Tulonge

Ala!,kumbe hii ndio siri ya umaskini Tanzania!!

Wataalamu wa masuala ya kiuchumi kutoka China na Vietnam wamesema kuwa, umasikini unaoikabili Tanzania pamoja na mambo mengine, unatokana na viongozi kuwa na maneno mengi kuliko vitendo.

Wataalamu wa masuala ya kiuchumi kutoka China na Vietnam wamesema kuwa, umasikini unaoikabili Tanzania pamoja na mambo mengine, unatokana na viongozi kuwa na maneno mengi kuliko vitendo.

Walisema hayo jana mbele ya Rais Jakaya Kikwete na kukosoa mchakato wa ubinafsishaji uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Tatu ambao umebinafsisha na kuua viwanda vingi vya msingi.

Aidha wachumi hao wamesema sera ya ubinifashaji viwanda nchini Tanzania haikutekelezwa kwa umakini unaotakiwa na matokeo yake viwanda vingi nchini humo vimekufa.

Profesa Do DucDinh wa Taasisi ya Kimataifa ya Uchumi ya Vietnam amesema inasikitisha kuona Tanzania ina kila rasilimali lakini ni masikini wa kutupwa.

Kwa upande wake, Profesa Li Xiaoyung wa Kituo cha Kimataifa cha Kuondoa Umasikini cha Beijing amesema maisha magumu yanayolalamikiwa na wananchi yanatokana na mfumuko wa bei hasa vyakula...

"Ugali ni chakula kikuu lakini bei ya unga ni kubwa ambayo wengine wanashindwa kumudu, unategemea nini?", alihoji mchumi huyo wa China.

Chanzo cha Habari:Kiswahili.irib.ir.

Na Chalii_a.k.a_ILYA

Views: 303

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Bonielly on March 30, 2012 at 16:04

machozi yananitoka kwa sababu hili lililoongelewa hapa ndilo lililo kichwani mwangu kila siku lkn sauti yangu ni nyembamba haiwezi kufika mbali, leo watanzania shughuli wanazozifanya ni ngumu kuliko,kipato ni kidogo majukumu ya hicho kipato ni mengi lkn waende wapi ili wasikilizwe? kila kona ukitaka haki lzm uwe na hela ya kuhonga, ili ununue haki, ukitaka upotelee giza sema ukweli, iko wapi tanzania ya mungu? wanakwenda wapi watu wa mungu? zinapotelea wapi mali za watanzania walizopewa na mungu? leo kiongozi mmoja anauza uhai wa watanzania anabinafsisha uhai wa watanzania, hajui samani ya wanzania, hajui kizazi kijacho kitaishi vipi kikikuta tanzania imebaki mashimo,

Comment by ILYA on March 29, 2012 at 22:52

Mkuu Tulonge@,unadhani unasema uongo,ni kweli kabisa viongozi wetu hawawezi kukubaliana na wewe kuwa hilo ndio tizo la umaskini kwa Bongo,watakuletea michongo mingine kibao.Ila hao wataalamu kutoka China na Vietnam wamenikuna sana maana wamelonga mbele ya Mheshimiwa Rais Jakaya,hii inamaanisha Mheshimiwa atajaribu kuwastua viongozi waache longolongo watende kazi kwa vitendo.

Comment by Tulonge on March 29, 2012 at 21:33

Nimeipenda hii mkuu, ila ukija waambia viongozi wetu watakubishia hadi ukome.Tena watabisha bila kufanya utafiti.

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*