: Michuzi Blog

Views: 1201

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mjata Daffa on February 5, 2014 at 12:00

wakinuna shauli yao wakicheka kivyao, mbona Mr. J alijinga na chadema. mambo yote CCM ila msije tugeuka! maana wasnii kama jina lao wanaweza kufanya usanii popote pale.

Comment by Mama Malaika on February 5, 2014 at 9:36
Ha haa haa haaa... CHA the Omniscient umenifurahisha eti Mama Malaika analilia dual citizenship. Hiyo dual citizenship ni ajili ya watoto wangu ambao ni waingereza (baba yao) hata hivyo mume wangu hataki wawe na uraia wa Tanzania
Comment by Mama Malaika on February 5, 2014 at 8:33
Kwa wengi, hiyo ndio njia pekee ya kutokea. Mfano mzuri ni Komba (Captain Komba) aliyekuwa mwimbaji jeshini
Comment by CHA the Optimist on February 3, 2014 at 17:57

Ni haki ya kila aliye mwananchi wa nchi hii ya Tanzania kuwa au kutokuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa, iwe CHADEMA, CUF au CCM. Ni haki ya mimi--CHA the Omniscient, ni haki ya Mkuu wa Kijiji hiki--Dismas, ni haki ya dada yetu--Mama Malaika (ambaye analilia dual citizenship kwenye katiba ya sasa), ni haki ya Dixon, ni haki ya Angela na wengine wote wapendwa kuchagua ama kujiunga na chama chochote cha siasa. Hivyo kwa hawa wasanii kujiunga na CCM ni haki yao ya kimsingi; ila kwa wao kujiunga na CCM chama ambacho kupitia serikali yake kimeshindwa kutetea na kulinda haki zao, ni sawa na kuacha kanisa, ama msikiti kisha kujiunga na dini ya kishetani--ambayo mwisho wa siku  inasababisha maumivu ya kiroho na kimwili.

CCM (kupitia serikali yake) imeshindwa kuboresha maisha ya wasanii hawa kwa kudhibiti biashara haramu ya kazi za hawa wasanii. Kazi za hawa wasanii zimekuwa zinauzwa kiharamia hasa kwenye vituo vya daladala vya Mwenge, Ubungo, Posta, na maeneo mengine mengi ya kona mbalimbali za jiji la Dar Es Salaam, na maeneo mengine ya nchi.

Iwapo CCM ingeweza kudhibiti uuzwaji huu wa kiharamia; wasanii hawa ambao wengi wao wanaganga njaa, wangeweza kuwa matajiri, wangeweza kumiliki magari ya kifahari, wangeweza kumiliki majumba mazuri ya kuishi, wangeweza kuwa na vitega uchumi; mfano kumiliki  ma-hotel, wangeweza kumiliki hata media-house kama ilivyo kwa Youssor Nd'our na wengine kama hao. Na si tu hawa wasanii wangeweza kuwa na maisha mazuri, au kumiliki vitega uchumi, bali serikali ingeweza kukusanya mapato kupitia wasanii hawa, hivyo kuongeza pato la taifa.

Kwa kutokujua, ama kwa kutokujitambua, wasanii hawa wameungana au wameshawishika kujiunga na CCM--chama ambacho kinawatumia ili kitimize malengo yake, na mwisho wa siku kinawasahau au kuwatekeleza (sorry! nimekosea, ninamaanisha kuwatelekeza). Kwa hivyo wasanii hawa wamepotea njia, ama dira. Wasanii hawa wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii, wana akili lakini hawazitumii ipasavyo, wana midomo lakini hawawezi kuongea. Na kama wanafikiri au kuna mtu kawalaghai kuwa kujiunga na CCM kutapelekea wao, kuboreshewa maisha na CCM, nawaambia hivi kwa  kumnukuu Albert Einstein kuwa "THE SAME PROBLEM, CAN NEVER BE SOLVED BY THE SAME LEVEL OF THINKING". na "MAISHA BORA KWA WASANII HAWA WATANZANIA WALIOJIUNGA NA CCM, HAYATOLETWA NA MAFISADI WALEWALE KUPITIA CHAMA KILEKILE--KWA SERA ZILEZILE ZA ARI MPYA, NGUVU MPYA, NA KASI MPYA"

Mawazo au maoni yangu yaweza kuwa si sahihi mbele za  bin-adamu, ila yakawa sahihi mbele za Mungu. --Mwenye Macho Aone, na Mwenye Masikio Asikie.

Comment by KUNAMBI Jr on February 3, 2014 at 10:17

washaona ndo sehemu ya kutokea

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*