Tulonge

Ahukumiwa kwenda jela mwaka mmoja kwa kumtumia SMS mbaya Waziri Nchimbi

Na Lydia Churi -- Mkazi Wa Mburahati Jogoo jijini Dar es salaam, Nassor Issa Mohamed (25) amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja au kulipa faini ya shilingi milioni tatu kwa kosa la kuwatumia ujumbe wenye nia mbaya wa simu ya mkononi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Emmanuel Nchimbi na Inspekta General wa Polisi Said Mwema.

Akitoa hukumu hiyo hakimu Helen Riwa wa mahakama Kisutu aliiambia mahakama kuwa Mohamed alisajili kadi zake za simu kwa majina tofauti na kwa mitandao tofauti kwa nia ya kutumia kadi hizo kutuma ujumbe wa simu wenye nia mbaya kwa viongozi hao.

Alisema mshtakiwa alikutwa akiwa na kadi ya simu yenye namba 0759 799956 ya Vodacom iliyosajiliwa kwa jina la Fadhil Issah, nyingine ya

Airtel 0687 521948 iliyosajiliwa kwa jina la Godfrey Joseph na kadi yenye namba 0687521947 ya Airtel iliyosajiliwa kwa jina la Fadhil Issa.

Hakimu Riwa aliitaka jamii kutumia kwa uangalifu mitandao kwa kuwa ni teknolojia mpya ambapo makosa yake yanakuwa ni mapya na sheria ni mpya. Alisema ametoa adhabu hiyo kwa kutumia Sheria ya Mawasiliano ya kielektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010 kifungu cha 132 ili iwe fundisho kwa wote wenye nia ya kufanya makosa kama hayo.

Awali Mwendesha Mashitaka Ladislaus Komanya aliiambia mahakama kuwa mnamo Mei 20 mwaka huu taarifa za kiinteligensia zilifikishwa kwa Maafisa wa juu wa jeshi la Polisi kuwa kuna mtu aliyesajili simu zake kwa mitandao tofauti anatumia simu hizo kuwatumia ujumbe mbaya wa simu ya mkononi Waziri Nchimbi na IGP na baada ya upelelezi ilipobainika kuwa namba hizo zilikuwa zimesajiliwa kwa majina tofauti.

Alisema iligundulika kuwa namba hizo zilikuwa zinamilikiwa na mtu huyo ambaye jina lake halisi ni Nassor Issah Mohamed. Alisema Mohamed alikamatwa Mei 25mwaka huu na baada ya mahojiano alikiri kumiliki kadi ya simu na kwamba ndiyo yeye aliyesajili namba hizo kwa mitandao tofauti akitumia majina tofauti ili kuficha utambulisho wake akiwa na lengo lakufanya uhalifu. Mshtakiwa alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Mei 27 mwaka huu na kukiri mashitaka

Via: wavuti.com

Views: 270

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*