Tulonge

13, ni namba inayotumiwa na wanachama wa Freemasons,watambue Freemasons kupitia alama zao!kisha jiepushe nao!.

Yafuatayo ni matukio ya kihistoria,tukirudi nyuma miaka 700 iliyopita,ulikuwa ni wakati uliohusiana na watu kuwa na hofu kubwa iliyotokana na wao kuiogopa namba 13 !!!.

Hii ni namba ya kishetani ambayo dini ya Ufreemasons iliichagua kuitumia katika harakati zake na kuifanya kuwa namba yao ya kibahati,namba hiyo hutumiwa na wanachama wa Freemasons kote wanakopatikana duniani,utawatambua kupitia namba hiyo na namba zingine,pamoja na alama nyingine nyingi kibao kama hiyo ya Square and Compasses inayooenaka kwenye picha ya news hapo juu au hapa chini:

Namba 13 ni namba inayoundwa na namba mbili zifuatazo: Namba 10 na namba 3.Namba 3 (wao) huichukuliwa kuwa ni namba takatifu na namba hiyo ni sehemu ya namba 13,hivyo kwa kuwa namba 3 takatifu inapatikana katika namba 13,hivyo ikaifanya namba mzima (13) kwa ujumla kuwa na utukufu wa hali ya juu.
Namba 13 ni namba yenye umuhimu mkubwa sana kwa Freemasons.Na kwa mujibu wa kauli ya wataalamu waliozama katika sekta ya " Numerology " pamoja na Freemasons wanaamini kuwa namba 13 ni namba ya Mageuzi(mabadiliko).

Huamini kuwa namba hii 13 huwakilisha mambo mengi (wanayoyajua wao) ikiwemo kuwakilisha mageuzi kutoka Makoloni (mbalimbali) hadi Taifa Moja (The number 13 may represent the transformation from colonies to a united nation.)

Namba 13 imekuwa ni namba moja muhimu sana katika historia ya Marekani na hutumika sana katika alama ya mihuri.Marekani hutumia sana alama nyingi za Freemasons sehemu mbali mbali.Na ukitaka kujua ufreemasons umeingia marekani tangu zamani,hebu tizama historia ya Marekani,utagundua kuwa hadi sana ni miaka 300 tangu ufreemasons kuanza nchini Marekani.Naweza kuelezea kwa ufupi kama ifuatavyo:

Tangu Marekani ipate uhuru wake tarehe 4,JULY,1776, chini ya uongozi wa wakati huo aliyeitwa,John Hanson,Rais wa kwanza wa Marekani, ndipo athari na harakati za u-freemasons zilipoanza kuchukua nafasi yake.
Historia inasema baada ya uhuru huo ulianza kujengwa mji wa Marekani wenye umaarufu mkubwa nchini humo,nao ni Mji wa Washington DC,yakajengwa ndani yake majengo ya kisasa na makubwa yaani yale tunaita "babu kubwa" ambayo ni ya kiserikali, kama vile Jengo la Capitol,ni jengo lile lile alipoapishwa Rais Baraka Obama akikabidhiwa uongozi wa Taifa la Marekani!.

Jengo hilo utaweza kuliona katika Dolla za kimarekani,hebu tizama Dollar 50 ya kimarekani,utaliona jengo hilo linaloitwa Capitol.

Pia walijenga ndani yake jengo lingine linaitwa  White House na majengo mengine mengi yanayopatikana ndani ya mji huo wa Washington DC !!.

Mji huo wa Washington DC, umejengwa kwa mujibu wa Imani ya Ki-freemasons,umejaza alama kibao lakini si rahisi wa mtu wakawaida kuweza kuzitambua alama hizo,ila wao wanachama wanazitambua kama vile tunavyolitambua jua.
Kuna alama zingine kama vile Nyota,hizi nazo ni alama za kishetani za Ki-Freemasons,alama kama hii huwakilishwa na jengo  moja linaloitwa Pentagon,jengo hili kila pembe ina maana yake na kitu inachokiwakilisha katika dunia hii,pembe ya kwanza inamaanisha: MAJI, ya pili: MOTO,ya tatu: NCHI, ya nne: HEWA, na ile pembe ya tano huwakilisha: ROHO YA SHETANI.Na katika ramani ya mji wa Washington DC,Ikulu ndio pembe ya tano,lakini wewe usiyetambua utaona kwamba ni jambo la kawaida tu na hutajishughulisha na hilo kwa kulitia katika fikra zako,lakini wenywe wanajua alama hizo na kwa mujibu wa imani zao wanajua ni jinsi gani zinavyowasaidia.

Hii ni historia kwa ufupi kunako ufreemasons nchini State baada ya kupatikana kwa uhur.Kwa sasa watu hao wa dini hiyo ya kishetani wamefikia uamuzi waisambaze duniani kote kupitia mawakala wao,wanao watu wanafanya kazi hiyo chini chini ingawa wengine sasa wanafanya wazi wazi kazi hiyo na kujitangaza kuwa wao ni sehemu ya Freemasons.

Kwa sasa wanataka kuufikisha ufreemasons ndani ya Tanzania,na watanzania wasiotafakari utaona wanavamia fikra hiyo na kukubali pasina kujiuliza athari zake mbaya.utaona wakiningiza maalama ya freemasons katika vifua vyao,na kutumikia dini hiyo ya kishetani na kujiweka mbali kabisa na Muumba wa dunia hii muweza wa kila kitu.

Kuna watu wakubwa kwa Tanzania nao wamejiunga na dini hii ya kishetani,ni hasara kubwa kwa Taifa hili la Tanzania kuona watu hao waliohesabika na kuheshimiwa kuwa ni watu wa fikra na mtazamo pana,wakijiunga na dini za kishetani!.Wamepelekea sasa na wasanii kudumbukia sehemu hiyo ambayo mwisho wake ni Jahannam.

KATIKA SEHEMU YA KOMENTI,NITAKUJA NA PICHA YA MSANII MAARUFU WA TANZANIA ANAYEONEKANA KUTUMIA ALAMA ZA FREEMASONS (UKITIZAMA NGUO ZAKE),NA WATU HAWAKUJUA KATIKA UHAI WAKE KUWA ALIKUWA KATIKA DINI HIYO YA KISHETANI KWA SABAU SI WATAALAMU WA KUGUNDUA ALAMA HIZO ZA KISHETANI !!!!!!!

Ukitaka kutizama alama zaidi za Freemasons zinazotumika kwa dini hiyo,unaweza kukandamiza link hii: http://www.garone.net/tony/random.html

Na Chalii_a.k.a_ILYA

Views: 45879

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by ILYA on June 11, 2012 at 21:50

Diamond nae anaelekea sio kwenyewe!.Hebu tazama picha hiyo hapo juu:kisha soma maelezo yanayopatikana kwenye link hii:

http://www.globalpublishers.info/profiles/blog/show?id=5398006%3ABl...

Comment by ILYA on June 11, 2012 at 13:15

habiba mustafa mlawa@unasema unataka uhakika wa hayo mambo!.we ukitaka kupata uhakika wa mambo haya usiwafuate wale wengi unaosema wanadhani,kwa kuwa wengi wanadhani we wafuate wale wachache wasiodhani.Hebu soma kipande hicho hapo chini:

VIGOGO  WA FREEMASONS  KATIKA  UKANDA  WA AFRIKA MASHARIKI  NA AFRIKA  KWA UJUMLA
Sir.Andy chande ajitokeza na kusema kuwa yeye ni mmoja wa freemason afrika mashariki .Pia hakuwa nyuma kuwataja viongozi wanaohusika kwenye chama hicho akiwemo rais mstaafu wa awamu ya tatu Mh.Benjamin Mkapa .
Pia alimtaja steven kanumba, msanii nguli hapa Tanzania,Baba Riz raisi wa Tz,lowassa,AY,Mr. Blue,na wengineo wengi. Pia hakusita kumtaja yoweri museveni raisi wa uganda,Obama raisi wa marekani,George Bush,Bill Clinton,George washington,Elizabeth malkia wa uingereza na wengineo wengi.
Sir.Andy Chande alitaja yeye kwenye chama hicho ni Grand District Master akiwa amebobea kwa miaka 18 iliyopita.
Alipoulizwa makao yao makuu hapa Tanzania yapo wapi alijibu bila kusita "we are located at sokoine Drive behind kilimanjaro hotel here in Dar es salaam" (tunapatikana barabara ya sokoine nyuma ya hoteli ya kilimanjaro).
Pia Sir. Andy alisema wananyaraka zote za kumiliki jengo hilo toka serikalini. Aliongezea kuwa vikao vyao hufanyika kwa siri nyakati za usiku na mtu akishaingia kwenye chama hiko hatotoka tena
TUKUTANE  KATIKA SEHEMU YA TATU  AMBAPO   TUTAZUNGUMZIA  JUU YA MALENGO YA FREEMASONS NA UJIO WA "NEW WORLD ORDER".......,
ASANTENI.
-------------------------------------------
Kifungu hicho hicho cha maelezo ya kina kimetoka hapa katika link ifuatayo:
Comment by Christer on June 11, 2012 at 12:40

Eeeeh Mungu Tusaidie!!!

Comment by habiba mustafa mlawa on June 11, 2012 at 8:55

mh uhakika wa haya mambo sijui ni nani atakae tupa na tukamuelewa, hakuna mtu mwenye uhakika wa hayo mambo watu wengi wanakuwa wanadhani tu

Comment by Tulonge on June 11, 2012 at 0:01

Pa1 mkuu Ilya

Comment by ILYA on June 10, 2012 at 23:58

Namba za Freemasons ni nyingi sana,kuna namba 11,13,na 33,hizi ni namba zao zinazowatambulisha watu hao popote walipoduniani,lakini namba maarufu sana ni hiyo 13.

Na si mbaya kuzaliwa tarehe 13 kwani namba ni namba tu na hutumiwa na watu wote,ila we sema kundi linaweza kuchagua namba fulani likaitumia katika bishara zake za kishetani,ingelikuwa wao ndio waasisi wa namba kumi na tatu,basi hapo tungelimzungumzia anayezaliwa tarehe 13,lakini namba hiyo ipo kabla hata ya kuja huo ushenzi kuanza.Hivyo hakuna ubaya wowote mtu kuzaliwa tarehe 13 au kuzaliwa ndani ya jengo kunakofanyika ibada za watu hawa wa Freemason,unaweza kuzaliwa ukiwa umezungukwa na vitu kibao vinavyohusiana na Freemason lakini ukawa huna ishu yoyote na u-Freemason.

U-Freemason kama sijakosea katoka data zangu umeanzia Marekani lakini bado kuna watu huko Marekani wanaupinga kupita maelezo.

Comment by Tulonge on June 10, 2012 at 23:22

Sasa mkuu Ilya unasemaje kuhusu wale walio zaliwa tarehe 13?

Comment by Tulonge on June 10, 2012 at 23:21

Asante sana Ilya kwa habari ya kusisimua. Hilo la Kanumba hapo chini limenistua kweli.Kama ni kweli basi ni balaa tupu.

Comment by ILYA on June 10, 2012 at 17:26


Nimeeleza kuwa 13 ni namba ya kishetani,alama hii hutumiwa na wanachama wa kishetani,utawatambua kupitia alama zao kma hiyo 13 na zingine nyingi mno.Si ajabu wengi watashangaa kusikia au kuona aliyekuwa msanii Maarufu wa Kitanzania Kanumba kuwa nae alikuwa ni miopngoni mwa wafuasi wa dini ya kishatani.
Alikuwa akitumia sana alama za kishetani katika nguo zake anapo vaa.
Alipofariki Kanumba watu walitumia pasina kujua picha yake katika kumtambulisha,na picha hiyo ilitumika kwa kuwekwa mbele ya kitabu cha wageni ambapo wangeni wengi walikija na kutia saini zao za rambi rambi,pia picha hiyo iliwekwa mbele ya jeneza lake katika shughuli nzima ya kumuaga msani huyo.

Picha hiyo haikufaa kutumika katika sehemu hizo maana ni picha mbaya ilikuwa,kwa sababu ilikuwa inazungumza picha hiyo kuwa Steven Kanumba ni mfuasi wa dini ya kishetani.!.

Ukiitizama picha hiyo utamuona Steven Kanumba akiwa amevaa nguo yenye alama ya fuvu la kichwa cha binadamu,na namba 13,alama hizo mbili ni alama za kishetani na hutumiwa na wanachama wa Freemasons.

Lakini kwa kuwa watu hawajui alama hizi za kishetani,hawakuwa tayari kuichambua picha hiyo,laiti wangelijua mapema wasingeitumia picha hiyo.

Tanzania tuamke,tusiwe wepesi kukubali kupotezwa na hawa watu wanaotuletea dini mbaya za kishetani ambazo hazitamfikisha kokote mwanadamu tofauti na kumuweka mbali na Mola wake Muumba,na hakika watapata hasara wenye kujiunga na dini ya ushetani.

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*