Tulonge

Rais Kikwete awakabidhi kadi za kujiunga na CCM baadhi ya wasanii maarufu Tanzania

Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wasanii mahiri wa Filamu hapa nchini,mara baada ya kuwakabidhi kadi za kujiunga na chama cha CCM kwenye maadhimisho ya  miaka 37 ya chama hicho huko Mbeya jana.

Katibu wa NEC, Itikadi,na Uenezi CCM Taifa,Nape Nnauye akiwatambulisha baadhi ya Wasanii nyota wa Filamu hapa nchini,ambao kwa nia thabiti wameamua kujiunga na chama hicho,wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB,Blandina Chagula,Mboto,Irene Uwoya,Single Mtambalike na wengineo.
Wasanii mahiri wa Filamu hapa nchini,wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB wakifuatilia yanayojiri hivi sasa ndani ya uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine,mkoani Mbeya juu ya kilele cha maadhimisho ya sherehe za miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho.

Mmoja wasanii Mwimbaji na Mwigizaji wa filamu,ajulikanae kwa jina la kisani kama Dokii akiimba mbele ya umati mkubwa wa wananchi na wanachama wa CCM waliofika kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama cha CCM,ndani ya uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine,mkoani Mbeya

JB akizungumza machace kwa niaba ya wenzake mara baada ya kutamka kuwa wamejiunga na chama cha CCM.

Wasanii hao wa Filamu wakifurahia jambo jukwaani.

Chanzo: Michuzi Blog

Views: 1203

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Christer on March 24, 2014 at 12:44

Uzalendo ni mgumu sana

Comment by Bonielly on February 11, 2014 at 11:03

nahisi labda jina langu lilijificha kwenye neno (na wengine wote) kilichoniuma kwanini ulimtaja angela mimi haukunitaja bora mimi na angela ungetuweka humo ndani, kwa wengine wote! aksante kaka dicked kwa kwa kaubagizi kako na wewe hujamtaja angela,

Comment by CHA the Optimist on February 10, 2014 at 16:58

Asante Dixon kwa kunisaidia. Maana Bonielly asingeniamini. Yaani sijui kwa nini Admin ali-delete jina lake kwenye maoni. Ha ha ha ha!

Comment by Dixon Kaishozi on February 10, 2014 at 16:51
Hahahaa.. Cha kwa kubagua bwana!! yani hakukutaja @Bonieli.. hahahaa...
Sasa nakutaja rasmi na namuonya Admin kudelete jina lako.. maana niniliona kwenye maoni ya Cha!!
Bonieli ukiwa kanma raia wa Tanzania.. una hakivya kidemokrasia kujiunga na chama chochote cha siasa ilimradi tu uwe umetimiza miaka 18 na kuendelea na una akili timamu.. haya sasa kazi kwako..
Comment by CHA the Optimist on February 10, 2014 at 16:24

Bonielly, sijui hata ilikuaje? Nilikuorodhesha na wewe katika maoni yangu ya  awali, sasa sijui Admin  (Dismas) amefuta kwa sababu zake anazojua, yaani ndo nashangaa sasa kutokuliona jina lako wakati niliorodhesaha. Tehe tehe tehe!

Comment by Bonielly on February 10, 2014 at 14:09

Kwanza nasikitita (cha) kunitenga bila ya kutaja jina langu na kumtaja angela, au sina haki ya kupenda chama? kwanini usinitaje bwana cha? haujui kama mimi na angela ni mapacha? usirudie tena siku nyingine, (NI UTANI TU) Unajua zipo stail za kujiunga na chama lkn sio hizi stail, zinaonesha kama ni usanii kwamfano, kama alivyosema bro dicked, kutoka dar hadi mbeya, je dar hawawezi kujiunga? (2)kwenda kundi zima kwa pamoja, je waonekane kwa rais? (3) siku zote walikuwa wapi? kwa kweli wachangiaji mliopita nimewaelewa, mimi mtazamo wangu, namuachia mungu, 

Comment by Dixon Kaishozi on February 7, 2014 at 18:06
Kaka nashukuru kwa kunielewa.. Na mimi nakuunga mkono kwa asilimia zote.. hawa jamaa wapo sahihi kabisa kujiunga na chama chochote na kwa wakati wowote.. na hiyo ndiyo demokrasia yenyewe.

Nimewaita mambulila kwa kuingiza usanii kwenye siasa. walicho kifanya ni usanii tu. wakati siasa nimaisha yetu yakila siku. Na kwa ulio wataja kama ulivyosema mpaka sasa wameshika uongizi flani maisha yasonge sasa hawa jamaa nao wameona huko ndiko kwa kutokea na ninauhakika hawajajiunga kutoka moyoni mwao ili kuikomboa hii nchi.
Comment by Mjata Daffa on February 7, 2014 at 17:56

Dix atakae kuchukia hajui maana ya democrasia, uko huru kusema unavyofikiri bila ya kuingilia uhuru wa mwinzio. BIG UP,

Lakini nakukumbusha kido msanii kujiunga na CCM siojambo geni, Hadija Kopa, Viki Kamata, Asha Baraka na wengine wengi walijiunga CCM na mpaka leo wako CCM tena wamekua viongozi.

Swali? hawajamaa umewaita mambulula kwa sababu wamejiunga na CCM? AU kwa sababu waingia kwenye siasa? maana kama nikuchanganya siasa na usanii ungeanza kumhoji Professor J alipojiunga na CHADEMA Last year.

ilakama nikuichkia tu CCM utakuwa sahihi kuwaita hawa jamaa Mambulula.

Comment by Dixon Kaishozi on February 7, 2014 at 10:41

Hawa ni mambulula.. sorry kama nitakua nimemkwaza mtu!.. Hapo wapo kwa masilahi zaidi.. Natolea mfano kwa msanii mmoja tu!! kwa wale waliopata nafasi ya kukumbana na tangazo moja alilocheza BABANA kupinga haya madudu ya serikali ya cccm inavyofanya Basi KAMWE HASINGEWEZA WEZA KUCHUKUA KADI NA KUJIUNGA NA CHAMA HICHO!!!

Walikua wapi siku zote? kuchukua kadi ilisubiri kwenye sherehe zilizofanyika mbeya ? wote wanatokea dar.. kwani kule dar kadi ziliisha ? huko ni kujitafutia umaarufu usio kuwa na tija.. na kama mwenzangu alivyosema hapo chini.. Kipindi hiki watatumika sana.. Kuna mahali nilisoma mgogoro ulio kwenye chama cha bongo movie kuhusu kupokea pesa ili wajiunge na chama tawala ambapo imepelekea mwenyekiti wao Steven Nyerere kuambiwa ajiuzuru..

Hamna kitu hapo!!! Msinichukie jamani na mimi ni mtazamo wangu tu!!

Comment by Wa Kimberly on February 6, 2014 at 23:15

Hao woote wapo hapo kisanii zaidi,ngoja watumike kwenye kampeni za uchaguzi mkuu ujao then tutasikia mapya juu yao.

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*